Ni ipi mantiki ya kuwabana madereva mchana kwa tochi wakati usiku wanatembea mpaka 140km/h

Heron

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
1,946
1,798
Bado nimeshindwa kuelewa lengo la kuwabana watembee speed 50/60 mchana,
Halafu ikifika saa 12 jioni mnaondoka,
kuna Hatari kubwa sana kwani jamaa inapofika tu saa 12 huwa wanakuwa speed mpka inatia wasi,,
Can you imagine basi ya kwenda mwanza mmeibana kwa tochi mchana kutwa hadi saa 12 inamkuta yupo Dom, mnataraji nini afanye?
Hebu fikiria umbali wa kutoka Dodoma saa 18:30 kwa bus lakin saa 24:15 yupo Shy, tena usiku,

MY TAKE: KWA MAMLAKA HUSIKA,
Kama mmeamua kuwabana hawa jamaa mchana basi na usiku mfanye hivyo hivyo
 
Usiku kunakuwa hakuna watembea kwa miguu wanaovuka bara bara.... By the way usiku sirikali huwa inalala fofofo...
 
Bado nimeshindwa kuelewa lengo la kuwabana watembee speed 50/60 mchana,
Halafu ikifika saa 12 jioni mnaondoka,
kuna Hatari kubwa sana kwani jamaa inapofika tu saa 12 huwa wanakuwa speed mpka inatia wasi,,
Can you imagine basi ya kwenda mwanza mmeibana kwa tochi mchana kutwa hadi saa 12 inamkuta yupo Dom, mnataraji nini afanye?
Hebu fikiria umbali wa kutoka Dodoma saa 18:30 kwa bus lakin saa 24:15 yupo Shy, tena usiku,

MY TAKE: KWA MAMLAKA HUSIKA,
Kama mmeamua kuwabana hawa jamaa mchana basi na usiku mfanye hivyo hivyo
hatutaki ajari itokee mchana, bora usiku
 
kuna kingamuzi kimefungwa bila shaka sasa hawatakimbia wakati wote
Mchana tochi usiku trucking system
 
Kazi ya wenye mamlaka husika ni kusubiri tukio badala ya kudhiti vyanzo vyake kweli tochi zmepunguza mwendo kasi lakini zimefungua mwendo kubahatisha kufika salama maana jamaa wanafunguka sawaswa
 
Mi binafsi nkitaka kusafiri nasafiri usiku.... natembea nitakavyo na si watakavyo wengine, mwendo wa wastani Tena kwa umakini mkubwa
 
Tuna iomba serikali yetu sikivu ije na tamko kwasababu tunaelekea kupunguza ajali za mchana na kuongeza za usiku. Wakoloni wanasema "work done is equal to zero "
 
Kazi ya wenye mamlaka husika ni kusubiri tukio badala ya kudhiti vyanzo vyake kweli tochi zmepunguza mwendo kasi lakini zimefungua mwendo kubahatisha kufika salama maana jamaa wanafunguka sawaswa
Sijui huwa wanawaza nini badala ya kuboresha barabara wanabuni mbinu za ajabuajabu sana, nakumbuka nilitoka dar kwenda tabora yaani SAA 1 usiku ndio unafika singida lakn tulipoondoka tukawa tunakimbizwa kama punda, inabidi waliangalie hili kwa kina
 
Kama mnakumbuka tulikua na speedgavaner wakati barabara zenyewe zilikua gavaner tosha kumbe lilikua dili tu sasa sishangai siku zjazo ukaambiwa hata tochi nazo dili nadhani kwa mtazamo wangu mchana watu watembee tu halafu muda wa usiku slow kwa sababu hata dereva anakua kachoka hebu fikiria mtu kachoka anahitaji kupumzila sasa ndo umefika muda wa kufungua mwendo huku anasinzia gari liko 140 likiacha njia sekunde 5 karibu kilometa 2porini huko sasa ndo wenye bahati ya kuishi mtawajua
 
Wakati dunia inakimbia kuelekea maendeleo, Tanzania ndivo Kila kukicha ina kimbilia kunako kinyume na maendeleo.

Ndugu zetu wakenya safari za regional wise zifanyika usiku.

Ni kweli kwamba hatuwezi kufanya jambo la tofauti kupunguza Ajali hizo za bara bara pasina kuwa waambia watembee. 50/80 km/h kea mchana.?
 
Mkuu unahoja. Bus usiku zinakimbia zaidi ya ndege. Kwa mfano bus linaweza kutoka singida saa moja jioni likafika mwanza saa 5 au 6 usiku. Wakati kama ni mchana linatoka mza saa 12 linafika singida saa 8.
 
Sahihi mkuu, na hiyo mimi nimeishudia juzi jumamos,
Hebu jaribu kufikiri kwa akili ya kawaida
Dar-Arusha 616+ km, Bus inatoka Dar saa 12 mpka saa moja jioni haijafika Chugga,

Hebu waache drama, yaani hata kama wangekubaliana Bus zitembee 80 Km/h. Bado bus zingetumia only 15hrs ambapo zingefika mwanza saa 21 usiku,
Tofauti na sasa inatumia 17 to 18 hrs,kisha asubuhi igeuke!!! Service imefanyiwa saa ngapi? Madereva wamepumzika saa ngapi?
Tanzania bana yaani utafikiri kila kitu kipo kwenye majaribio, kumbe ndo life style
 
Back
Top Bottom