Ni kiasi gani cha Kodi ulipiwa ukiingiza Body ya gari bila Chasis toka nje ya nchi???

Muhamala

Senior Member
Oct 1, 2017
101
88
Kwema wakuu.

Bila shaka mnamalizia wikiendi kwa utulivu kabisa.

Niende kwenye swali langu moja kwa moja kuwa hivi ninapo nunua/agiza body la gari bila chasis kutoka nje ya nchi kuja hapa nchini kwetu ni njia gani ya makadilio ya kodi hutumika ili kupata kiasi cha kodi kinachopaswa kulipiwa pindi body la gari linapokuwa limefika??? Naombeni msaada katika hili wakuu najua humu wapo waliowahi kuagiza body ya gari toka nje ya nchi.

Karibuni kwa michango yenu wakuu.
 
Mkuu hakuna utaratibu unaoeleweka, labda lipeleke uganda utalipia kama screpa then peleka gari yako uganda kavalishe bodi urudi.
Bonge la akili mkuu ila shida sasa hapo gharama inaongezeka.
 
Hii issue iliwasumbua sana Befoward mpaka wakaacha kuleta nose cut na baadaye kufunga kabisa warehosue yao ya spare pale Tabata. Hakuna mfumo maaalum it seems wa kucharge vipande vipande vya gari vinavyoingizwa nchini...
 
kuna kipindi darexpress waliagiza bodi za marcopolo hawakurudia tena sijui kiliwakuta nini!
Duuuh hapo majibu tushayapata kuwa walipigwa kodi ya kufa mtu. Sasa kwa mtindo huu watakosa mapato kwa watu wanaoogopa kuagiza wakihofia tozo kubwa la kodi
 
Kila mtu atafikiwa kisha wimbo tutaimba mmoja tu!!! Muda ni mwalimu mzuri sana
Fafanua vizuri mkuu wengine tumeishia darasa la 7D kwahiyo vichwa vyetu ni vigumu sana kunyambua mafumbo magumu kama lako :):)
 
Back
Top Bottom