Ni asilimia 21 tu zitaenda kwa Wazanzibari katika Nafasi 1,097 za kazi kutoka TRA, marekebisho yanahitajika

Ukweli huu muungano wa Zanzibar hawautaki kabisa. Ila wa bara ndio tunautaka.

Halafu humu vilaza wengi hawajui Zanzibar = Zanzibar only. Huku Tanzania = Tanganyika + Zanzibar.

Yaani bila Zanzibar hakuna Tanzania. Na hapo TRA ni Tanzania revenue authority .kila taasisi yenye neno Tanzania m Zanzibar ana haki ya kuajiriwa napo maana yeye ni m Tanzania
cariha pitia point muhimu hii, itajibu maswali yako mengi
 
Mkuu unapoona shirika au Taasisi ina neno la Tanganyika, hapo ni watanganyika tu wanahusika, mfano Tanganyika law society chama cha wanasheria wa Tanganyika

unapoona shirika au Taasisi ina neno la Zanzibar, hapo ni Wazanzibar tu wanahusika, ZRB shirika na kukusanya mapato Zanzibar, ZFF shirika la mpira Zanzibar


unapoona shirika au Taasisi ina neno la Tanzanja, hapo wote watanganyika na wazanzibar wana haki ya kushiriki, mfano TRA, ATCL, JWTZ, n.k
Yule shangazi yenu alivyokuwa TLC ni mtanganyika?
 
View attachment 1986349

Kwanza nitoe pongezi kwa serikali iliyosikia kilio cha vijana kwa kutoa ajira zaidi ya elf 1 TRA.

Kama mnavyojua, Kwenye ajira wazanzibar hupewa asilimia 21, kwa hio katika hizi nafasi 1,097 ni sawa na wazanzibari 230 tu,

230 hao bado ni wachache kulingana na idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo

Naona ingependeza walau kuwe na wazanzibar 300 ili kufidia fidia vijana wengi ambao bado wapo mitaani na degree zao.
Acha ujinga si mna mamlaka yenu huko je ni wangapi wabara wanapata huko kwenye hiyo mamlaka yenu,pia inaonekana hesabu zimekupiga chenga, fanya uwiano wa idadi (population) ya wabara na wazanzibar je unataka ajira ziwe sawa kwa kulinganisha kijiji na wilaya, wakati kijiji kina watu 50 na wilaya ina watu zaidi ya laki tano halafu unataka ajia zifanane, mnabahati sana na utawala huu. Nyie si ndio hamtaki muungano lakini ajira mnazitaka halafu ni wavivu kazi kuamuka saa tano asubuhi
 
Acha ujinga si mna mamlaka yenu huko je ni wangapi wabara wanapata huko kwenye hiyo mamlaka yenu,pia inaonekana hesabu zimekupiga chenga,fanya uwiano wa idadi (population) ya wabara na wazanzibar je unataka ajira ziwe sawa kwa kulinganisha kijiji na wilaya, wakati kijiji kina watu 50 na wilaya ina watu zaidi ya laki tano halafu unataka ajia zifanane, mnabahati sana na utawala huu. Nyie si ndio hamtaki muungano lakini ajira mnazitaka halafu ni wavivu kazi kuamuka saa tano asubuhi
Muungano si mnaupenda ehh? Kwanini mnachukia sasa 😂😂😂.
 
Zanzibar ni nchi kamili. Sio sawa na mwanza ama mbeya huko wanakoangalia usawa wa idadi wanapogawa pembejeo.

Jiulize kwanini Zanzibar lazima iwe na raia wake katika vyeo viwili vya juu kila awamu yaani mgombea urais na mgombea mwenza wa Tanzania ni lazima mmojawapo atoke zanzibar kila awamu.

Maswala ya idadi ni kwenye mikoa sio nchi
ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa MBONA HAINA KITI UN ASSEMBLY??? "MNAJIJAMBISHA NA KUSHTUKA WENYEWE" "ZANZIBAR NI SISIMIZI anayetamati kupiga hatua ya TEMBO" , Kamwe hawezi labda aamue kuruka kama anao ubavu.....ahaaaaa, ahaaaaaa
 
Nyerere alikuwa na akili sana kumeza Zanzibar alitumia vigezo vifuatavyo kwanza biashara huru kwa wanzanzibar bara ona walivyojazana bara Mila za kinzanzibari wametupilia mbali wanakula Hadi kitimoto na pombe

Cha pili akatumia Elimu ya juu kuwa jambo la muungano wanejazana vyuo vya bara Hadi hijabu hawavai Tena baada ya kuchanganyika wanavaa vikaptula watoto wa kike Mila za kinzanzibari Kwisha

Cha tatu ajira wanabebwa vijana wa kinzanzibari wanaajiriwa bara wanaharibikia huku kutokana na mchanganyiko na msikitini hawakanyagi Tena baada ya kushika ajira bara na ramadhani hawafungi wanaoa na kuolewa na Wala nguruwe wa bara mengine ongezeeni!!!

