Ni dalili gani zinazoonesha unatumika?

Ni dalili gani zinazoonesha unatumika?

Naona watu hawajaelewa mada sjui,
Hii mimi pia imenishangaza

swali ni dalili zipi zinazoashiria mtu anatumika anyway twende tu
anyway dalili mojawapo mtu kukupa treatment nzuri za ghafla hii wengi huwa traped.
Mtu kua mwema kupitiliza
Ila sasa kuna ubaya gani mtu kua mwema ?
utajuaje huu wema ni chambo?
Nyingine mtu anakutengenezea msala alafu baadae anajifanya kukusaidia ili akutumie kirahisi hata hata serikalini huu mfumo unatumika sana,cheki series ya ozark utaona huu mfano.
Noma sana
 
Everyone has a price, and you have to know what it is,

Everyone has a breaking point or a price tag, whether that price is paid in cash, power, loyalty, or time.
 
Hivi hii issue ya Limbwata ni kweli au 🤣🤣 naomba maelekezo
Kama wewe ni 'KE' nitumie Majina yako matatu,la Mama yako na la Baba yake na Mama yako.Tuanzie hapo...Utakuwa unaniona kwenye Maji ya kuoga,ya kunawa usoni,ya kupigia maswali na kwenye chai na mkojo wako.Na utanitafuta nikutumie kwa faida...
 
Mara nyingi utasikia watu wakisema, Huyu anatumika na watu fulani, au Huyu anatumiwa tu.

Lakini swali linakuja, kutumika ni nini hasa?

Kipengele A:

Kutumika kwenye mahusiano

Kwenye mahusiano mtu anaweza kutumika kama chombo cha starehe

Yaani hakuna future yoyote, hakuna upendo wa kweli, ila upande mmoja anajua kabisa anachofanya Anaweza kuwa mwanaume au mwanamke

Ugumu unakuja kwa yule anayetumika

Mara nyingi si rahisi kugundua kwa sababu anakuwa amelewa mapenzi
Hisia zinakuwa zimemtawala kiasi kwamba haoni wala hasikii

Hata akionyeshwa na watu wa karibu kuwa anatumika, mara nyingi haamini

Anaona anaonewa wivu, wanamchonganisha au hawataki kuona akifurahia mahusiano yake

Lakini siku akigundua ukweli, mara nyingi anakuwa tayari kapotezewa muda, kaumizwa na kuchezewa hisia

Ndipo huanza kurudisha kumbukumbu nyuma na kukumbuka vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kama red flags, lakini kipindi kile hakuweza kuviona kwa sababu hisia zilikuwa zimemtawala

Kipengele B:

Kutumika kufanya uhalifu au kutimiza ajenda za wengine

Mtu anaweza pia kutumika kufanya uhalifu au kutimiza malengo ya watu wengine

Anaweza akawa anajua anachokifanya,
lakini pia anaweza akawa hatambui kabisa kuwa anatumika

Mimi naongelea zaidi yule anayetumika bila kujua

Mara nyingi watu wanaowatumia wenzao huwa smart sana

Wanajua namna ya kukufanya uwaamini

Wanaweza kukuonyesha upendo, kukujali, kukusaidia au kukupa nafasi mpaka uanze kuona hawawezi kuwa na nia mbaya(Fake treatment)

Watu wa pembeni wanaweza kuona mapema kwamba unatumika na wakajaribu kukuambia, lakini mara nyingi ni vigumu kuamini

Unaona kama wanakuhukumu vibaya au wanataka kukuchonganisha

Mpaka siku wale waliokuwa wanakutumia wanapomaliza kile walichokuwa wanakitaka, ndipo wanakuacha ukatupwa kama toilet paper hapo akili inarudi

Sasa hapo ndipo unaanza kukumbuka maneno ya watu waliokuwa wanakuonya, lakini yanakuwa hayana msaada tena()

Unaanza kuunganisha matukio na kukumbuka zile ishara ndogo ndogo ulizopuuzia, ukitambua kwamba zilikuwa ni red flags lakini lahaulaaa umechelewa tayari

Swali la mjadala

Kwa maoni yako, mtu anawezaje kugundua kuwa anatumika?

