Ni dalili gani zinazoonesha unatumika?

Ni dalili gani zinazoonesha unatumika?

Ukijihisi una mimba, hiyo ndio dalili ya kwanza ya mimba.

Nadhani nimeeleweka 😎
 
Inabid uangalie red flag mapema ujue kama unatumika. Muhimu ni kutunza energy yako usipende kujirahisisha ili hata kama utatumika utumike kwa ghrama kubwa.

Usikubali kutumika kwa bei chee kama pipi mtu akutumie kwa gharama japo haitalingana na thaman yako. Mm hapa napita tu maana natumika kwenye kampuni moja
 
Inabid uangalie red flag mapema ujue kama unatumika. Muhimu ni kutunza energy yako usipende kujirahisisha ili hata kama utatumika utumike kwa ghrama kubwa.

Usikubali kutumika kwa bei chee kama pipi mtu akutumie kwa gharama japo haitalingana na thaman yako. Mm hapa napita tu maana natumika kwenye kampuni moja
Asantee Mkuu
 
Mara nyingi utasikia watu wakisema, Huyu anatumika na watu fulani, au Huyu anatumiwa tu.

Lakini swali linakuja, kutumika ni nini hasa?

Kipengele A:

Kutumika kwenye mahusiano

Kwenye mahusiano mtu anaweza kutumika kama chombo cha starehe

Yaani hakuna future yoyote, hakuna upendo wa kweli, ila upande mmoja anajua kabisa anachofanya Anaweza kuwa mwanaume au mwanamke

Ugumu unakuja kwa yule anayetumika

Mara nyingi si rahisi kugundua kwa sababu anakuwa amelewa mapenzi
Hisia zinakuwa zimemtawala kiasi kwamba haoni wala hasikii

Hata akionyeshwa na watu wa karibu kuwa anatumika, mara nyingi haamini

Anaona anaonewa wivu, wanamchonganisha au hawataki kuona akifurahia mahusiano yake

Lakini siku akigundua ukweli, mara nyingi anakuwa tayari kapotezewa muda, kaumizwa na kuchezewa hisia

Ndipo huanza kurudisha kumbukumbu nyuma na kukumbuka vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kama red flags, lakini kipindi kile hakuweza kuviona kwa sababu hisia zilikuwa zimemtawala


Kipengele B:

Kutumika kufanya uhalifu au kutimiza ajenda za wengine

Mtu anaweza pia kutumika kufanya uhalifu au kutimiza malengo ya watu wengine

Anaweza akawa anajua anachokifanya,
lakini pia anaweza akawa hatambui kabisa kuwa anatumika

Mimi naongelea zaidi yule anayetumika bila kujua

Mara nyingi watu wanaowatumia wenzao huwa smart sana

Wanajua namna ya kukufanya uwaamini

Wanaweza kukuonyesha upendo, kukujali, kukusaidia au kukupa nafasi mpaka uanze kuona hawawezi kuwa na nia mbaya(Fake treatment)

Watu wa pembeni wanaweza kuona mapema kwamba unatumika na wakajaribu kukuambia, lakini mara nyingi ni vigumu kuamini

Unaona kama wanakuhukumu vibaya au wanataka kukuchonganisha

Mpaka siku wale waliokuwa wanakutumia wanapomaliza kile walichokuwa wanakitaka, ndipo wanakuacha ukatupwa kama toilet paper hapo akili inarudi

Sasa hapo ndipo unaanza kukumbuka maneno ya watu waliokuwa wanakuonya, lakini yanakuwa hayana msaada tena()

Unaanza kuunganisha matukio na kukumbuka zile ishara ndogo ndogo ulizopuuzia, ukitambua kwamba zilikuwa ni red flags lakini lahaulaaa umechelewa tayari


Swali la mjadala

Kwa maoni yako, mtu anawezaje kugundua kuwa anatumika?

Ni dalili zipi ukiziona unaweza kusema

Hapa kuna kitu si sawa, nahisi natumika

Iwe kwenye:

1 Mahusiano
2 Kazi.
3 Siasa
4 Urafiki
5 Au maisha kwa ujumla

Karibuni tushirikishane mawazo na uzoefu
Huenda majibu yako yakamsaidia mtu kugundua mapema kuwa anatumika kabla hajachelewa

Midnight:02
ShesRise_1 🤚
Kujua kuwa unatumika inaweza kuwa tricky kwa sababu anayekutumia anakuwa amekushinda kwa ujanja. Nikupe mfano mmoja. Nlikuwa na demu moja mwenye makebo makubwa. Tatizo ni kuwa alikuwa na akili ndogo sana hivyo anatumika na shoga zake. Walikuwa wanamtumia kwa kumpeleka bar na kwa sababu alikuwa ana-attract attention ya ''wanaume wakware wa Dar'' na wao wanapata soko. Wakati mwingine walikuwa wanamweka ''mtu kati'' na kumpiga mnada wa wanaume. Alichezewa kwa muda mrefu mpaka alipokuwa zilipendwa ndiyo alihangaika kunitafuta... too late.
 
Kujua kuwa unatumika inaweza kuwa tricky kwa sababu anayekutumia anakuwa amekushinda kwa ujanja.
kweli kabisa unakua kama umevalishwa miwani ya mbao
Nikupe mfano mmoja. Nlikuwa na demu moja mwenye makebo makubwa. Tatizo ni kuwa alikuwa na akili ndogo sana hivyo anatumika na shoga zake. Walikuwa wanamtumia kwa kumpeleka bar na kwa sababu alikuwa ana-attract attention ya ''wanaume wakware wa Dar'' na wao wanapata soko. Wakati mwingine walikuwa wanamweka ''mtu kati'' na kumpiga mnada wa wanaume. Alichezewa kwa muda mrefu mpaka alipokuwa zilipendwa ndiyo alihangaika kunitafuta... too late.
Mwanamke unamfanyia mwenzako hivi
Kuna haja ya kua makini na tunaowaita marafiki
 
Back
Top Bottom