Ni aidha uwe na mvuto au uwezo wa kuwahudumia. Vinginevyo wanawake hawana simile na wewe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
Kwema Wakuu!

Weka akilini, mwanaume hujaumbwa kuchekacheka, ku-relax. Wanasema wanaume tumeumbwa Mateso na kuhangaika(mwimbaji Fulani aliimba).

Wanawake hawatakuchekea wala kukuonea huruma ukikosa hayo mambo mawili au kimojawapo. Watakudharau, watakudhihaki, watakutumikisha na kukufanya msukule wao, watahakikisha unateseka haswa.

Jambo moja ambalo wanawake wengi wanalo ni kuwa; hawana busara na hekima imewapita mbali ndio maana wanakosa huruma na watakuchana makavu pasipo kupepesa macho.

Utasikia, nikupeleke wapi na umaskini wako? Unanuka umaskini pyuu! Huna muonekano, wala hauvutii, unataka nichekwe. Unataka nizae Watoto wanilaumu. Bora hata ingekuwa unapesa kidogo kingekufikiria. Unaniletea mikosi yako tuu.

Ukishajijua huna mvuto, jitahidi utafute Pesa. Sio uwe nazo nyingi hapana, angalau zinazokutosha wewe na watu wengine kama watano hivi.

Kama vile wanaume tulivyo, ndivyo Wanawake walivyo. Nao wanapenda wanaume Wazuri, wanasisimkwa wakiona mwanaume mzuri. Wanababaika na unaweza kuwababaisha ikiwa tuu unamvuto au Una Mawe, lumbelele, shekeli au Pesa.

Kwa mwanamke utachagua option mbili ili uishi naye kwenye ndoa. Akupende sana au akuogope sana.

Mwanamke ili akupende lazima uwe dream husband wake, na moja ya vigezo vya dream husband Kwa wengi ni uzuri na mvuto. Achana na ule unafiki wao kwamba hawavutiwi na uzuri, huo ni Uongo tuu.

Ni sawa na wale wanaume wanaosema hawataki wanawake wazuri, wanatania na inaitwa sizitaki mbichi hizi.

Mwanamke anataka wenzake wamsifie pindi akiwa na wewe. Wamuoñee wivu, watake kumpindua, kisa yupo na mwanaume ambaye ni ndoto ya wanawake wengi.

Hapo ni aidha uwe na pesa (uzuri wa pesa) wanaita uzuri bandia, au uwe na uzuri wa asili ambao utazaliwa nao.

Karibuni kwa maoni.
 
Back
Top Bottom