Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,660
- 218,147
Nafahamu kwamba siasa za CCM kwa vyama vya upinzani zimejaa uadui na uhasama wa kutisha sana , na ndio maana vyama vya upinzani kwa miaka 6 sasa vimepigwa marufuku kufanya siasa za majukwaa kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi.
Lakini hatukutarajia chuki hizo zifike hadi kwenye Msiba wa Rais wa nchi kwa kushindwa kuwatambua viongozi wa upinzani na hasa Chama kikuu kama Chadema ambacho zaidi ya nusu ya Watanzania ni wafuasi wake, huu utamaduni haukuwepo kwenye nchi hii tangu enzi na enzi, ni nani ameuleta na kuusimika?
Natambua kwamba kwenye Maombolezo ya Zanzibar ACT WAZALENDO imetajwa na kutambuliwa kuwepo kwenye msiba huo , lakini itambulike kwamba ACT ni sehemu ya Serikali hasa baada ya kujumuika na ccm kwenye serikali ya umoja wa kitaifa, hivyo chama hiki huwezi kukipa jukumu la kuwakilisha wapinzani.
Mwisho: Ijulikane kwamba tunapoandika haya hatuna maana ya kugombania haki za msiba, la hasha, bali ni lazima tufahamu kwamba Msiba wa Rais ni Msiba wa Kitaifa ni vizuri kushirikisha wadau wote ili kuonyesha mshikamano, ingekuwa aliyekufa ni Katibu Mkuu wa CCM au labda Katibu Mwenezi basi bila shaka msiba huo ungebaki kuwa wa CCM na washirika wao tu.
Kamati ya Mazishi ya Msiba wa Dr Magufuli ijitafakari.
Nitasema kweli daima , Fitna kwangu mwiko .