NHC: Hatujamuonea Mbowe

NHC: Hatujamuonea Mbowe

Cybercrime

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
3,246
Reaction score
1,113
NHC-620x308.jpg

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Mbowe Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya kampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.

Source:
Mwanahalisi Online
 
Suala la Mbowe ni la kibiashara zaidi. Hakufuata masharti ya kupanga. Msichanganye masuala ya biashara na siasa
Ukiishia kuandika hivyo huwezi kueleweka, hebu tuwekee in details ni namna gani hakufuata masharti-utuwekee mkataba baina ya hizo pande mbili na namna ulivyokuwa ukitekelezwa hadi kutokea yaliyotokea!
 
Yote sawa tu wafanye wapendavyo ili mioyo yao isuuzike na kupata amani. Ila, baadaye msijesema hao wengine mna utaratibu mwingine mnaotaka kuutumia kupata kodi zenu. Sheria iwe msumeno
Na pale Ufipa nimempa notice asipolipa nafukuzia mbaaaaali huko, ofisi ataweka nyumbani kwake
 
Back
Top Bottom