Ni dalili zipi ukiziona unaweza kusema

Hapa kuna kitu si sawa, nahisi natumika

Iwe kwenye:

1 Mahusiano
2 Kazi.
3 Siasa
4 Urafiki
5 Au maisha kwa ujumla

Karibuni tushirikishane mawazo na uzoefu
Huenda majibu yako yakamsaidia mtu kugundua mapema kuwa anatumika kabla hajachelewa

Midnight:02
ShesRise_1 🤚
Misukule ya misikitini na makanisani bila kusahau misukule ya CCM.
 
Kujua kama unatumika ni kujiuliza je ikiwa leo nitaacha kutoa kile kinachowafanya watu waendelee kunipenda iwe ni pesa, muda, ushawishi, ngono, maarifa au msaada, bado wataendelea kuonyesha upendo na thamani ile ile?

Kama jibu ni hapana, kuna uwezekano mkubwa unatumika.

Mfano kwenye mahusiano, mtu anakutafuta tu akiwa na shida ya fedha, anahitaji sex, au emotional support, ukipata matatizo yako mwenyewe, ghafla anakuwa busy, anakupotezea au anakukasirikia, hapo bila kupepesa macho unatumika.

Kazini mwajiri wako anakupa majukumu ya watu watatu, lakini mshahara, nafasi na appreciation haviongezeki, kila ukidai haki yako unaambiwa, "kuwa mvumilivu." Hapo unatumika.

Kwenye siasa Unahamasishwa kupigana, kutukana au kujitolea kwa nguvu zote kwa ajili ya viongozi ,hili nadhani tuna ushuhuda nalo hata humu ndani namna baadhi ya members wanavyo pigania maslahi ya viongozi wao hata sehemu wanazo paswa kupinga wao wana support tu , hawa wanatumika tena vibaya sana.

Kwenye urafiki ni wewe ndiye unakuwa unajitoa zaidi kwenye matatizo yao, siku wewe ukiwa na shida hakuna anayepatikana wala kujitoa kwa ajili yako, hapo unatumika.

Kwa kifupi, ukitoa muda, pesa, nguvu na uaminifu kuliko unavyopokea heshima, ukweli na support, stop and re evaluate, mahusiano yoyote yenye afya yanapaswa kuwa na mutual benefit.
 
Mara nyingi utasikia watu wakisema, Huyu anatumika na watu fulani, au Huyu anatumiwa tu.

Lakini swali linakuja, kutumika ni nini hasa?

Kipengele A:

Kutumika kwenye mahusiano

Kwenye mahusiano mtu anaweza kutumika kama chombo cha starehe

Yaani hakuna future yoyote, hakuna upendo wa kweli, ila upande mmoja anajua kabisa anachofanya Anaweza kuwa mwanaume au mwanamke

Ugumu unakuja kwa yule anayetumika

Mara nyingi si rahisi kugundua kwa sababu anakuwa amelewa mapenzi
Hisia zinakuwa zimemtawala kiasi kwamba haoni wala hasikii

Hata akionyeshwa na watu wa karibu kuwa anatumika, mara nyingi haamini

Anaona anaonewa wivu, wanamchonganisha au hawataki kuona akifurahia mahusiano yake

Lakini siku akigundua ukweli, mara nyingi anakuwa tayari kapotezewa muda, kaumizwa na kuchezewa hisia

Ndipo huanza kurudisha kumbukumbu nyuma na kukumbuka vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kama red flags, lakini kipindi kile hakuweza kuviona kwa sababu hisia zilikuwa zimemtawala

Kipengele B:

Kutumika kufanya uhalifu au kutimiza ajenda za wengine

Mtu anaweza pia kutumika kufanya uhalifu au kutimiza malengo ya watu wengine

Anaweza akawa anajua anachokifanya,
lakini pia anaweza akawa hatambui kabisa kuwa anatumika

