Habari wakuu wa jukwaa,
Naomba msaada wenu. Ningependa kufahamu ni vigezo gani vinavyotumika kupanga bei ya nyumba hizi.
Je, bei huamuliwa kwa kuzingatia mambo kama eneo ilipo nyumba, ukubwa wa jengo, ubora wa ujenzi, huduma zilizopo, miundombinu, au kuna vigezo vingine muhimu vinavyotumika?
Nitaushukuru sana mchango wenu kwa yeyote mwenye uzoefu au taarifa juu ya hili.View attachment 3523988
Service charge hio. Nyumba yako ila kila mwezi unaweza kujikuta unalipa kodi ya pango ya Goba.Bado monthly home association payment.
Hapo unaweza ambiwa uchangie 300,000 kila mwezi for security, takataka, lift, usafi wa mazingira n.k
Hawawezi kukuelewa. Mtu kazoea aishi na bata mbuzi kuku apartments ataziweza wapi? Halafu asilimia kubwa wanaonunuq hizo sio first time home owners.
Kwa sisi tunaopenda kuishi kwenye nafasi natoa million 20 namiliki ekari mia Moja hapa pwani pembeni kabisa ya dar iliyobaki nashusha mjengo Wa maana nikipata na usafiri wangu safi kabisa halafu mtu ananiambia nitoe zaidi ya million mia kununua kile chumba?Yaani nitoe milioni 112 kwenye makazi kama mabweni ya wanafunzi wakati nikienda hao kibaha napata kiwanja kikubwa MIta 100 Kwa 100 Kwa shilingi milioni20-30.ukiishi kwenye apartment ni matumizi mabaya pa pesa