Ni jinsi gani naweza kuishinda HOFU na WOGA?

May 25, 2016
63
45
Habari zenu wanajf,,,
Mimi mwenzenu ninakama wiki na kitu sasa nimekuwa nikiishi kwa hofu na woga sana,, nashindwa hata kuelewa in kwanini
Naombeni ushauri jamani namna ya kuishinda hii hali...
 
Pole, una tatizo lolote la kiafya? Kuna jambo linalokutatiza hujalipatia ufumbuzi??
 
Kuna mahali umeharibu, jikaze urekebishe mapema. Unavyoendelea kuogopa ndo unaongeza tatizo. Im talking from experience.
 
Uoga ni mental illness kuna magonjwa mengi sana ya akili takuwekea orodha yake.
Anxiety attack-:kwa jina lingine hii huitwa panic attack ni tatizo linalosumbua wengi na hutokea pasipo wewe kupenda yaani dalili zake ni kupata uwoga kama kuogopa kufa au kuhisi hupati pumzi ya kutosha hili ni janga la kitaifa na linaweza kupunguza nguvu kazi yako kama hujalitibu haraka.matibabu yake yanaitwa exposure au embrace your fear!
PTSD-POST TRAUMATIC STRESS DISORDER hili ni tatizo la akili huwapata sana watu kama wanajeshi au sehemu kwenye vita.
Yapo mengi mno matatizo ya kiakili ila naona uvivu kuandika na kufananua kiundani pamoja na tiba zake
 
huo ni ugonjwa unaitwa Anxiety. upo kundi la magonjwa ya kisaikolojia yaitwayo mood disorders. ni hali ya kuwa na wasiwasi bila sababu hususa. inaweza pelekea kupata panic attack. dawa zake zipo.
 
Hofu juu ya nini ???

Maradhi au .............. basi jua hakuna aliyekuja kuishi milele.
Madeni ...... sehemu ya maisha na jaribu kupambana nayo.
Maisha .......... waangalie wale uliowazidi wanaishi vipi?
Utapoteza kiungo cha mwili .............. waangalie waliopoteza kabla yako wanaishi vipi.
 
Kama kuna mtu umemdhulumu au umentapeli mtu......nenda kampe mali zake na umuombe msamaha ili upate amani ya moyoni.....

Kama kuna mambo unayafanya ya kiujanja ujanja hapo ofisini ili kujiongezea kipato haramu......achana nayo ili upate amani ya moyo......

Kama kuna mke wa mtu unatembea naye achana naye mara moja.......

Kama kuna mtu ulimkopa na unamzunguza kumlipa....mlipe mara moja.......

UKWELI UNAKUWEKA HURU......
 
Back
Top Bottom