Mimi naongelea zaidi yule anayetumika bila kujua

Mara nyingi watu wanaowatumia wenzao huwa smart sana

Wanajua namna ya kukufanya uwaamini

Wanaweza kukuonyesha upendo, kukujali, kukusaidia au kukupa nafasi mpaka uanze kuona hawawezi kuwa na nia mbaya(Fake treatment)

Watu wa pembeni wanaweza kuona mapema kwamba unatumika na wakajaribu kukuambia, lakini mara nyingi ni vigumu kuamini

Unaona kama wanakuhukumu vibaya au wanataka kukuchonganisha

Mpaka siku wale waliokuwa wanakutumia wanapomaliza kile walichokuwa wanakitaka, ndipo wanakuacha ukatupwa kama toilet paper hapo akili inarudi

Sasa hapo ndipo unaanza kukumbuka maneno ya watu waliokuwa wanakuonya, lakini yanakuwa hayana msaada tena()

Unaanza kuunganisha matukio na kukumbuka zile ishara ndogo ndogo ulizopuuzia, ukitambua kwamba zilikuwa ni red flags lakini lahaulaaa umechelewa tayari

Swali la mjadala

Kwa maoni yako, mtu anawezaje kugundua kuwa anatumika?

Ni dalili zipi ukiziona unaweza kusema

Hapa kuna kitu si sawa, nahisi natumika

Iwe kwenye:

1 Mahusiano
2 Kazi.
3 Siasa
4 Urafiki
5 Au maisha kwa ujumla

Karibuni tushirikishane mawazo na uzoefu
Huenda majibu yako yakamsaidia mtu kugundua mapema kuwa anatumika kabla hajachelewa

Midnight:02
ShesRise_1 🤚
Maisha ni either ule au uliwe
 
Kujua kama unatumika ni kujiuliza je ikiwa leo nitaacha kutoa kile kinachowafanya waendelee kunipenda iwe ni pesa, muda, ushawishi, ngono, maarifa au msaada, bado wataendelea kuonyesha upendo na thamani ile ile?
🥰🥰 siongezi chochote
Kama jibu ni hapana, kuna uwezekano mkubwa unatumika.
💯
Mfano kwenye mahusiano, mtu anakutafuta tu akiwa na shida ya fedha, anahitaji sex, au emotional support, ukipata matatizo yako mwenyewe, ghafla anakuwa busy, anakupotezea au anakukasirikia, hapo bila kupepesa macho unatumika.
Brother 😍😍
Kazini mwajiri wako anakupa majukumu ya watu watatu, lakini mshahara, nafasi na appreciation haviongezeki, kila ukidai haki yako unaambiwa, "kuwa mvumilivu." Hapo unatumika.
Siongeziii neno👏👏
Kwenye siasa Unahamasishwa kupigana, kutukana au kujitolea kwa nguvu zote kwa ajili ya viongozi ,hili nadhani tuna ushuhuda nalo hata humu ndani namna baadhi ya members wanavyo pigania maslahi ya viongozi wao hata sehemu wanazo paswa kupinga wao wana support tu , hawa wanatumika tena vibaya sana.
I wish wasome hapa
Kwenye urafiki ni wewe ndiye unakuwa unajitoa zaidi kwenye matatizo yao, siku wewe ukiwa na shida hakuna anayepatikana wala kujitoa kwa ajili yako, hapo unatumika.
Siongezii🙌🙌
Kwa kifupi, ukitoa muda, pesa, nguvu na uaminifu kuliko unavyopokea heshima, ukweli na support, stop and re evaluate, mahusiano yoyote yenye afya yanapaswa kuwa na mutual benefit.
♥️♥️♥️🙏🙏👏👏🫡🫡🫡🫡
Shukran sana ☺️
 
In short according to psychology

We like in others what's missing in us, so they end up making us stay...

We hate in others what we hate in our selves, so people piss us off because they make our shadows visible

Kwenye haya maisha hakuna kutumika, tunafanya na kukubali kila kitu kibaya kinacho tutokea. Hata kama sisi wenyewe hatujui
Mkuu kwanini kuna dhana kama emotional manipulation, coercive control na undue influence?
 
Back
Top Bottom