Hii inaitwa kumeza nchi ya mtu mwingine technically
Naunga mkono hoja wazanzibari wengi waajiriwe bara
 
ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa MBONA HAINA KITI UN ASSEMBLY??? "MNAJIJAMBISHA NA KUSHTUKA WENYEWE" "ZANZIBAR NI SISIMIZI anayetamati kupiga hatua ya TEMBO" , Kamwe hawezi labda aamue kuruka kama anao ubavu.....ahaaaaa, ahaaaaaa
Kukweli ni muungano wa kinyonyaji, hizi ajira 21% nmeona wengi wakilalamika kuna upendeleo kumbe ni upendeleo uliokaa kimpango zaidi, Yote kwa yote wacha vijana wajaze hizo ajira wapooze machungu kwa mishahara,
 
Kwani si TRA wana kusanya Hadi Zanzibar?
Wavunje TRA isiwe ya Muungano
Wa Zanzibar wawe na TRA Yao..

Hapo ndo tuhoji why iajiri Wazanzibar?

Binafsi siku zote natamani Muungano ufe...
Wewe unahisi Zanzibar ndo inafaidika..
Wengine tunaamini Zanzibar ndo inafanywa masikini na huu Muungano
Mkuu ukinunua kitu Zanzibar ukija huku unatozwa upya Kodi so I don't see any logic behind, ka TRA ni moja why watenge nafasi flani ni watu flani wakati tunasema nchi ni moja hyo hyo.
 
Ukweli huu muungano wa Zanzibar hawautaki kabisa. Ila wa bara ndio tunautaka.

Halafu humu vilaza wengi hawajui Zanzibar = Zanzibar only. Huku Tanzania = Tanganyika + Zanzibar.

Yaani bila Zanzibar hakuna Tanzania. Na hapo TRA ni Tanzania revenue authority .kila taasisi yenye neno Tanzania m Zanzibar ana haki ya kuajiriwa napo maana yeye ni m Tanzania

Lakini m Tanganyika ama mbara hana haki ya kuajiriwa Zanzibar revenue authority sababu neno Zanzibar halimuhusu yeye mbara
Umedadavua vizuri kwelikweli
 
Mbona amepita mulemule ndio maana nasema huu muungano una favor one side zaidi
Zanzibar haina kiti UN, haina timu ya taifa kicheza makbe ya fifa, mikopo ya kimataifa haipati, n.k hizi ajira ni changa la macho tu kuwapooza watu wasahau ila bado zanzibar inaminywa
 
ka TRA ni moja why watenge nafasi flani ni watu flani wakati tunasema nchi ni moja hyo hyo.
Sio nchi moja, Ni muungano kwa hio Taasisi zote za Tanzania pande zote mbili zinahusika.

Jwtz, polisi, Usalama wa taifa, Tra, Bot, Bandarini, Nssf, Mahakama, airport, karibu taasisi zote tu Mzanzibari ana haki kupewa ajira tena kwa hizo asilimia 21.

Njoo urushiwe mbegu kama unaona tunafaidi na mwanao nae awe kwenye hizo 21% 😂😂
 
Kirefu cha ZRB ni nini ? Je m Tanganyika anawezaje kuajiriwa ZRB wakati sio M Zanzibar?

Na kirefu cha TRA ni nini? Je Mzanzibar sio m Tanzania?
Kirefu cha TLC ni nini na mbona fatima karume alikuwa TLC.

Hivi hujui kuwa ukikaa Zanzibar zaidi ya miaka 5 unatakiwa kupewa kitambulisho cha mkaazi; unajua maana yake ni nini?
 
Hivi ni watu wangapi wa bara wanautaka muungano?
Nadhani wanotaka muungano ni viongozi tu ila sisi raia kwa asilimia kubwa hata hatujali.
 
Kirefu cha TLC ni nini na mbona fatima karume alikuwa TLC.

Hivi hujui kuwa ukikaa Zanzibar zaidi ya miaka 5 unatakiwa kupewa kitambulisho cha mkaazi; unajua maana yake ni nini?
TLC sio ajira ya uma wala sio ajira ya kudumu. Ni kama chama cha wanataaluma fulani. Ndio maana nafasi aliyoipata bint karume ni ya kugombea. Sio ya kuomba kazi ama kuteuliwa na rais.

Kumbuka TLC sio shirika la uma

Ila ZRB sio chama bali ni taasisi inayomilikiwa na serikali ya Zanzibar. ZRB ni ajira ya uma. Lazima ilindwe kama taasisi za uma zingine.
 
Mama yetu kitu kikubwa alichofanya ni kuondoa neno la Wanyonge baaasii😂
 
Back
Top Bottom