Ni halali ndg Edward Lowassa kuitwa 'Waziri Mkuu mstaafu'?

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Hili swali limekuwa likinitatiza siku nyingi, lakini nadhani sijui neno "kustaafu" maana yake ni nini. Hivi ni kweli pamoja na kashfa zote alizofanya na anazoendelea kufanya mpaka akalazimika kujiuzulu tunapashwa kumwita EL kwamba ni PM Mstaafu?

Nilidhani atafutiwe sifa nyingine, siyo hiyo. Je, tukimwita mstaafu, tutatumia sifa gani kwa Marehemu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi, Marehemu Kawawa, Warioba, Sumaye nk.

Naomba michango yenu ya mawazo ili hatimaye tupate sifa inayoendana na na ufisadi wake.

Nawakilisha.

Nimeshangaa sana na bado nitaendelea kushangaa na isitoshe serikali ya chama cha mapinduzi kwenye taarifa zenu za habari kuupotosha uma wa watanzania kua eti Eduward Ngoyai Lowasa ni waziri mkuu msaatafu hii ni aibu na sintakubaliana na vyombo vya habari TBC1/Gazeti la Uhuru/Gazeti la Habari leo na viombo vyoote vinavyomilikiwa na serikali ya CCM kuupotosha uma wa watanzania kuhusiana na habari hii husika hapo juu!

Taarifa ya habari ya tarehe 23/10/2011 saa mbili ya usiku nimeona na nimeisikiliza na kumuona bwana Lowasa AKA Nywele Nyeupe akiwa kanisani sijui alikua anatoa rambirambi au alikua anapata maombi kama tulivyomzoea kipindi hiki tokea ajiuzulu na sio amestaafu haachi kuhangaika na makanisa tofauti akitafuta maombi kutokana na imani yake sasa hivi! Eti chombo hiki cha habari cha taifa kuutangazia uma kua waziri mstaafu ndugu Eduward Lowasa! Amesema blablabla na sijui nini!

Tafadhali sana watu wa TBC1 na vyombo vyombo vingine natoa tamko kuwa nitavichukulia sheria za kinidhamu kwa kuupotosha uma kwa kutamka kauli hii! kuanzia sasa nitaweka wanasheria wangu kama nitasikia tena kua mnatamka kua bwana Eduward Lowasa ni waziri mstaafu!

Nataka vyombo vya habari vitamke kua Ndugu Edward Lowasa ni aliyekua waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza ya raisi Jakaya Kikwete na akajiuzulu kwa kashfa ya Richmond na kuwasababishia watanzania kukaa kwenye kiza kinene mpaka sasa hivi! Wanasheria wangu wako tayari kwa chombo chochote kama nitasikia tena kauli kama hii.
Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalili vya TBC almost zote (radio $ TV),na wamekuwa wakisisitiza ukweli na uhakika pamoja na kuweka utaifa mbele kwa maendeleo ya Tanzania, ijapokuwa makosa mengi yanaonekana lakini hili si kosa ni tatizo ambalo linakinzana na kauli mbiu yai ya ukweli na uhakika.

Kitendo cha kutuambia kila siku Lowassa ni waziri mkuu mstaafu si kweli!

Nani asiyejua Lowassa alijiuzuru kwa kashfa nzito na akaatamka mwenyewe bungeni kuwa anaachia ngazi? Hilo TBC hawalijui au bado wanaamini alisingiziwa?
 
Huyo si mstaafu.Ni makosa kumwita mtu aliyelazimishwa kujiuzulu kuwa ni mstaafu.Waandishi wengi hasa wale wa upande wake wanapenda kumwita waziri mkuu mstaafu.Hivi leo hii kama Kikwete angeng'oka madarakani tungemwita mstaafu wakati bado hakutaka kustaafu kwa hiari yake ila wananchi wamemstaafisha?Aliyestaafu ni yule aliamua kwa matakwa yake mwenyewe na vinginevyo.Chukulia mfano wa Malecela kule Mtera alitaka ubunge tena lakini wananchi wakagoma kwa njia ya kura ya maoni.Huyu tunaweza kumwita mbunge mstaafu?Hapana.Waziri mkuu aliyejiuzulu.Ndilo jina halisi hapa.
 
Mie nililiona hili katika sherehe za kuapishwa JK nikashangaa lini Lowassa amestaafu? Au niulize vizuri ni lini Lowassa alitumikia cheo chake hadi akastaafu? Kama jibu ni hapana basi kwanini aliwekwa pamoja na akina Msuya, Sumaye, na wengineo kwani asitolewe maana yeye ni waziri aliyejiuzulu au kutaka kufukuzwa na bunge. Ila ndio Tanzania yetu.
 
kama mwinyi ni mstaafu, mkapa naye pia, jk very soon, kwa ufisadi ambao hawa jamaa waliufanya mnategemea watadeclare EL si mstaafu? and who has the power to declare that?
 
kumuita mstaafu si mbinu tu za ccm kumlinda ili aendelee kupata benefits na heshima za mawaziri wakuu wastaafu.yule ilibidi apotezewe mazima
 
Pamoja na hayo, pia kustaafu siyo kuachia ofisi kwa hiari tu, kwani wengine hustaafu kwa mujibu wa sheria , say 60 years kwa watumishi wa umma, rais kutoweza kuwa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka 5 kila kimoja
 
Hili swali limekuwa likinitatiza siku nyingi, lakini nadhani sijui neno "kustaafu" maana yake ni nini. Hivi ni kweli pamoja na kashfa zote alizofanya na anazoendelea kufanya mpaka akalazimika kujiuzulu tunapashwa kumwita EL kwamba ni PM Mstaafu?

