Subiri muda si mrefu atakapokuwa waziri uje tena na ushuhudaWakuu, mwezi mmoja nyuma nilikutana na msafara Mwenge wa kufa mtu, msafara uliokuwa unaelekea Ubungo ukiwa na Magari zaidi ya mia moja yakiwa yamesheheni polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi, Usalama wa Taifa, makada yote ya wanaCCM Dar, vigogo wote wa serikali Dar, msafara uliokuwa na mbwembwe za kila aina na ving'ora vya kuogofya.
Msafara huo uliokuwa na polisi wa lining'inia pembeni mwa milango ya Magari na brigedi ya UVCCM, ulikuwa unaelekea Ubungo kwa kupita hiii barabara ya Mlimani City, ni moja ya misafa yenye mbwembwe na ya hatarii niliyowahi shuhudia katika maisha yangu iliyokuwa na idadi kubwa ya Magari na watu walining'inia kwenye milango ya Magari ikijumuisha speed ya kukimbia na ving'ora vyenye sauti ya kuogofya.
Wakuu, leo hiii nimekutana na makonda akiwa hana mlinzi, hana ving'ora wala wasaidizi akionekana mtu wa kawaida na mwenye woga woga akiwa anatazama huku na huku kwa kupitia miwani dizani ya wale wazee wa kuangalia watu kwa kutumia kwenye upenyo wa juu ya miwani yaliyovaa wakisingizia kuwa miwani wamevaa kwaajili ya kusomea tu.
Wakuu ilibidi nifute vizuri vumbi kwenye uso Wangu ili niweze kuona kama kweli mtu huyu anaeonekana mbele yangu ni Makonda au nimepata shida ya macho niligundua kuwa ni yeye, ilinibid nipige simu kwa mmoja wa watu tuliokuwa nao siku ile ya ule msafara kuuliza kuwa hivi ule msafara ulikuwa ni wamakonda kweli? Akanihakikishia kuwa alikuwa yeye.
Wakuu, leo ndio nimegundua kuwa kweli lile somo nililofundishwa kule Msalato Secondary School kwamba dunia inazingua katika muhimili wake ni kweli.
Wakuu, tumuachie MUNGU kwa kila jambo hapa duniani yeye ndie anaejua muda siku na saa, maisha tunayoishi hapa duniani ni record ya mchezo wa mpira tulioucheza uliokuwa unatazamwa na mwenyezi MUNGU pekee na ndie anaelewa mwisho wa matokeo ya mpira uliochezwa na kila mmoja wetu, daaah!
Kupitia huyu bwana lazima watawala wajifunze kitu hapa, kuna kitu MUNGU amekionesha kupitia kwa huyu makonda ila wenye uwezo wa kuelewa wataelewa na wenye uwezo mdogo wa uelewa hawataelewa kilichotokea ila MUNGU hapa alikuwa na maaana yake, ujue MUNGU anaweza kukushusha chini kwa muda wa siku moja tu au week tu kwa nia ya kukuonesha kitu au kwa nia ya wenzio kujifunza halafu baadae akakupandisha.
Lazima tujifunze kuhusu madaraka kuwa ni dhamana maaana huyu walifika mahali wakasema kuwa anamadaraka kumzidi Waziri Mkuu pasipo kujua kuwa Waziri Mkuu hata akistaafu atalindwa maisha yake yote.