Ni binamu yangu lakini nashindwa kumwelewa

Ni binamu yangu lakini nashindwa kumwelewa

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Ni mtoto wa shangazi yangu, ni mzuri kweli kweli, nikisema mzuri naomba muelewe hivyo sintoweza kuanza kutoa sifa hapa mara ana shingo ya nini sijui macho yamekaaje mara hivi mara vile, eleweni tu kwamba ni mzuri sana.

Tatizo nilianza kuliona miaka miaka mitatu iliyopita wakati wote tunaishi nyumbani Ilikuwa tukikaa sebuleni labda kuangalia TV, japo makochi ni mengi yeye anakuja kunikalia mapajani, nikiwa nipo nje ya nyumbani kwa muda mrefu, ninaporudi anakuja kunipokea tena ananikumbatia na busu juu la mdomoni.

Wakati mwingine nikawa nahisi kuwa labda kanimaindi lakini anashindwa kufunguka au ni vp labda, nilikuwa huru kumshikashika maeneo mbalimbali ya mwili wake na akiona naelekea mahali sio penyewe hagombi wala nini ananiondoa mkono taratibu tu.

Nikabaki njia panda kwamba nimwambie au, na nikimwambia je kama hakuwa na nia mbaya atanionaje, nikawa sina la kufanya hapa juzi kati akapata mchumba na process zote zikaenda vizuri hatimae wakafunga ndoa na sherehe kubwa tu.

Sasa hiyo siku ya ndoa ilipofika wakati wa zawadi tukaanza kutoa, nilipofika kwa bi haruc nikampa mkono nikashangaa ananivutia kwake akanikumbatia halafu akanong'ona sikioni mwangu ni kwanini siku zote hizo ulishindwa kunielewa?

Sasa ndo najiuliza kwamba nilishindwa kumuelewa kwa lipi? au alitaka ni mnanihii? Na ndoa yenyewe ilikuwa ni juzi tu hapa nisaidieni mawazo kwa hilo wadau.
 
Tukusaidie mawazo umuelewe au?

Inawezekana kusoma ni taabu mkuu, hata picha hukuona!!
 
Its too late now... You are a good president she never had, Just like Odinga! Just accept that...
 
Tatizo lipo wapi hapa ili tukusaidie? Ni binam huyooo sa ulitaka nini? Hakujua kuwa weye ungemheshimu hivyo, hakujua kuwa ungemlinda hivyo, sasa nini tena?
Ngoja akijifungua mtoto wake nenda na kibuyu cha maziwa umwambie anywe uji ka kule home zamani. Baasi, utamwelewa na yeye atakuelewa kuwa uzinzi ni dhambiiiii. Acha kuwaza uovu juu ya mke wa mtu weye
 
Back
Top Bottom