Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

hata hii link uloweka mbona bado inaonyesha malima aliingia wizara hiyo mwaka 1983? hapo mwandishi alipoandika ("ilipobakia miaka miwili kabla ya mwalimu kung'atuka katika uraisi 1985 (miaka miwili kabla maana yake si ni 1983) alimteua Profesa Kighoma Malima kuwa waziri wa fedha") au wewe mwenzetu unasoma kinyume?
Achana na hayo mambo, tuambieni waliochoma benki ni akina nani?
 
Nashangaa sana hizi taarifa sijui mnazipata wapi wadau. Hivi kweli akina Memba na jamaa zake wameteka ndege ya ATC na kuipeleka Uingereza mwaka 1984?! Hapana. Hiyo ndege imetekwa mwezi March, 1982. Na unatwambia jumuiya ya EAC ilikuwepo mwaka 1984????? What a joke!

Hayo majibu mengine kuhusu mawaziri waliopita pale wizara ya fedha andika "minister of finance (Tanzania)" kisha u search kupata facts.

Yes, Hayati Mwalimu nakumbuka alihutubia mkutano wa makubaliano ya kuvunja kabisa jumuiya hiyo baada ya miaka 17 tokea 1977 EAC ilipovunjika ilikuwa ni mwezi May 1984 mjini Arusha.

Viongozi wa Uganda, Kenya na Tanzania hawakuwa wamesaini makabrasha ya kukubaliana kuvunja umoja huo na kulifuatia matatizo mengi baada ya hapo likiwemo suala la watumishi wa EAC wengine kuja kuwa wazee huku bado wakiwa wanafuatilia viinua mgongo vyao.

Hilo la kutekwa ndege upo sahihi ni mwaka 1982 kwasababu Mzee Msuya alikuwa waziri mkuu kabla ya hayati Sokoine.

Ahsante kwa kuniweka kumbukumbu zangu sawa.
 
Bob makani alikuwa ni mmoja wa waazilishi wa chadema.
Pia umekosea kidogo tu.
Kigoma Malima aliingia 1985.
Naomba tusiwapotoshe watu. Tuweke siasa pembeni.
Hapana marehemu Kighoma Ali Malima aliingia wakati wa mwalimu Nyerere kuanzia 1983 hadi 1985 kwa mara ya kwanza na baadaye akawepo tena kwenye awamu ya pili
 
Sasa hapo ndio unataka kupotosha jamii kwa makusudi.
Hebu nakuomba uniambie. Ni waziri yupi aliyedumu kwada mrefu? Hivi unajua luhusu Waziri wa fedha Jamal?
Ukishamjua niambia huyo waziri Malima alianza lini uwazir!!!?

Kighoma Malima alianza 1985. Nakumba usiwapotoshe watu kuna watu hawajui hayo.
tcvcl;'.ludfrd
 
BoTi kuchomwa moto ilikua kama movie was planned
Mastermind alikua Mkonoh

Baada ya kuweka mazingira safi na kutawanya pesa kama escrow, wakatia kiberit, ukiwa unalenga documents maarum na zoez lilifanikiwa apo mwalimu hakuwa TZ
Baada ya mission kuisha, mkonoh mwenye akachukua simu na kumvutia simu mwalmu

Mkonoh; mwalimu habar, uku nyumban BoTi imeungua na moto

Kama dakka mbil iv

Mwalmu; Mkonoh nikirud Tz nisikukute nakufunga maanina ww!!! ( mwalmu alijue hii sio kawaida watakua wamefanya yao tu)

Mkono alipotea Tz ad kifo cha mwalmu ndio alirud
 
BoTi kuchomwa moto ilikua kama movie was planned
Mastermind alikua Mkonoh

Baada ya kuweka mazingira safi na kutawanya pesa kama escrow, wakatia kiberit, ukiwa unalenga documents maarum na zoez lilifanikiwa apo mwalimu hakuwa TZ
Baada ya mission kuisha, mkonoh mwenye akachukua simu na kumvutia simu mwalmu

Mkonoh; mwalimu habar, uku nyumban BoTi imeungua na moto

Kama dakka mbil iv

Mwalmu; Mkonoh nikirud Tz nisikukute nakufunga maanina ww!!! ( mwalmu alijue hii sio kawaida watakua wamefanya yao tu)

Mkono alipotea Tz ad kifo cha mwalmu ndio alirud
Kawahadithie wanafesibuku wenzako
 
1. Waziri aliyedumu muda mrefu ni Ameir Jamal.
2. Ndiyo najua kuhusu Ameir Jamal. Aliyewahi kuwa waziri wa fedha kwa vipindi vitatu tofauti ambavyo ni 1965-1972, 1975-1977 na 1979-1983 alipoingia Kighoma Malima na kuhudumu hadi 1985 kabla ya kurudi tena 1994.
3. Kighoma Malima alianza uwaziri wa fedha mwaka 1983. Mkuu nimejibu maswali yako yote uliyouliza. Sioni sababu ya kuendelea kubishana juu ya hili. Mdau Mkupuo hapo juu katoa ushauri mzuri wa kujibu swali lililoulizwa "Ni Akina Nani Walichoma BOT" basi tujikite huko.

Vijana wa dotcom kizazi cha Jakaya hawawezi kukuelewa!

Unajua siku hizi ignorance is a choice. Hivi hizi smart phones watu sijui wanazifanyia kazi gani.

Its a shame kwa kweli...
 
Back
Top Bottom