Ni halali kuchagua viongozi washirikina? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni halali kuchagua viongozi washirikina?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jile79, Oct 28, 2010.

 1. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Tangu sheikh yahaya ajipambanue kwa watanzania kuwa yeye ndiyo mchawi na mlinzi mkuu wa kikwete kwa kutumia majini, si kikwete wala makamba wala kinana wala riziwani wala salma kikwete aliyekanusha ulinzi huo wa kichawi wa yahaya kwa kikwete....Kwa Tanzania ya sasa ni sahihi kweli kumchagua kiongozi wa nchi mshirikina na ambaye yuko tayari wananchi wake watishwe na mganga wake?
  "HERI WASIOENDA KATIKA NJIA YA WASHIRIKINA"
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kuona nchi imeendelea kwa wananchi wake kutishwa na wachawi wa viongozi wao.......ni tanzania tu ambako tuna viongozi mambumbu
   
 3. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Na hili ndilo linalonishangaza sana

   
 5. x

  xman Senior Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua katika hii dunia kuna mambo mengi,wazungu ambao leo tunawaona wameendelea katika karne ya 15 na kurudi nyuma walikuwa wanapenda sana uchawi lakini as time went na hasa baada ya industrial revolution katika nchi zao wakaona uchawi hauna ishu tena katika maendeleo ya nchi ama ya mtu binafsi, so huyo sheikh Yaya kwa ufahamu wangu mdogo kuhusu yeye najua ni mtabiri wa nyota sasa hizo kazi za ulinzi wa kishirikina kwa Rais ameanza lini,ama ndio mbwembwe z kutafuta umaarufu mjini
   
 6. E

  ELLET Senior Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi sio mshabiki wa uchawi. Ila swala la mtu na mungu wake ni binafsi. Mimi namwamini Mungu wa mbinguni, na siwezi kumlaumu mtu anaye amini wachawi, majini (yani mashetani). Kazi yangu (na yako) ni kumpa ushaidi kwamba Mungu wangu ndo Mungu wa ukweli. Ila kwasababu na sisi tunaojifanya kwamba tuna Mungu wa ukweli lakini matendo yetu na tabia zetu ni kama wao, wenzetu wanashindwa kuelewa Mungu wetu na miungu yao ina tofauti gani. kazi yangu na kazi yako ni kuwathibitishia wanaoamini uchawi kwamba Mungu wa Mbinguni ndo Mungu peke wa kuabudu, au sivyo lets not make noise at them when we havent settled our relationship with our God. Na kibaya zaidi, wote mbele za Mungu sote ni wadhambi hakuna aliye na upper hand.
   
Loading...