Sijawahi kupanda ndege, Mambo gani ya muhimu ya kuzingatia ukisafiri na ndege kwa mara ya kwanza?

impelle

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
832
1,100
Salaaam ndugu zangu,
Ninatarajia kusafiri kwa usafiri wa anga kwa mara ya kwanza kwenda ughaibuni, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutumia ndege, kwenye ticket inaonyesha nitabadilisha ndege mara tatu ndo ntafika mwisho wa safari.

Kwa hali hiyo naomba wale mlowahi kutumia huu usafiri mnipe walau hints za vitu muhimu vya kuzingatia kabla na wakati wa safari.

Nikifika nitawakaribisha sana, nitakaa huko miaka 3.
=======

Muhimu wahi, usikubali kupokea mzigo wa abiria yeyote mwingine, vitu vidogo vidogo kama passport na fedha weka kwenye hand luggage, usipack vimiminika kwenye hand luggage utaviacha vyote uwanjani wanapofanya ukaguzi.

Ukiona umeingia sehemu labda hawatumii kiingereza au kwa sababu ya maspika yale husikii vizuri hasa zile airport kubwa kama Schipol Amsterdam wewe kula sahani moja na abiria wenzako tu, utaongozana nao hadi kule waiting lounge au kama umefika mwisho kwenye mikanda ya kuchukulia mabegi na hadi kwenye exit.

Ndani ya ndege angalia usinywe juice ya tomato inaweza kukuzingua ukakosa raha ya safari nzima... pia hapo kwa kuwa kuna kupaa na kutua mara nyingi chukua bubble gums uwe unatafuna inasaidia masikio yasiumie.

Otherwise dude likishatulia kule angani ni kama tu uko sebuleni kwako unaweza hata kucheza kiduku... safari njema

Nimesoma jokes nyingi sana ila ngoja nikushauri kitu kidogo
1. I assume tayari umeshapata visa ya huko unakokwenda
2. Print kabisa ile ''invitation letter'' ya huko uendako na uwe na hard copy kabisa. Kama ukiweza unaweza kuprint hata emails exchange zinazonyesha safari yako. Kuna wapuuzi wanaweza kukuzingua huko mbele, hasa wakicheki rangi yako (it happened to me once..)
3. Uwe na kiasi flani cha fedha (US$/Any official currency inayotumika huko uendako) kwenye wallet yako. Tena tafuta recent notes. Kuna sehemu hawataki minotes ya zamani sana. Kuna wapuuzi wachache wanaweza kukuuliza kama una hela za kuanzia maisha kule au kukata ticket ya kurudi kama kuna la kutokea
4. Kwa kuwa utakuwa unachange ndege mara kadhaa, jaribu kuwa unacheki gate utakalopandia ndege na huchezi mbali na pale. Kuna baadhi ya gates pale Schiphol Amsterdam unaweza kujikuta umetembea angalau dakika 15 kulifikia
5. Usiwe na limzigo likuuuubwa. Usibebe vitu unnecessary - nguo wastani tu na vitu kama vitabu unaweza kununua huko au ukatafuta soft copies
6. Charge kabisa simu/tablet yako. You may need to use it along the way, au kama utakaa sana Airport.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera Mkuu Kwa kwenda ughaibuni, cha msingi ufuate maelekezo kuanzia nje hadi ndani ya ndege na haswa kwenye Viwanja utakavyobadilisha ndege, bila kusahau usiwe na mzigo mkubwa kama begi ndani ya ndege
 
unatakiwa uwanjani si chini ya dk 45 ,za ndege kuondoka kwa ajili ya check in na mambo mengine ya taarifa kuhusu safati.
 
Hongera Mkuu Kwa kwenda ughaibuni, cha msingi ufuate maelekezo kuanzia nje hadi ndani ya ndege na haswa kwenye Viwanja utakavyobadilisha ndege, bila kusahau usiwe na mzigo mkubwa kama begi ndani ya ndege

Hongera mkuu, kuna mwenzetu anaogopa kupanda ndege mwaka wa pili huu

Psalm 133:1 "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."

Hivi kwenda ughaibuni kunahitaji hongera??
 
Salaaam ndugu zangu,
Ninatarajia kusafiri kwa usafiri wa anga kwa mara ya kwanza kwenda ughaibuni, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutumia ndege, kwenye ticket inaonyesha nitabadilisha ndege mara tatu ndo ntafika mwisho wa safari.
Kwa hali huyo naomba wale mlowahi kutumia huu usafiri mnipe walau hints za vitu muhimu vya kuzingatia kabla, na wakati wa safari.

Nikifika nitawakaribisha sana, nitaakaa huko miaka 3.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inchi gani hyo unayobadilisha ndege mara tatu...na unaanzia safari wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom