Nguvu ya saikolojia

DIDAS TUMAINI

Senior Member
Nov 11, 2014
154
500
Na Dr.Christopher Cyrilo

Siku moja, mtu mmoja alitoka nyumbani kuelekea hospitalini kwa sababau ya maumivu makali aliyokuwa nayo mkono wa kulia.

Alipokutana na daktari, alimueleza namna mkono ule unavyouma hadi kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.
Daktari alipougusa, mtu yule alitoa sauti kubwa inayoashiria maumivu makali.

Daktari, akahisi kuwapo kwa tatizo kubwa zaidi ya maumivu yale. Mtu yule hakuwa amepata ajali, hakuwa amepigwa, hakuwa ameanguka. Hakukuwa na jibu la sababu ya maumivu yake kutoka katika maelezo yake. Uchunguzi wa papo kwa papo aliofanya daktari nao haukutoa majibu yoyote. Kwahiyo tegemeo pekee alilobaki nalo daktari ni vipimo.
Hata hivyo vipimo havikuonesha tatizo lolote.

Daktari alibaki na kitendawili kigumu akilini mwake. Aliwaza kama kweli mtu huyo anaugua au anajifanya kuugua. Lakini kwa tahadhari kubwa, aliendelea kuonesha kujali. Ndipo alipouliza zaidi na zaidi na kugundua kuwa yule jamaa alikuwa na matatizo makubwa kwenye ndoa yake. Matatizo ya miaka kadhaa hivi.

Nyumbani kwake hakukuwa na amani hata kidogo, mkewe na watoto wake walikuwa wamemtenga baba yao, kutokana na makosa aliyotenda huko nyuma. Pia, wazazi na baadhi ya ndugu wa huyo jamaa walifariki kwa pamoja kwenye ajali ya gari la familia. Kwa matukio hayo na kutosamehewa na mke na watoto, yule jamaa aliathirika kisaikolojia kiasi cha kuwa na dalili za maradhi ya akili.

Mojawapo ya dalili hizo ni hiyo ya kuhisi maumivu yasiyokuwepo.
Kwa kuwa ubongo ndio unaotafsiri maumivu, bila ubongo mtu hawezi kuhisi maumivu. Na endapo kuna athari katika sehemu ya ubongo inayotafsiri maumivu ya sehemu fulani ya mwili, basi kuna uwezekano mtu kupata maumivu sehemu hiyo ya mwili hata kama hakuna sababu katika sehemu husika, lakini kama kuna tatizo la kiakili/kwenye ubongo.

Dalili za aina hii hutokea kwa nadra. Mara nyingi huanza kwa hisia za kutambaliwa na mdudu mwilini wakati hakuna kitu (Tactile Hallucinations); kisha huweza kuendelea zaidi na kufikia kupata maumivu, kwa sababu za kisaikolojia.

Yule daktari alipogundua uwezekano wa maradhi ya akili kwa mtu yule, aliamua kubadili mbinu za kumsaidia. Alimpa ushauri, na uhakika wa kupona, na dawa za maumivu. Kisha akamualika nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha jioni.

Siku fulani jioni, yule jamaa alifika nyumbani kwa daktari wake. Daktari alimkaribisha na kuanza kupiga naye stori bila kumuuliza hali ya mkono wake. Stori nyingi zilikuwa za kuchekesha au kufurahisha. Baada ya muda, Daktari alimkaribisha yule jamaa ndani kwa ajili ya chakula, huku stori zikiendelea.

Kwa makusudi kabisa, Daktari alimkabidhi yule jamaa birika la chai, upande wake wa kulia wa yule jamaa, naye alipokea kwa mkono wa kulia (uliokuwa na maumivu) na kuanza kumimina chai kwenye kikombe. Wakati jamaa akiendelea kumimina chai, kulikuwa na ukimya, lakini daktari alikuwa akitazama ule mkono kwa mshangao kidogo.

Yule jamaa alipogundua daktari anautazama mkono wake, mara moja mkono ukaanza kuuma, akaliachia lile birika la chai na kuanza kupiga kelele za maumivu.

Tendo hilo liliweza kumpatia majibu ya uhakika daktari, kwamba maumivu yale yalisababishwa na maradhi ya kisaikolojia.

Saikolojia ni elimu pana sana. Ndio daraja linalounganisha imani na sayansi, na ndio ukuta unaotenganisha mambo hayo mawili.
Tazama wagonjwa wa akili wanaozurura barabarani na kula takataka chafu lakini wanaendelea kuishi. Kula wewe unayejua kuwa ni uchafu uone kitakachotokea.

