Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,863
- 5,694
Hivi najaribu kujiuliza maswali ya kifasaha kwa swala hili la bomoa bomoa linalo endelea hapa Dar sipati majibu.
Hivi najiuliza serikali ilifikiri kwanza madhara ya ubomoaji huo holela kwa wananchi kabla hawaja tekeleza?
Kama walifikiri vizuri ni kwa nini walianza kubomoa halafu wakasitisha zoezi?
Huhitaji Elimu ya chuo kikuu kujua serikali imevunja haki za raia wake. Wameona machozi ya wanyonge yakibubujika kwa kubomolewa vibanda ndipo hisia ikawapata kuwa hawatendi haki kwa RAIA wake tena wema.
Wakagundua kuwa iliwapasa kuweka utaratibu mzuri kabla ya uhalifu huu kutendeka.
Lakini tayari watu wamepata madhara makubwa kwa utendaji huu unaotumia nguvu kwanza halafu akili ifuate.
Leo umewavunjia baadhi ya watu nyumba wakiwa makazini na kupoteza mali zao halafu wengine unawapa muda wajiandae kweli ndo utawala wa sheria huu?
Kimsingi watendaji wengi Wa awamu hii wataleta madhara makubwa kwa taifa kuliko tija.
Hawana ubunifu wa strategic plan za kuongoza badala yake wanazurula na waandishi wa habari kutuonesha wamefanya ziara za ghafla au wamesimamisha watu kazi.
Tukiendelea kuchekea utendaji Wa namna hii lazima tujiaandae kulipa fidia mabilioni ya pesa lakini yapo madhara mengine hayana fidia kwa kuwa yanaweza kuleta vifo au magonjwa yasiyo lazima.
Madiliko tuliyoyataka sio ya kubomoa na kuharibu mali tulizo hangaikia kwa miaka mingi bali kuongeza utajiri.
Kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Wasalaam.