broken ages
JF-Expert Member
- Mar 23, 2012
- 235
- 84
Ninachokiona ni kwamba watu hawajaweza kufikiri na kutafakari kwa umakini na wengi pia wanashindwa kutambua ikiwa ni habari zipi za kuamini kwani habari ni nyingi za uongo na uzushi ambao unaosemwa kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari na watu ambao ni wapotoshaji pengine kwa maksudi ama kutokuelewa kwa habari ya chanjo ya Covid 19.
Watu ambao wameaminiwa na watu wengine na ambao ndo walipaswa wawe ni ambao wangeweza kuelimisha jamii juu ya habari ya chanjo ya Covid 19 wamegeuka kwamba ndio wenye kupinga na wakati wakipinga chanjo kwa nguvu zao zote pia hawatoi suluhisho la nini kifanyike ili watu wasiendelee kufa kwa kasi kubwa kama inavyotokea kwa sasa ndani ya Tanzania na duniani.
Na hawatoi pia uthibitisho wa nani alifanya covid vaccine akapata madhara gani ama changamoto zipi ndiyo maana mimi naita huu kuwa ni upotoshaji kuwaambia watu wasichanje.
Kwa sababu wengi tumeshuhudia madhara yatokanayo na kuugua covid tumeshuhudia kwa kuwapoteza marafiki,ndugu ama jamaa ambao wameugua Covid na hata kama aliugua mtu akawa ametibiwa na kupona lakini pia ni kwa bahati sana kwa sababu tu rehema na huruma ya MUNGU ilikuwepo juu ya mtu huyo hii ni tofauti na kwamba upande wa pili wa waliochanja ambao kutokana na chanjo hatujayaona madhara yaliyowapata ndugu zetu jamaa ama marafiki.
Tutakuwa pia hatujafikiri vizuri ikiwa tutakubaliana na mtu atakayetuambia kwamba chanjo inayo madhara kwa sababu hatuna uthibitisho wa nani alichanja na ikamdhuru vipi.
Ninachokiona na kwa sababu ya shuhuda tulizopata kupitia ugonjwa wa Covid 19 ni kwamba ni heri tuchanje tupambane na Changamoto kama zingejitokeza za kuchanja kulikoni kupambana na changamoto za kuugua Covid kwa sababu inaonekana kwamba ni nguvu Kubwa sana kupambana na changamoto kwa mtu anayeugua Covid 19.