Ni kwanini mimi sidumu

Ni kwanini mimi sidumu

Za leo marafiki na wapenzi wa jf
Za siku nyingi
Natatizo moja ni kwanini mimi nakuwa siwezi kudumu katika urafiki yaani nakuwa na mtu halafu mwisho wake sielewi mtu tu anakaa kimya tu mara yupo busy yaani mtu huelewi why hata kama wewe hajakutumia sijui why .
Naombeni ushauri ila sio pm hata hapa itasaidia pia.
Ukweli hili huwa linatokea. Yapo mazingira yanayoweza kupelekea haya kutokea.
1.nature ya mtu mwenyewe.
Yaani kuna watu mionekano yao wawapo na wenzi wao marafiki ni ya kikatili isiyo na hamasa. Sawa mtu huenda si muongeaji lakini akikutazama macho tu ukayaona unahamasika mno. Sura ya mwanamke pia hupotea kutegemeana na aliyotendewa maishani mwake.

2.tamaduni
Wengi huenda wasiamini. Migogoro ya kifamilia huathiri watoto ktk mahusiano wa kiume ama wakike. Asili ya familia iliyokuzaa wewe ikiwa haina baraka na furaha huambikiza karaha hizo kwa watoto kutofurahia maisha.

3.kutojikubali
Hii hali inawakumba wanawake wengi .Wanashindwa kujikubali wanajiona wana mapungufu hivyo wanajiingiza ktk mitindo ya ovyo ambayo inapelekea wanaume kuwaona ni wahuni tu. Mwanamke kujiremba ni vzr lakini kuna ujirembaji ambao haukubaliki mbele za wanaume tunakuona kama kahaba tu. Kila jambo lifanye kwa kiasi.

4.makila
Huu ni ugonjwa mbaya. Umevunja mahusiano ya wengi na umeua watoto sana. Ukiona migogoro na mpenzi na hating nyingi ujue yameota. Ukishayakata tu unakuta mahusiano yanakaa vizuri. Ufafanuzi wake ni mpana. Utakuta mtu hujamkosea au kosa dogo mno linapelekea hadi vikao talaka na usumbufu mwingi. Ujue ni hayo makila na yapo ya ndani yaonekanayo na yasiyooonekana.

5.Nyota
Ni mwonekano wako kwa watu, ucheshi, kupendwa na mengineyo. Hali hii inapishana kwa kila mtu. Kuna mtu hapendi kujitoa kwa ajili ya wengine ila anataka wengine wajitoe kwa ajili yake. Ujue kila upatacho kilipandwa bila wewe kujua. Lazima ubadilike.

6.uchafuzi
Unaweza kuwa unaishi mahali kumbe ulishafuliwa kwa sifa mbaya na wabaya wako bila wewe kujua na unakuta ni sifa ambayo wewe huna. Mfano watu wanaeneza taarifa kuwa ni mchawi, huwa anawateka wanaume kwa limbwata, ni mkopaji sana,mwizi, tapeli, ameathirika, ana mkosi wa kuua wapenzi,uchoyo, ni dhaifu huzimia penzini, ana kifafa na mengineyo. Huu tunauita ni uchafuzi ktk mapenzi.
7.ukatili
Unaweza kuta wewe ni katili kupita hata wanaume huna sauti laini kama mwanamke hupendi kushuka kama mwanamke. Ujue upole kuzidi siyo mzuri lakini ndiyo unaomfanya mwanamke bora aendelee kuwa bora.

8.yasiyojulikana.
Ni yale ambayo mimi na wewe hatuyajui lakini yanakufanya uwe kituko kwa wanaume.

Yote hayo juu yana tibika. La msingi ni wewe kujua ni lipi kati ya hayo linakugusa. Na pia yaweza kuwa zaidi ya moja pia yatosha uyafanyie kazi. Kuumizwa ni kawaida kwa kila kiumbe ila kuendelea kuvumilia maumivu ni uzembe wako mwenyewe.
 
Raise your game. Don’t let anybody lower your down. If you don’t learn to love yourself, nobody else will.
# listen to Whitney Houston ‘ greatest love of all’
 
Back
Top Bottom