Ni Bora Wazungu watutawale tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Bora Wazungu watutawale tena?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Mar 8, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi hali ya nchi kiutawala na kimaendeleo inavyokwenda,nionavyo twendako ni giza tupu ,sasa nikifikiria ile hali ya wazee wetu wa zamani ,tuseme baada ya kipindi cha utumwa ambapo bado wazungu waliendelea kutawala na nisikiavyo nchi ilikuwa nzuri na sheria na hali ya amani kwa wananchi na mali zao ilikuwa ni ya kuridhisha sana ,watu wakilala milango wazi ikafikia milango hufungwa madirisha wazi.

  Ila baada ya kupata UHURU ikaondoka kulala madirisha wazi na kufikia hatua za madirisha na milango ya raia wa kawaida kuwa kama madirisha ya mahakamani au tuseme nyumba za siku hizi hazitafautiani na jela kwa style ya milango na madirisha ,nondo tupu hata umbu inakuwa mtihani kupita. Kumbuka tupo katika kujitawala wenyewe Raisi akiwa Kikwete na wengine waliopita.

  Je ni lipi litakaloweza kukufanya usione bora kurudi mtawala mzungu kwani imeonekana hata kazini ikiwa kiongozi ni mzungu basi mambo na taratibu huwa nzuri na kila mmoja anazifuata bila ya manung'uniko.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acha UBAGUZI wewe Mwiba.

  Utamwitaje binadamu mwenzio Mzungu? Wee ukienda Marekani wakuite NIGGA utafurahi?

  "Hallow, what's up my Nigga boy......." Hahahaaaa...... Mkuki kwa binadamu unauma siyo?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mweupe atabaki kuwa mweupe na mweusi atabakia hivyo hivyo, sasa mweupe akikwita mweusi na ukakasirika inaonyesha utakuwa hujielewi au wewe mwenyewe kama mwenyewe utakuwa unajichukia kwa vile ulivyokuwa mweusi.

  Mimi sioni hilo katika mada niliyoigusia ,kimuelekeo wakati wa utawala wa kizungu maisha inasemwa yalikuwa mazuri sana sana na hata ukiangalia zile nchi ambazo mzungu alichelewa kuondolewa kiutawala zilipiga hatua kubwa mno ,lakini baada ya hao wazungu kuondoka leo imebaki majuto matupu kiasi cha wengine kufikia kusema bora mkoloni mweupe au hujawahi kusikia watu wakisema hayo kwa hasira ? Inakuwaje hapo ?
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Watu weusi tuna laana ya kuzaliwa!
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  kweli kabisaa ndugu yangu. kudai uhuru sio big deal sana ila kutumia elimu yako kwa faida ya wote ndio big deal. wewe unategemea nini kutawaliwa mtu mwenye kuweka sifa zake binafsi mbele kuliko sifa za umma? sifa za umma ni kujenga uchumi imara na siyo kutawaliwa na siasa safi. Nchi duniani husifiwa kwa kuwa na mafanikio mazuri ya kujenga uchumi tuu na sio kingine. ndio maana marekani ina jina kubwa kuliko Urusi.Kenya sasa inaitwa economic giant of east africa! inaviwanda vya kimbo karibia katika nchi saba africa mash na kati! sisi tuna makada karibia nchi nne za kusini mwa africa. Msumbiji, angola, namibia na ......!

  Mkazo tuliouweka baada ya kupata uhuru ni huu:
  Kusaidia wakimbizi na kuikomboa africa wakati 99% ya watanzania hawajakombolewa kielimu wala kupata kazi!

  Kufukuza mabepari nchini na kunyang'anya mali zao, wakati huwezi kumkomboa mtu asiye na ajira bira kuwa na mabepari!

  Kufundisha mgambo!

  kuwapeleka watu wasio na kazi vijijini na kuwaita wakulima ingawa hawana mashamba makubwa ya kuima kibiashara!

  kwa mtaji huu tumejikuta tunaitwa one of the most poorest country in the world.

  tukiendelea na watu kama kikwete na mkapa , lazima tutafika mbali. maana maraisi hawa wamefanyi akzi pale alipoacha mkoloni.
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mwiba una tatizo la kijinsia.
  Usiombe kumilikiwa Kama the fair gender.
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Dawa sio kuleta wazungu, dawa ni kuwaondoa CCM na kuweka Chadema. Na wenyewe wakiharibu tunatoa tunaweka wengine, hatimae iko siku tutapata wazalendo wa kweli, lakini Wazungu hawafai. Achaneni na fikra za kitumwa.
   
 8. I

  IFRS 9 Senior Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda wakutawale wewe na mjomba wako.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,983
  Trophy Points: 280
  Nani amesema tulishawahi kupata uhuru?Nakubaliana na mleta mada, maybe tuwaachie wakoloni usukani, tupiganie tu haki za kibinadamu, yani tusiwe second class citizens na kusiwe na ubaguzi, tuwakabidhi utawala, hawa manyapara wanachosha.
   
 10. W

  We know next JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umenena Mkuu
   
 11. jponcian

  jponcian Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Mkuu nadhani urudi na kutafakari upya kuhusu mada yako...Ni nini kinakufanya uhusianishe ukoloni na amani? Huoni kama inawezekana huo ulikuwa mfumo wa uaminifu ambao jamii zetu zilikuwa zimejiwekea? Kama unadhani wazo lako lina mashiko anza wewe kubinafsisha utawala wa familia yako kwa mzungu halafu tujifunze kutokana na hilo ndo tuweze kuamua kuwaleta tena au la!
   
Loading...