Umewahi kubanwa na tumbo la kuendesha? Fikiria unavyokaribia chooni na hali unayoisikia, kadiri unavyokikaribia choo, hali inakuwa mbaya zaidi. Lakini ukikuta kuna mtu bado unaweza kuvumilia, huyo mtu akitoka hali inaanza kuwa mbaya zaidi wakati unaingia kujisaidia. Ukichelewa tu unachafua nguo.

Wamasai na jamii nyingine wanaishi na kupishana na simba porini, ni saikolojia.
Mtoto mdogo anayetambaa anacheza na nyoka, ni saikolojia.

Saikolojia inaathiri sana maisha yetu, uchumi wetu, afya zetu na mahusiano yetu.
Cha msingi ni kujifunza kwamba; kuna nguvu kubwa katika ubongo wa binadamu. Nguvu hiyo ni kubwa kuliko mbingu na ardhi kwa pamoja.

Ndio nguvu inayobadili mambo madogo kuwa makubwa na makubwa kuwa madogo. Ndio nguvu inayofanya ya muhimu yasiwe muhimu na yasio muhimu yawe na umuhimu mkubwa.
Itaendelea.

Christopher Cyrilo
 
Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
488
500
Kweli kabisa, na jamii nyingi za kiafrika zinateketea kwa kutokufahamu mambo kama hayo, na cha kuhuzunisha kabisa ni kuwa hawapo tayari kujifunza hata kidogo, ila mwisho wa siku kila tatizo wanasema serikali haijatoa elimu.
 
doughter

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
446
500
Na Dr.Christopher Cyrilo

Siku moja, mtu mmoja alitoka nyumbani kuelekea hospitalini kwa sababau ya maumivu makali aliyokuwa nayo mkono wa kulia.
Alipokutana na daktari, alimueleza namna mkono ule unavyouma hadi kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.
Daktari alipougusa, mtu yule alitoa sauti kubwa inayoashiria maumivu makali.

Daktari, akahisi kuwapo kwa tatizo kubwa zaidi ya maumivu yale. Mtu yule hakuwa amepata ajali, hakuwa amepigwa, hakuwa ameanguka. Hakukuwa na jibu la sababu ya maumivu yake kutoka katika maelezo yake. Uchunguzi wa papo kwa papo aliofanya daktari nao haukutoa majibu yoyote. Kwahiyo tegemeo pekee alilobaki nalo daktari ni vipimo.
Hata hivyo vipimo havikuonesha tatizo lolote.
Daktari alibaki na kitendawili kigumu akilini mwake. Aliwaza kama kweli mtu huyo anaugua au anajifanya kuugua. Lakini kwa tahadhari kubwa, aliendelea kuonesha kujali. Ndipo alipouliza zaidi na zaidi na kugundua kuwa yule jamaa alikuwa na matatizo makubwa kwenye ndoa yake. Matatizo ya miaka kadhaa hivi. Nyumbani kwake hakukuwa na amani hata kidogo, mkewe na watoto wake walikuwa wamemtenga baba yao, kutokana na makosa aliyotenda huko nyuma. Pia, wazazi na baadhi ya ndugu wa huyo jamaa walifariki kwa pamoja kwenye ajali ya gari la familia. Kwa matukio hayo na kutosamehewa na mke na watoto, yule jamaa aliathirika kisaikolojia kiasi cha kuwa na dalili za maradhi ya akili.
Mojawapo ya dalili hizo ni hiyo ya kuhisi maumivu yasiyokuwepo.
Kwa kuwa ubongo ndio unaotafsiri maumivu, bila ubongo mtu hawezi kuhisi maumivu. Na endapo kuna athari katika sehemu ya ubongo inayotafsiri maumivu ya sehemu fulani ya mwili, basi kuna uwezekano mtu kupata maumivu sehemu hiyo ya mwili hata kama hakuna sababu katika sehemu husika, lakini kama kuna tatizo la kiakili/kwenye ubongo. Dalili za aina hii hutokea kwa nadra. Mara nyingi huanza kwa hisia za kutambaliwa na mdudu mwilini wakati hakuna kitu (Tactile Hallucinations); kisha huweza kuendelea zaidi na kufikia kupata maumivu, kwa sababu za kisaikolojia.

Yule daktari alipogundua uwezekano wa maradhi ya akili kwa mtu yule, aliamua kubadili mbinu za kumsaidia. Alimpa ushauri, na uhakika wa kupona, na dawa za maumivu. Kisha akamualika nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha jioni.

