Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,410
3,548
Habari wakuu wa jamvi

Mliokuwepo miaka hiyo ya zamani tujuzeni ni akina nani waliosuka mpango wa kuunguza benki kuu ya Tanzania ( BoT ) na walikuwa na dhumuni gani hasa? Je walikamatwa? Na kama walikamatwa hukumu zao zilikuaje?

Tujuzeni ili tuweze kujua kwa faida ya kizazi hiki na kijacho hasa ukizingatia historia na mambo mbalimbali yaliyowahi kutokea huko nyuma kuhusu Taifa letu yanafichwa na kufanywa siri kubwa sana!!

Karibuni wakuu...
 
Sio kweli, BOT ilipoungua gavana alikuwa marehemu Charles Nyirabu na waziri wa fedha alikuwa Edwin Mtei!! Boss alikuwepo enzi hizo .
Mkuu umeandika nusu ukweli na nusu siyo kweli. Kumbukumbu sahihi ni kwamba BOT iliungua moto mwaka 1984. Wakati inaungua waziri wa fedha alikuwa ni Kighoma Malima ambaye alikuwa katika nafasi hiyo kuanzia mwaka 1983 hadi 1985 na wakati huo gavana alikuwa ni Charles Nyirabu aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka 15 kuanzia 1974 hadi 1989. Nyirabu alipokea kijiti cha ugavana kutoka kwa Edwin Mtei mwaka 1974.

Pia baada ya Kighoma Malima kutoka katika nafasi hiyo ya uwaziri wa fedha mwaka 1985 alirudi tena kwa mara ya pili kwenye nafasi hiyo mwaka 1994 ambako alihudumu kwa miezi kadhaa tu ndani ya mwaka huo huo na baadae kufariki 1995.

Kwa hiyo kwa upande wa Mtei alikuwa gavana kuanzia 1966 hadi 1974 na pia waziri wa fedha kuanzia 1977 hadi 1979 alipohitilafiana na Mwalimu Nyerere kuhusu kukubali au kutokubaliana na utekelezaji wa masharti ya IMF.

Bob Makani alikuwa ni naibu gavana kuanzia 1974 hadi 1986 hii ikimaanisha kwamba wakati BOT inaungua Mtei hakuwa gavana pale BOT wala waziri wa fedha isipokuwa Nyirabu na Bob Makani ndiyo walikuwa ofisi moja yaani Nyirabu akiwa gavana na Makani akiwa ni naibu wake na Kighoma Malima akiwa ni waziri.
 
Bob makani alikuwa ni mmoja wa waazilishi wa chadema.
Pia umekosea kidogo tu.
Kigoma Malima aliingia 1985.
Naomba tusiwapotoshe watu. Tuweke siasa pembeni.
 
Uko sahihi mkuu,sina ubishi!!
 
Bob makani alikuwa ni mmoja wa waazilishi wa chadema.
Pia umekosea kidogo tu.
Kigoma Malima aliingia 1985.
Naomba tusiwapotoshe watu. Tuweke siasa pembeni.
Sasa mkuu haujisikii aibu kudai tuweke siasa pembeni wakati katika post yangu sijaandika chochote kuhusu siasa na badala yake wewe ndiye umekuja na habari za Chadema?

Kighoma hakuingia wizara ya fedha 1985. Aliingia 1983 na kuondoka 1985 huku nafasi yake ikichukuliwa na Cleopa Msuya 1986 ambaye alidumu pale hadi 1989. Kighoma aliporudi kwenye uwaziri huo 1994 na kuondoka mwaka huo huo ndipo Jakaya Kikwete akachukua kijiti chake kwa mwaka mmoja hadi mwaka 1995 alipomwachia Simon Mbilinyi.

Badala ya kuleta ubishi usio wa lazima ni vizuri tukatumia hata hivi vi smartphones vyetu vilivyosalimika kwenye tsunami ya TCRA kupata facts mbalimbali.
 
Sasa hapo ndio unataka kupotosha jamii kwa makusudi.
Hebu nakuomba uniambie. Ni waziri yupi aliyedumu kwada mrefu? Hivi unajua luhusu Waziri wa fedha Jamal?
Ukishamjua niambia huyo waziri Malima alianza lini uwazir!!!?

Kighoma Malima alianza 1985. Nakumba usiwapotoshe watu kuna watu hawajui hayo.
 
1. Waziri aliyedumu muda mrefu ni Ameir Jamal.
2. Ndiyo najua kuhusu Ameir Jamal. Aliyewahi kuwa waziri wa fedha kwa vipindi vitatu tofauti ambavyo ni 1965-1972, 1975-1977 na 1979-1983 alipoingia Kighoma Malima na kuhudumu hadi 1985 kabla ya kurudi tena 1994.
3. Kighoma Malima alianza uwaziri wa fedha mwaka 1983. Mkuu nimejibu maswali yako yote uliyouliza. Sioni sababu ya kuendelea kubishana juu ya hili. Mdau Mkupuo hapo juu katoa ushauri mzuri wa kujibu swali lililoulizwa "Ni Akina Nani Walichoma BOT" basi tujikite huko.
 
Back
Top Bottom