Hili swali limekuwa likinitatiza siku nyingi, lakini nadhani sijui neno "kustaafu" maana yake ni nini. Hivi ni kweli pamoja na kashfa zote alizofanya na anazoendelea kufanya mpaka akalazimika kujiuzulu tunapashwa kumwita EL kwamba ni PM Mstaafu?
Nilidhani atafutiwe sifa nyingine, siyo hiyo. Je, tukimwita mstaafu, tutatumia sifa gani kwa Marehemu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi, Marehemu Kawawa, Warioba, Sumaye nk.
Naomba michango yenu ya mawazo ili hatimaye tupate sifa inayoendana na na ufisadi wake.
Nawakilisha.

Mkuu,Ila ninachojua ni kwamba hata hao tunaowaita 'wastaafu PM'...sidhani kama kweli walistaafu. Kiukweli katiba yetu si nzuri.
Kustaafu ni hali ya mtumishi kufikia ukingo wa kutumika (kiumri) na kwamba hastahili kuendelea na nafasi yake hivyo kuhitajika 'kustaafu'. Ukitazama kwa undani...mawaziri wakuu wote hakuna hata mmoja katika nchi hii (PM) aliyefikia hatua ya kwamba mimi ninastaafu, NI BABA WA TAIFA TU NDIE ALIYEFIKIA HATUA AKIWA RAIS KUTAMKA KUWA SASA 'ANANG'ATUKA', waliosalia ni aidha muda wao wa ukomo umefika (kwa mujibu wa aliyemteua) au wamebadilishwa na wakuu wao kwa sababu za kiutendaji kwa manufaa ya UMMA na si kustaafu.
naombeni mnisahihishe kama nimepotoka,
NAWASILISHA.
Mzee wa kufyatuka!Unatulipia broadband?? nenda zako motoni.
Waziri Mkuu wa ZAMANI
Lowassa ni Waziri Mkuu aliyefukuzwa Kazi.