Siku fulani jioni, yule jamaa alifika nyumbani kwa daktari wake. Daktari alimkaribisha na kuanza kupiga naye stori bila kumuuliza hali ya mkono wake. Stori nyingi zilikuwa za kuchekesha au kufurahisha. Baada ya muda, Daktari alimkaribisha yule jamaa ndani kwa ajili ya chakula, huku stori zikiendelea.
Kwa makusudi kabisa, Daktari alimkabidhi yule jamaa birika la chai, upande wake wa kulia wa yule jamaa, naye alipokea kwa mkono wa kulia (uliokuwa na maumivu) na kuanza kumimina chai kwenye kikombe. Wakati jamaa akiendelea kumimina chai, kulikuwa na ukimya, lakini daktari alikuwa akitazama ule mkono kwa mshangao kidogo. Yule jamaa alipogundua daktari anautazama mkono wake, mara moja mkono ukaanza kuuma, akaliachia lile birika la chai na kuanza kupiga kelele za maumivu.

Tendo hilo liliweza kumpatia majibu ya uhakika daktari, kwamba maumivu yale yalisababishwa na maradhi ya kisaikolojia.

Saikolojia ni elimu pana sana. Ndio daraja linalounganisha imani na sayansi, na ndio ukuta unaotenganisha mambo hayo mawili.
Tazama wagonjwa wa akili wanaozurura barabarani na kula takataka chafu lakini wanaendelea kuishi. Kula wewe unayejua kuwa ni uchafu uone kitakachotokea.
Umewahi kubanwa na tumbo la kuendesha? Fikiria unavyokaribia chooni na hali unayoisikia, kadiri unavyokikaribia choo, hali inakuwa mbaya zaidi. Lakini ukikuta kuna mtu bado unaweza kuvumilia, huyo mtu akitoka hali inaanza kuwa mbaya zaidi wakati unaingia kujisaidia. Ukichelewa tu unachafua nguo.

Wamasai na jamii nyingine wanaishi na kupishana na simba porini, ni saikolojia.
Mtoto mdogo anayetambaa anacheza na nyoka, ni saikolojia.

Saikolojia inaathiri sana maisha yetu, uchumi wetu, afya zetu na mahusiano yetu.
Cha msingi ni kujifunza kwamba; kuna nguvu kubwa katika ubongo wa binadamu. Nguvu hiyo ni kubwa kuliko mbingu na ardhi kwa pamoja.
Ndio nguvu inayobadili mambo madogo kuwa makubwa na makubwa kuwa madogo. Ndio nguvu inayofanya ya muhimu yasiwe muhimu na yasio muhimu yawe na umuhimu mkubwa.
Itaendelea...

Christopher Cyrilo
Ni kweli aisee nimekumbuka nikisex siku za hatari uwa nakua na wasiwasi sana cha ajabu kama uwa na nablidi tarehe 12 basi inaeza sogea mbka 20 sijui ndo hofu alafu mbka dalili za mimba nakua nazisikia kumbe hamna kitu asa nikianza blidi nakua najiuliza kile kichefuchefu kilitoka wapi na mbona nilianza adi kuchagua vyakula yaan uwa nashangaaga na sio mara moja afu sio kwangu tuu vile akili unavowaza na mwili unareact hahaa eti mbka kutapika kumbe tumboni hamna kitu..dah.
 
Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
44,364
2,000
Saikolojia inaathiri sana maisha yetu, uchumi wetu, afya zetu na mahusiano yetu.
Cha msingi ni kujifunza kwamba; kuna nguvu kubwa katika ubongo wa binadamu. Nguvu hiyo ni kubwa kuliko mbingu na ardhi kwa pamoja.
Ndio nguvu inayobadili mambo madogo kuwa makubwa na makubwa kuwa madogo. Ndio nguvu inayofanya ya muhimu yasiwe muhimu na yasio muhimu yawe na umuhimu mkubwa.
UMESOMEKA MKUU
 
Truth Teller

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
1,249
2,000
Kuhusu bipolar je?
Na Dr.Christopher Cyrilo

Siku moja, mtu mmoja alitoka nyumbani kuelekea hospitalini kwa sababau ya maumivu makali aliyokuwa nayo mkono wa kulia.
Alipokutana na daktari, alimueleza namna mkono ule unavyouma hadi kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.
Daktari alipougusa, mtu yule alitoa sauti kubwa inayoashiria maumivu makali.

Daktari, akahisi kuwapo kwa tatizo kubwa zaidi ya maumivu yale. Mtu yule hakuwa amepata ajali, hakuwa amepigwa, hakuwa ameanguka. Hakukuwa na jibu la sababu ya maumivu yake kutoka katika maelezo yake. Uchunguzi wa papo kwa papo aliofanya daktari nao haukutoa majibu yoyote. Kwahiyo tegemeo pekee alilobaki nalo daktari ni vipimo.
Hata hivyo vipimo havikuonesha tatizo lolote.
Daktari alibaki na kitendawili kigumu akilini mwake. Aliwaza kama kweli mtu huyo anaugua au anajifanya kuugua. Lakini kwa tahadhari kubwa, aliendelea kuonesha kujali. Ndipo alipouliza zaidi na zaidi na kugundua kuwa yule jamaa alikuwa na matatizo makubwa kwenye ndoa yake. Matatizo ya miaka kadhaa hivi. Nyumbani kwake hakukuwa na amani hata kidogo, mkewe na watoto wake walikuwa wamemtenga baba yao, kutokana na makosa aliyotenda huko nyuma. Pia, wazazi na baadhi ya ndugu wa huyo jamaa walifariki kwa pamoja kwenye ajali ya gari la familia. Kwa matukio hayo na kutosamehewa na mke na watoto, yule jamaa aliathirika kisaikolojia kiasi cha kuwa na dalili za maradhi ya akili.
Mojawapo ya dalili hizo ni hiyo ya kuhisi maumivu yasiyokuwepo.
Kwa kuwa ubongo ndio unaotafsiri maumivu, bila ubongo mtu hawezi kuhisi maumivu. Na endapo kuna athari katika sehemu ya ubongo inayotafsiri maumivu ya sehemu fulani ya mwili, basi kuna uwezekano mtu kupata maumivu sehemu hiyo ya mwili hata kama hakuna sababu katika sehemu husika, lakini kama kuna tatizo la kiakili/kwenye ubongo. Dalili za aina hii hutokea kwa nadra. Mara nyingi huanza kwa hisia za kutambaliwa na mdudu mwilini wakati hakuna kitu (Tactile Hallucinations); kisha huweza kuendelea zaidi na kufikia kupata maumivu, kwa sababu za kisaikolojia.

Yule daktari alipogundua uwezekano wa maradhi ya akili kwa mtu yule, aliamua kubadili mbinu za kumsaidia. Alimpa ushauri, na uhakika wa kupona, na dawa za maumivu. Kisha akamualika nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha jioni.

Siku fulani jioni, yule jamaa alifika nyumbani kwa daktari wake. Daktari alimkaribisha na kuanza kupiga naye stori bila kumuuliza hali ya mkono wake. Stori nyingi zilikuwa za kuchekesha au kufurahisha. Baada ya muda, Daktari alimkaribisha yule jamaa ndani kwa ajili ya chakula, huku stori zikiendelea.
Kwa makusudi kabisa, Daktari alimkabidhi yule jamaa birika la chai, upande wake wa kulia wa yule jamaa, naye alipokea kwa mkono wa kulia (uliokuwa na maumivu) na kuanza kumimina chai kwenye kikombe. Wakati jamaa akiendelea kumimina chai, kulikuwa na ukimya, lakini daktari alikuwa akitazama ule mkono kwa mshangao kidogo. Yule jamaa alipogundua daktari anautazama mkono wake, mara moja mkono ukaanza kuuma, akaliachia lile birika la chai na kuanza kupiga kelele za maumivu.

Tendo hilo liliweza kumpatia majibu ya uhakika daktari, kwamba maumivu yale yalisababishwa na maradhi ya kisaikolojia.

Saikolojia ni elimu pana sana. Ndio daraja linalounganisha imani na sayansi, na ndio ukuta unaotenganisha mambo hayo mawili.
Tazama wagonjwa wa akili wanaozurura barabarani na kula takataka chafu lakini wanaendelea kuishi. Kula wewe unayejua kuwa ni uchafu uone kitakachotokea.
Umewahi kubanwa na tumbo la kuendesha? Fikiria unavyokaribia chooni na hali unayoisikia, kadiri unavyokikaribia choo, hali inakuwa mbaya zaidi. Lakini ukikuta kuna mtu bado unaweza kuvumilia, huyo mtu akitoka hali inaanza kuwa mbaya zaidi wakati unaingia kujisaidia. Ukichelewa tu unachafua nguo.

Wamasai na jamii nyingine wanaishi na kupishana na simba porini, ni saikolojia.
Mtoto mdogo anayetambaa anacheza na nyoka, ni saikolojia.

Saikolojia inaathiri sana maisha yetu, uchumi wetu, afya zetu na mahusiano yetu.
Cha msingi ni kujifunza kwamba; kuna nguvu kubwa katika ubongo wa binadamu. Nguvu hiyo ni kubwa kuliko mbingu na ardhi kwa pamoja.
Ndio nguvu inayobadili mambo madogo kuwa makubwa na makubwa kuwa madogo. Ndio nguvu inayofanya ya muhimu yasiwe muhimu na yasio muhimu yawe na umuhimu mkubwa.
Itaendelea...

Christopher Cyrilo
 
Brightdeemed

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
291
250

Content kubwa sana hii, ubarikiwe ndugu kwa ku share
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom