Nguvu ya Umma - hisia zilichomokea kwa sakata la Wamachinga na Serikali

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Kweli Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga, kama mlifuatilia fumuko la mvutano kati ya Serikali na wananchi (Wamachinga), Kuna kitu ikiwa ni wenye akili mmekisoma na faida zilizopatikana ni serikali kurudi na kunywea na kuwasikia viongozi wao wakisema....endeleeni...bakieni....malizeni kuorodhesha majina yenu na misamiati kibao, na waliohojiwa.

Inawezekana kabisa ni waunga juhudi ambao wamekuja na nembo ya kuisifu serikali na kama haioshi kwa kuwapa muda na zaidi kuwapangia meneo, yote ni tukubali serikali imeshindwa kutumia mabavu katika kuwahamisha.

Wamachinga kwa umoja wao walisimama japo kuna sehemu walivurugana wenyewe kwa wenyewe, lakini asilimia kubwa walikuwa damu inawachemka.

Sasa nafikiria hali hii ikija kufikia stage ya mambo ya kisiasa, Tunadai katiba mpya, tume huru halafu umma usimame mfano wa kuushinda msimamo wa wamachinga. Lazima miCCM itakuwa zamu yao kuhama nchi tena kwa makundi.
 
Sijaona msimamo wowote kwa machinga. Watanzania ni walewale.
Afteral wamachinga ni wavunjaji wa sheria, hivyo msomamo wao hauwezi kuwa na nguvu dhidi ya sheria.
 
Back
Top Bottom