Nilidhani atafutiwe sifa nyingine, siyo hiyo. Je, tukimwita mstaafu, tutatumia sifa gani kwa Marehemu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi, Marehemu Kawawa, Warioba, Sumaye nk.

Naomba michango yenu ya mawazo ili hatimaye tupate sifa inayoendana na na ufisadi wake.

Nawakilisha.

Tena kama anaendelea kupata masurufu yoyote yale ambayo wanapata Mawaziri wakuuu wastaafu inabidi yasitishwe, ningeshauri wanasheria waangalie hili na kumshtaki manake ni ubadhirifu mwingine huu wa kodi zetu.

Hakustaafu hivyo hatakiwi kuchukuliwa hivyo. Ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa period!!!

Wanasheria pls jamani..... tunaibiwa!!!
 
Pamoja na hayo, pia kustaafu siyo kuachia ofisi kwa hiari tu, kwani wengine hustaafu kwa mujibu wa sheria , say 60 years kwa watumishi wa umma, rais kutoweza kuwa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka 5 kila kimoja

Usijaribu kumsafisha wala kumtetea. Tusaidie kama unataka kumtetea Lowassa alipoondoka madarakani kipindi chake cha utumishi wa waziri mkuu kilikuwa kimefikia ukomo? Haya uliyotaja yote yanalenga ukomo wa kuwa waziri mkuu but Lowassa alipojiuzulu alikuwa bado ana umri wa kuendelea kuwa madarakani, rais aliyemteua alikuwa bado rais hivyo angelitaka kuendelea angelikomaa tu akaendelea. In short yule ni waziri mkuu aliyejiuzulu au kutaka kufukuzwa na bunge (nikinukuu maneno ya Dr Mwakyembe).
 
Tatizo ni waandhishi wa habari....................... Hawajui namna ya kuandika au wanaogopa kumwandika kama waziri mkuu wa zamani (Former PM). Na kama kweli anapata mafao then huo utakuwa ni ufisadi mwingine.
 
Wanamme wanapojadiliana na kuweka records straight mama kama wewe kazi yako ni jikoni kuandaa kahawa,sawa mrembo?

Mkuu mwonee huruma pengine akili zake ni kama yule aliyesema kuwa Lowassa ni mwanaume wa shoka kushinda wanaume wengine sasa sijui alikuwa anamaanisha nini!!!!!
 
GrEatThinkers,

Huo ni uzumbukuku kuburuzwa kila kitu hata kifikra.

Wote mnajua alifukuzwa kazi na Watanzania kupitia kamati ya bunge letu.

Wote mnajua alitamka:

"Nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana, nimetukanwa

Sasa kama tatizo ni uwaziri mkuu nimeamua kuachia ngazi"

Mpuuuzi gani aliyesikia kuwa alistaafu kwa sababu ya maradhi au Uzee?

Hayo ni madudu ya TBC na matumizi mabaya ya Shirika letu, wamnampamba mno.

Nijuavyo mimi alifukuzwa kazi. FINAL:peep:
 
mi nadhani wakitakiwa nguruwe huwezi kupeleka kondoo
maana aliyejiuzuru na aliyestaafu ni tofauti,
sawa na mwanafunzi aloacha shule kwa mimba na aliyehitimu
 
mamvi haja staff ila tamaa zake za ufisadi ndio zilizo mponza. Huyo mamvi wala hastahili kuitwa mstaafu na pia yupo kwenye shortlist ya iron hand(nyundo ya kuwatokomeza mafisadi)kama sijakosea yeye ni no.4 na muda muafaka ukifika mmoja mmoja atakufa kifo kibaya sana. VERY PAINFUL DEATH zaidi ya patrice lumumba na merkiol ndandaye. Wataona tu.
 
mamvi haja staff ila tamaa zake za ufisadi ndio zilizo mponza. Huyo mamvi wala hastahili kuitwa mstaafu na pia yupo kwenye shortlist ya iron hand(nyundo ya kuwatokomeza mafisadi)kama sijakosea yeye ni no.4 na muda muafaka ukifika mmoja mmoja atakufa kifo kibaya sana. VERY PAINFUL DEATH zaidi ya patrice lumumba na merkiol ndandaye. Wataona tu.
 
Back
Top Bottom