Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

1. Waziri aliyedumu muda mrefu ni Ameir Jamal.
2. Ndiyo najua kuhusu Ameir Jamal. Aliyewahi kuwa waziri wa fedha kwa vipindi vitatu tofauti ambavyo ni 1965-1972, 1975-1977 na 1979-1983 alipoingia Kighoma Malima na kuhudumu hadi 1985 kabla ya kurudi tena 1994.
3. Kighoma Malima alianza uwaziri wa fedha mwaka 1983. Mkuu nimejibu maswali yako yote uliyouliza. Sioni sababu ya kuendelea kubishana juu ya hili. Mdau Mkupuo hapo juu katoa ushauri mzuri wa kujibu swali lililoulizwa "Ni Akina Nani Walichoma BOT" basi tujikite huko.
Sita umchafue Malima kwa manufaa yako. Hebu soma hapa:
Mawaziri 16 wa fedha walioifikisha Tanzania ilipo sasa tangu
 
Kuna watuhumiwa kadhaa ambao waliachiwa huru baada ya kesi kwenda miaka kadhaa lakini mpaka leo haijajulikana ni nani alianzisha moto ule na ulianzia wapi.
 
Habari wakuu wa jamvi

Mliokuwepo miaka hiyo ya zamani tujuzeni ni akina nani waliosuka mpango wa kuunguza benki kuu ya Tanzania ( BoT ) na walikuwa na dhumuni gani hasa? Je walikamatwa? Na kama walikamatwa hukumu zao zilikuaje?

Tujuzeni ili tuweze kujua kwa faida ya kizazi hiki na kijacho hasa ukizingatia historia na mambo mbalimbali yaliyowahi kutokea huko nyuma kuhusu Taifa letu yanafichwa na kufanywa siri kubwa sana!!

Karibuni wakuu...

Ilikuwa ni tarehe 17 May 1984 alfajiri ya saa 12 asubuhi moshi ulipoonekana unafuka kutoka katika jengo la BOT makao makuu na baadae kuonekana dhahiri kwamba kuna moto unaunguza jengo hilo.

Jengo liliungua sana na makabrasha na taarifa muhimu na fedha zote zilipona kwa kuwa zilikuwa zimehifadhiwa Chumba cha Chuma au strong room.

Baadhi pia ya makaratasi muhimu na rekodi kadhaa ziliteketezwa na moto huo ila sehemu kubwa ya documents zote za maana zilikuwa zimepona kwa kuwa zilikuwa zimehifadhiwa NBC- National Bank of Commerce
 
Ilikuwa ni tarehe 17 May 1984 alfajiri ya saa 12 asubuhi moshi ulipoonekana unafuka kutoka katika jengo la BOT makao makuu na baadae kuonekana dhahiri kwamba kuna moto unaunguza jengo hilo.

jengo liliungua sana na makabrasha na taarifa muhimu na fedha zote zilipona kwa kuwa zilikuwa zimehifadhiwa Chumba cha Chuma au strong room.

Baadhi pia ya makaratasi muhimu na rekodi kadhaa ziliteketezwa na moto huo ila sehemu kubwa ya documents zote za maana zilikuwa kuwa zimehifadhiwa NBC.
BoT ya hapa Dar au mkoani mkuu?
 
Sita umchafue Malima kwa manufaa yako. Hebu soma hapa:
Mawaziri 16 wa fedha walioifikisha Tanzania ilipo sasa tangu
Ilipobaki miaka miwili kabla ya Mwalimu Nyerere kung'atuka katika urais mwaka 1985, alimteua Profesa Kighoma Malima kuwa Waziri wa Fedha naye alitumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili.

Kweli kuna watu wabishi. Kwa hiyo hiyo aya hapo juu iliyo katika hiyo link yako uliyotegemea ikulinde kwenye ubishi wako inamaanisha Kighoma Malima aliteuliwa na Nyerere kuwa waziri wa fedha mwaka 1985?! Mwalimu Nyerere aling'atuka mwaka gani? Siyo 1985? Na miaka miwili kabla ya 1985 Nyerere alipong'atuka ni lini? Siyo 1983? Kwa heri mkuu.
 
Nyerere aliikalia ripoti ya Scotland Yard....
walimwambia ukiripoti vinginevyo tutakukanusha.....tetesi zilisema
haikuwahi kutangazwa hiyi ripoti

Hizo ni classified materials.

Halafu kama unaunganisha dots vizuri pia Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki tarehe 12 April mwaka 1984.

Hivyo jengo liliungua mwezi mmoja baada ya kifo chake tarehe 17 May 1984
 
Mbona inaJulikana ni mkono na alikimbilia ulaya mpaka nyerere alipokufa
 
Habari wakuu wa jamvi

Mliokuwepo miaka hiyo ya zamani tujuzeni ni akina nani waliosuka mpango wa kuunguza benki kuu ya Tanzania ( BoT ) na walikuwa na dhumuni gani hasa? Je walikamatwa? Na kama walikamatwa hukumu zao zilikuaje?

Tujuzeni ili tuweze kujua kwa faida ya kizazi hiki na kijacho hasa ukizingatia historia na mambo mbalimbali yaliyowahi kutokea huko nyuma kuhusu Taifa letu yanafichwa na kufanywa siri kubwa sana!!

Karibuni wakuu...
Ukipata jibu usisahau kuuliza aliyechoma Ikulu miaka ya mwanzoni mwa 2000,walisema chanzo chake ni moto wa pasi.
Wale waliokuwa na kili nadhani wanakumbuka tukio hili,si kwamba ikulu iliungua yote ila sehemu fulani iliungua.
 
Hizo ni classified materials.

Halafu kama unaunganisha dots vizuri pia Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki tarehe 12 April mwaka 1984.

Hivyo jengo liliungua mwezi mmoja baada ya kifo chake tarehe 12 May 1984
Ahaa...twende taratibu sasa!! Inaonekana ni kweli kifo cha Sokoine ni faulo ilichezwa. Turudi sasa kwenye mada yetu, Nimrod alikuwa nani kipindi hiko?
 
Ahaa...twende taratibu sasa!! Inaonekana ni kweli kifo cha Sokoine ni faulo ilichezwa. Turudi sasa kwenye mada yetu, Nimrod alikuwa nani kipindi hiko?

Daah! Mkuu mimi naongezea mdalasini kwenye nyama yetu hii ya mbuzi, sasa alieleta kuku mzima ni Baba Yenu hapo juu ungemuuliza yeye hilo suali la Nimrod Mkono.

Maana ametoa hilo dai huku ametulia, sivyo?
 
Hizo ni classified materials.

Halafu kama unaunganisha dots vizuri pia Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki tarehe 12 April mwaka 1984.

Hivyo jengo liliungua mwezi mmoja baada ya kifo chake tarehe 12 May 1984
Kwa mujibu wa archives zilizopo BOT iliungua tarehe 17 May 1984.
 
Back
Top Bottom