NHIF yatoa Ufafanuzi kuhusu Dawa na Vifaa Tiba vinavyodaiwa Vimeondolewa kwenye Kitata kufuatia taarifa zinazosambaa Mitandaoni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,114
NHIF yatoa Ufafanuzi kuhusu Dawa na Vifaa Tiba vinavyodaiwa kuondolewa kwenye Kitita

Ufafanuzi unafuatia taarifa zinazosambaa Mitandaoni kwa kasi

Taarifa kamili inakujia

1710263067151.png
 
NHIF yatoa Ufafanuzi kuhusu Dawa na Vifaa Tiba vinavyodaiwa kuondolewa kwenye Kitita

Ufafanuzi unafuatia taarifa zinazosambaa Mitandaoni kwa kasi

Taarifa kamili inakujia

serikali inatakiwa kukaa chini na kujitafakari kama wameshindwa kutoa huduma ya afya kwa wapiga kura wao, wakati hapohapo wanaweza kutoa zawadi kwa wacheza mpira, na pesa nyingi zinaibiwa serikalini. kwahiyo mtu masikini asiye na uwezo kabisa wa bima, afanye nini? afe? hizo dawa atanunulia nini? inamaana serikali imebeba mzigo wa wale wanaojiweza tu, manake wale wanaonunua bima walau kiafrikaafrika tunasema wanajiweza kuliko wengine, majority ambao ni masikini ukienda pale muhimbili wanalala pale nje kwenye jengo la coca cola kwasababu they can't afford kuishi mle ndani na kulipia kitanda, kweli tuseme serikali imekosa kabisa pesa kutoa hata bima ya bure kwa watanzania wote? hizo ndege mmenunua zimetusaidia nini? mabilioni mamia hayo yanayonunua ndege mngepeleka kwenye bima ya raia huko watu watibiwe bure si mngeokoa uhai? lini tutapata viongozi wenye huruma?
 
Jana nilienda pale muhimbili, nakuambia kuna watu wanapata shida pale, hasa wa hali ya chini, they can't afford kitanda mle ndani, wanalala pale nje kwenye coca cola, hata sijui wanaoga wapi. hivi kweli serikali inashindwa kutoa bima kwa kila raia kweli? watu wanaenda pale baadhi ya dawa wanaambiwa bima hailipi, tena zile za garama, za bei rahisi izo fresh, vipimo vile vya muhimu unaambiwa bima haiwezi kucover, kama kwa mwenye bima ipo hivyo, kwa wale wametolewa kijijini hawajui hata bima ni nini mnafikiri watatibiwaje? hivi ninyi viongozi wa serikali mnaweza kulala nje pale mng'atwe na mmbu wiki nzima mnauguz amgonjwa au mnajiuguza kwasababu tu hamna hela ya kitanda? kweli, oneeni huruma watanzania masikini jamani. pesa mnazo, mnaiba tu, mnatumia safari za nje zisizo na faida, mnanunua ndege kwa mabilioni na hazina faida, ila raia masikini wanakufa mioyo ikijaa majonzi, machozi yao mnaweza kuyalipa mbele za Mungu?
 
Back
Top Bottom