tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,822
- 18,247
Katika maisha yetu ya kila siku kuna kusingiziwa na maonevu ya hapa na pale, hasa pale mtu unaposingiziwa kosa na hata kuadhibiwa bila sababu. Hii ni hali ya kawaida kabisa katika maisha kwa kuwa tunaishi katika dunia iliyojaa watu wa aina mbalimbali na wenye maamuzi anuwai.
Sio rahisi binadamu yeyoye yule asipitie hali kama hii akiwa shuleni, nyumbani au mtaani. Kwa mfano, binafsi nimewahi kusingiziwa na hata kuadhibiwa kwa makosa kadhaa mabayo sikuyatenda ng’o. Na hili sio kwangu tu, hata kwako pia huenda kwa namna moja au nyingine uliwahi kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukulitenda hata kidogo, lakini maisha yakaendelea kama kawaida. Ila kuna siku ukikaa chini na kutafakari unajisemea moyoni: “siku ile niliadhibiwa bila kosa masikini mie!!”. Inauma lakini unapiga moyo konde na kusonga mbele. Ndivyo maisha yalivyo.
Mimi nimewahi kusingiziwa mara kadhaa na kuadhibiwa bila shuruti kwa makosa mbalimbali ambayo sikuyatenda kabisa. Mosi, wakati nikiwa mtoto mdogo huko kijijini kwetu Mchambawima, niliwahi kusingiziwa kudokoa mboga nikaadhibiwa kulala bila kula na masimamgo juu kwamba, “umevuna ulichopanda nenda kalale na njaa ujifunze adabu njema”. Kwa kuwa niliadhibiwa na wazazi baada ya wao kujiaminisha kimakosa, sikuwa na namna bali kukubali adhabu bila shurti baada utetezi wangu kugonga mwamba.

Wakati fulani binadamu huvuta hisia nzuri na mbaya za wakati uliopita
Pili, wakati nikisoma shule siku moja kulikuwa na concert kule ukumbini. Siku hiyo sikuwa nafahamu kwamba kuna concert hivyo nikaenda zangu kule gallery kujisomea prep kama kawaida yangu. Ghafla akaja prefect mmoja na kuniuliza kwanini nimeingia kule gallery na kunituhumu kuwa nimeenda pale ili kutazama conert bila kulipia.
Nilijaribu kumfahamisha kuwa sikuwa nafahamu kuhusu uwepo wa concert yenyewe na hata conert yenyewe ilikuwa haijaanza. Ningesikia kelele za concert wala nisingeenda mle kujisomea. Pamoja na kwamba nilikuwa na madaftari ya kujisomea hakunielewa katu. Akanipeleka kwa mwalimu Mgimwa akanipa adhabu ya kuchimba kisiki nyuma ya bweni la Shaaban Robert East.
Niliamua kukubali yaishe kwa kuwa wakati huo maprefects wa Complex walikuwa wanajiona ni miungu watu. Nikaadhibiwa na maisha yakaendelea. Lakini kitendo kile kinaniuma mpaka leo. Yapo maonevu mengi ambayo nimewahi kuadhibiwa bila kosa, lakini kwa uchache nimeltaja haya mawili kama sample.
Ni dhahiri kuwa hata wewe kwa namna moja au nyingine uliwahi kusingiziwa au kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukuwa umelitenda lakini ukakubali kufunika kombe mwanaharamu apite. Hebu tuambie ilikuwaje na ulidahibiwaje.
Nawasilisha.