#COVID19 Ni heri kupambana na changamoto za chanjo kuliko kupambana na changamoto za kuugua COVID-19

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
223
225
Ninachokiona ni kwamba watu hawajaweza kufikiri na kutafakari kwa umakini na wengi pia wanashindwa kutambua ikiwa ni habari zipi za kuamini kwani habari ni nyingi za uongo na uzushi ambao unaosemwa kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari na watu ambao ni wapotoshaji pengine kwa maksudi ama kutokuelewa kwa habari ya chanjo ya Covid 19.

Watu ambao wameaminiwa na watu wengine na ambao ndo walipaswa wawe ni ambao wangeweza kuelimisha jamii juu ya habari ya chanjo ya Covid 19 wamegeuka kwamba ndio wenye kupinga na wakati wakipinga chanjo kwa nguvu zao zote pia hawatoi suluhisho la nini kifanyike ili watu wasiendelee kufa kwa kasi kubwa kama inavyotokea kwa sasa ndani ya Tanzania na duniani.

Na hawatoi pia uthibitisho wa nani alifanya covid vaccine akapata madhara gani ama changamoto zipi ndiyo maana mimi naita huu kuwa ni upotoshaji kuwaambia watu wasichanje.

Kwa sababu wengi tumeshuhudia madhara yatokanayo na kuugua covid tumeshuhudia kwa kuwapoteza marafiki,ndugu ama jamaa ambao wameugua Covid na hata kama aliugua mtu akawa ametibiwa na kupona lakini pia ni kwa bahati sana kwa sababu tu rehema na huruma ya MUNGU ilikuwepo juu ya mtu huyo hii ni tofauti na kwamba upande wa pili wa waliochanja ambao kutokana na chanjo hatujayaona madhara yaliyowapata ndugu zetu jamaa ama marafiki.

Tutakuwa pia hatujafikiri vizuri ikiwa tutakubaliana na mtu atakayetuambia kwamba chanjo inayo madhara kwa sababu hatuna uthibitisho wa nani alichanja na ikamdhuru vipi.

Ninachokiona na kwa sababu ya shuhuda tulizopata kupitia ugonjwa wa Covid 19 ni kwamba ni heri tuchanje tupambane na Changamoto kama zingejitokeza za kuchanja kulikoni kupambana na changamoto za kuugua Covid kwa sababu inaonekana kwamba ni nguvu Kubwa sana kupambana na changamoto kwa mtu anayeugua Covid 19.
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,888
2,000
Umenena vema mkuu. Mimi nimechanjwa yapata siku 12 hadi sasa na sijapata madhara yeyote. Niko fiti bin ngangari na furaha tele moyoni.
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,163
2,000
Unazungumzia changamoto za chanjo( ambazo hazijulikani) au unazungumzia maudhi madogo madogo tu ya chanjo ambayo huduma kwa muda mchache tu na kuisha?

Tuwekane sawa hapo.
 

Zenis

Senior Member
Mar 28, 2021
147
250
Kubali dunia iko kwenye utafiti wa tatizo, haiwezekani watu wote wawe sample za utafiti. Waliochanjwa wanatosha kuwakilisha . Tukutane baada ya utafiti
 

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
223
225
Kubali dunia iko kwenye utafiti wa tatizo, haiwezekani watu wote wawe sample za utafiti. Waliochanjwa wanatosha kuwakilisha . Tukutane baada ya utafiti
Tutakutana tu iwapo wewe na ambao mnaopinga mtakuwa hamjadhurika
 

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
223
225
Unazungumzia changamoto za chanjo( ambazo hazijulikani) au unazungumzia maudhi madogo madogo tu ya chanjo ambayo huduma kwa muda mchache tu na kuisha?

Tuwekane sawa hapo.
🤝Ni kweli ni vimaudhi vidogo vidogo na ndiyo maana nikaeleza kwamba ikiwa zitatokea changamoto maana hadi tunapoongea haijajitokeza changamoto yeyote yenye kusababishwa na chanjo
 

4IR

JF-Expert Member
Apr 21, 2014
1,007
2,000
Naona kila mtu ameamua kuwa mtafiti na mshauri wa chanjo. Ukichanja hatuna haja ya wewe kutujulisha na usipochanja iwe hivyo pia. Mambo ya kuandika yapo mengi tu. Zungumzia hata shughuli zako kiuchumi, watu tule madini muhimu.
Note: sikupangii uandike nini, ni ushauri tu.
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,163
2,000
🤝Ni kweli ni vimaudhi vidogo vidogo na ndiyo maana nikaeleza kwamba ikiwa zitatokea changamoto maana hadi tunapoongea haijajitokeza changamoto yeyote yenye kusababishwa na chanjo
Na unaweza usisikie kabisa japo wenyewe wanasema hakuna chanjo isiyo na side effects.
 

Zenis

Senior Member
Mar 28, 2021
147
250
Tutakutana tu iwapo wewe na ambao mnaopinga mtakuwa hamjadhurika
Lakini wasilazimishe kucheza na sampling outside scope range.
Research itavurugika.
Imagine hao sample group waki mutate negatively? The case will be catastrophic.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom