Umewahi kusikia kitu kinaitwa Tego?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Umri wangu sio mdogo, unatosha kabisa kunifanya nami niwe Kamhenga ingawa si Mhenga kamili hivyo kama nyani mzee tu nimekwepa mishale mingi.

Miaka ya 2000+ Nilikuwa Field Lindi, Pitapita ya hapa na pale nikazama kwa mke wa mtu bila kujua (Nilidanganywa) hapo ndo nikakutana na hiyo kitu inaitwa Tego.... Mateso niliyoyapata siwezi kusahau.

Mwanzo nilifikiri ni ugonjwa wa kawaida, Namshukuru daktari mmoja ambaye aliniita chemba na kunieleza wazi kuwa tatizo ninalopambana nalo kwake Si la kawaida hivyo akanisaidia wapi niende, kweli nikapelekwa kijijini (Chiuta) na ndugu wa huyo Daktari. kuhusu mtaalam aliyenitibu kwa sasa ni Marehemu..

TATIZO LILIVYO KUWA.
Nilikuwa nakojoa mkojo mweusi kama oil chafu, nikishakojoa yalikuwa yanafuata maumivu makali ya kiuno na Sehemu za siri zilikuwa zinawaka moto na wakati mwingine kuvimba.

Nje ya yule Daktari, mdogo wake na yule mganga (Marehemu) sijawahi kumueleza yeyote siri hii, Leo naliweka hadharani ili mpate kujifunza maana ni takribani miaka 21 sasa.

Yule mzee alikataa kunisaidia mpaka pale alipojihakikishia kuwa sikutembea makusudi na Mke wa mtu. Mwisho alinionesha majani ambayo siyajui jina ambayo alisema unaweza kutumia kumgundua Mwanamke aliyetegwa.

Muhimu:
Jiepusheni na wake za watu ndugu zangu, kuna watu wanakufa bila kugundua chanzo ni hao wanawake.

Nawatakia usiku mwema.
 
Nilienda Tanga Miaka mitatu iliyopita huko ndiko nilijua kuhusu hilo neno TEGO.

Kwa kifupi ni kama kifungo huwa anawekewa mwanamke ili asiwe ana tembea na wanaume anaweza kuwa MKE wa mtu au Mwanafunzi wa kike.

Wewe mwanaume ukienda lala naye basi hilo TEGO litakupata.

Hapo hapo utapatwa na maumivu makali sana ya kiuno na sehemu za siri usipo wahi KUTEGUA umaweza kufa bila ya utani, anaye tegua ni aliye liweka mara nyingi ni mzazi au mume wa huyo mke wa mtu.

Ni mambo ya Waganga wa kienyeji ni kama ushirikina fulani hivi.

So waka niambia huko kijijini kwakuwa nilikuwa mgeni basi niwe makini sana niache tabia ya kutembea na wake au watoto za watu.

VIJANA Wengi wamekufa kisa TEGO.
 
Ukiachana na hayo, kuna hili TEGO, ukitembea na mwanamke aliyetegwa, mwili unakufa gazi
1. Huwezi kuongea lakini unasikia kinachozungumuzwa
2. Huwezi kupumua lakini upo hai,
3. Huwezi kujitikisa, wala kujigeuza,

Watu watazani umekufa kumbe hujafa, hivyo utaenda kuzikwa makaburini wakati bado upo hai 😥😥,
1. Unavyo pelekwa makaburini utasikia na
2. sauti za ndugu jamaa na marafiki wanavyoomboleza utasikia , ila ndo hivyo Huwezi kufanya chocote. R. I. P
 
Ukiachana na hayo, kuna hili TEGO, ukitembea na mwanamke aliyetegwa, mwili unakufa gazi
1. Huwezi kuongea lakini unasikia kinachozungumuzwa
2. Huwezi kupumua lakini upo hai,
3. Huwezi kujitikisa, wala kujigeuza,

Watu watazani umekufa kumbe hujafa, hivyo utaenda kuzikwa makaburini wakati bado upo hai 😥😥,
1. unavyo pelekwa makaburini utasikia na
2. sauti za ndugu jamaa na marafiki wanavyoomboleza utasikia , ila ndo hivyo Huwezi kufanya chocote. R. I. P
Mmmh ipo hii?!
 
Back
Top Bottom