Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

okoyoko

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
2,664
3,639
Hello,

Nadhani most of us have all been there, maybe nduguyo kakupa zawad ya million 5, au dili zimekubali ukashika mpunga mrefu, au job ndiyo umepokea mshahara wako wa kwanza au maybe umepata boom la chuo for first time ndo unashika laki 6, ni kitu gani ulichokifanya kutumia hiyo hela mpaka baadaye ukajutia ukasema laiti ningejua nisingeitumia ile hela kivile.

Kuna ile euphoria au excitement mtu unapata unaposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza, ingawa wa2 tunatofautiana intesity za iyo euphoria. Mimi nakumbuka mara ya kwanza kushika hela nyingi haikumaliza hata wiki 2 I was broke mpaka machizi wakajua kuwa this guy is now flat broke; I guess nlikuwa Dallas ndogo kwa kipindi hicho..lol

Wadau tupeane uzoefu juu ya hili.
 
Nilinunu laptop kwa shilingi 470 naada ya kulpwa double mshahara...ila juz nmeiuza kuongeza fedha then nmenunua kiwanja.
 
Nashukuru Mungu huwa nikishika pesa ndefu huwa sinaga kile kimuhemuhe cha kutumia vibaya zaidi hukaa na kupanga nifanyie nini cha maana kwa faida.

Pesa ya kwanza kuishika ilikuwa bum la kwanza first year nikatumia kiasi kwa matumizi ya kawaida chuoni nyingine nikaweza nilipopata mabum mengine niksongeza na kufanikiwa kununua kompyuta nikiwa mwaka wa kwanza.
 
Last edited:
Nilienda duka la nguo kununua mitoko, kuns t-shirt fulani mpaka leo najuta kuinunua kwa gharama ile.
na jeans moja hivi bei ghali mpaka leo sijawahi kuivaa ni modo moja matata siipendi... vyote nimeviweka tu siku nikipata mda nitakuja kuvitoa as msaada kwa muhitaji.
 
Mie mpaka leo nikikumbuka najuta sana maana Nililala na madada wanaonizidi umri watatu kwa siku moja na kunywa vilevi vikali siku inayofuata na kulala kwenye mtaru nilishituka saa mbili asubuh tena kwa kushituliwa na watu wakijuwa nimekufaa,,,yani ndani ya siku mbili nikawa nimeshamaliza mil 1000,000/-,,Yani nikikumbuk huwa naumia sana
 
Nilisafiri mkoani kumfuata mwanamke Niliekuwa Nikiota kumpata mpaka Nikawa Naumwa. Tulitumbua raha kwa kuhama hoteli kadhaa za kifahari mkoa ule. Yaani ilikuwa Tukichukua chumba halafu Tv ikazingua au channel za Movies hazieleweki, kesho yake Tunatafuta hoteli kali zaidi na kitu cha kwanza kukagua ni Channels na ndipo mengine yanafuata.

Yaani hadi leo huwa Nadata sana na huyu mwanamke maana siinjoi hata kinywaji Nikikumbuka navyoinjoi kunywa nae. Nikarudi Dar bado haikutosha, Nikamtumia Nauli, breki ya kwanza Ilikuwa mitaa fulani inayoongoza kwa Bar na ukahaba hapa Dar ambako Tulikaa kwenye lodge moja kali sana kwa kama siku saba mfululizo Tukitoka night tu. Pesa inazuzua sana usipotulia ingawa binafsi Nachokumbuka ni matukio Niliyowahi kufanya kwa namna ya hatari sana kwa sababu sikumbuki mara ya kwanza kushika pesa nyingi aisee. Huyu Tuliefanya nae hizi vurugu ni mama wa baby wangu sasa na bado yuko ndotoni mwangu, it feels stupid and crazy sometimes.

Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kumfuata msichana Kampala ambako Tulitumbua pesa kama vichaa pia kwa wiki mbili. Ingawa Nilikuwa Naishi mwenyewe, Nahisi kosa nililofanya ilikuwa kutomuaga mtu yeyote katika familia yangu.

Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kile Nilichokifanya baada tu ya kutoka kuchukua pakee ya mgao wangu, Nikaenda Tigopesa, Airtel money na M-pesa Nikazijaza laini zote na pesa full. Nikabakiza kama M 1.5 mfukoni, Nikavuka na pantoni kigamboni kuja town. Hapo niko raugh kweli kweli, Nikamchukua taxi driver Nikamuuliza gharama ya kutoka pale hadi Bagamoyo ambako Nilimtanguliza mtu, aliponipa bei, Nikamwambia Tupite Sinza Nijafanye Shopping mpaka ya begi Nikatafuta lodge Nikaoga na kuchange, kisha Tukanyoosha mpaka Bagamoyo.

Kilichotokea ni kuwa pamoja na mbwembwe zote hizo, Tuliishia kutibuana na alienisubiri halafu Nikaharibu zaidi baada ya kutongoza mtu mwingine kwa hasira. In short Tuliishia kulala vyumba tofauti na kurudi kila mtu na njia yake. Ila utoto ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa.

Nina visa vingi ila hebu wengine wachangie.
 
Mie mpaka leo nikikumbuka najuta sana maana Nililala na madada wanaonizidi umri watatu kwa siku moja na kunywa vilevi vikali siku inayofuata na kulala kwenye mtaru nilishituka saa mbili asubuh tena kwa kushituliwa na watu wakijuwa nimekufaa,,,yani ndani ya siku mbili nikawa nimeshamaliza mil 1000,000/-,,Yani nikikumbuk huwa naumia sana
Kwanini uumie mkuu?
 
Mimi hela kubwa ya kwanza kushika ilikuwa ni ya Karo nikalipie adaya tangu form 3 had form 4 na michango yote...hapo imebaki kama wiki tufanye mtihani wa taifa kuhitimu. Basi jioni nikaenda zangu Villa Park (Mwanza), pembeni yake kuna Kiss Club...hizi nilikuwaga nazipita tu najiuliza humo ndani kuna nini, sasa ndo hivyo nimeshika hela...breki ya kwanza ikawa hapo. Actually, kabla sijatoka nikawaza kuwa hebu nisibebe hizi hela zote, ila nikasema aagh ngoja tu nizibebe zote ila ntatumia elfu 20 tu, aisee nimefika Villa Park mambo ikawa mambo...tena siku hiyo hiyo kanga moko walikuwepo kutoka Dar, kunwa sana...piga mademu ofa...nikamalizia kwenda kulala na malaya, asubuhi kumekucha nina mia 700 tu mfukoni...dah
 
Hii yako ni hatari sana aisee! Sijawahi kula ada ya sekondari aisee, Nilikuwa Naiogopa kama mahakama na mhalifu.
 
Back
Top Bottom