Nguvu Ya CHADEMA Kigoma:Kuna Wabunge na Madiwani Wangapi Wa CHADEMA?

Uipinzani wako wengi lakini si chadema kwa mujibu wa memba wenye data.

KWa sababu waliwatimua dakika za mwisho sasa walitegemea nini? ama ndio ilikuwa njama kuwatimua ili kigoma ikose wabunge wa CHADEMA harafu baadae aje ahojiwe Zitto badala ya kamati iliyo watimu?
 
Kwani hujui aliwapigia kampeni kwa tiketi ya nccr?Kwahio tukisema amejenga nccr huko Kigoma ntakuwa nimekosea?Again,it comes with a territory,kungekuwa na diwani zaidi ya mmoja asingetake cedit?
 
Kwani hujui aliwapigia kampeni kwa tiketi ya nccr?Kwahio tukisema amejenga nccr huko Kigoma ntakuwa nimekosea?

Kampeni ni ku stamp tu kazi ambayo inakuwa imefanyika kwa kipindi cha miaka 5. ile kampeni ya mwezi haibadirishi matokeo. Zitto na CHADEMA iliwajenga hao vijana watatu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 4, na kuivunja ndani ya kipindi cha siku za kampeni nafikiri ni ngumu. Wenda chadema waliwatimua kwa kuhofia kwamba kungetoka wabunge hao 4 kutokea kigoma, nguvu ya CHADEMA ingehamia kigoma na kuweza kumpa Zitto uenyekiti....

Sijui kama aliwapigia kampeni, na hata hivyo, na kama aliwapigia kampeni kwenye chama tofauti na bado wananchi wakamsikiliza wakawapa ubunge, sasa wewe huoni kua kweli Zitto ana nguvu kule Kigoma kwamba anaweza dictate terms?
 
Yea,ana nguvu lakini si chama.NCCR ndo ina nguvu.
 
Yeah, kwa sababu CHADEMA walipendelea NCCR iwe na nguvu. CHADEMA pamoja na Zitto wamewajenga hao vijana kwa kipindi cha karibu ya miaka 4 nusu, na kisha kuwatimua.
Anayetakiwa hapa kuhojiwa ni hiyo kamati kwanini ilitumia resources kwa kuwajenga hao vijana na kisha kuwatimu gafra dakika ya mwisho. Ni CHADEMA ndo imewajenga hao vijana kwa manufaa ya NCCR, kujaribu kumbebesha mzigo Zitto nafikiri si uungwana. Ni CHADEMA hao hao ndo walitaka Kigoma wasiwe na wabunge wa kutosha, kumuuliza leo Zitto na kuiacha kamati iliyowatimua si uungwana.

Ni sawa na kujenga watoto kisoka mpaka wakafikia kupiga soka vizuri kabisa, dakika chache kabla ya legi kuanza, mkawatimua wachazaji wenu hawa mliowajenga na wakahamia team pinzani. Mkikutana nao kwenye match wakawapiga mabao mtalaumu mshika kibendera? ama mtalaumu aliyewatimua wachezaji wenu dakika za majeruhi?
 
Kuna mambo kadhaa yanayonifanya niseme wazi kuendelea na zito ndani nikuiuwa chadema

1. Unafsi

ZZK amekuwa mbinafsi kwa muda mrefu hufanya mambo kwa faida zake/kujitengenezea umaarufu.

Kwenye harakati za kichama ambazo zinashirikisha viongozi wenzake ZZK maranyingi kama si zote hashiriki,

Kiongozi anayeendekeza oneshowman ni mpuuzi na hafai katika chama.

2. ZZK fundi wa kuunda migogoro

-Shonza, mtela nawengine walifukuzwa kwasababu ya zzk kutengeneza malengo yake nje ya utaratibu wa kichama.

-Kule mkowani mara, mwigamba wa Arusha na mkumbo wa singida ni wahanga wa siasa za makundi za ZZK

3. mchochezi ndani ya chama

-Alichochechea tena kwa maandishi Lwakatare afukuzwe kwa video feki ya mwigulu ambayo chanzo chake ni ZZK
Na mwigulu walipoipromoti katika kipindi cha tuongee asubuhi Star TV

Huwezi kujenga chama imara unapokuwa na chawa ndani ya nguo akikuteketeza tena kwa mikasa na vituko mfululizo.

Huwezi kujenga chama imara kwa kuwa na mtu asiefanya mjumuiko wa pamoja na viongozi wenzake, chama nizaidi ya mtu

Huwezi kujenga chama imara kwa kufuga mvurugaji eti kwasababu anakubalika mkowa mmoja, hakuna chama cha mkowa mmoja, huu nao niupuuzi wa ainayake

Kwa maana hiyo, heshima, umoja na mshikamano wa chadema utatukuka endapo zzk atafukuzwa ilichama kujitofautishe na ccm.
 
Chadema walisema siku 14 zikifika watakuwa wameshampa adhabu Zitto. Tangu waseme hivyo huu ni mwezi wa pili sasa!

Nguvu ya Zitto walikuwa hawaijui mpaka pale Slaa alipoweka historia ya kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kufurumushwa na mawe na wananchi wazalendo wenye hasira kali!
arrgh...
 
Yeah, kwa sababu CHADEMA walipendelea NCCR iwe na nguvu. CHADEMA pamoja na Zitto wamewajenga hao vijana kwa kipindi cha karibu ya miaka 4 nusu, na kisha kuwatimua.
Anayetakiwa hapa kuhojiwa ni hiyo kamati kwanini ilitumia resources kwa kuwajenga hao vijana na kisha kuwatimu gafra dakika ya mwisho. Ni CHADEMA ndo imewajenga hao vijana kwa manufaa ya NCCR, kujaribu kumbebesha mzigo Zitto nafikiri si uungwana. Ni CHADEMA hao hao ndo walitaka Kigoma wasiwe na wabunge wa kutosha, kumuuliza leo Zitto na kuiacha kamati iliyowatimua si uungwana.

Ni sawa na kujenga watoto kisoka mpaka wakafikia kupiga soka vizuri kabisa, dakika chache kabla ya legi kuanza, mkawatimua wachazaji wenu hawa mliowajenga na wakahamia team pinzani. Mkikutana nao kwenye match wakawapiga mabao mtalaumu mshika kibendera? ama mtalaumu aliyewatimua wachezaji wenu dakika za majeruhi?
Wewe umeshasema eti chadema hawakutaka wabunge wa kutosha Kigoma ili asipate uenyekiti.Hilo ni sawa na kutapa tapa tu.Hapa wala simlaumu Zitto,bali najiuliza hiyo nguvu ya chadema Kigoma,chama kinajengwa,na matokeo ya ujenzi huko Kigoma ndo yana utata.
 
Mie nimekwambia toka awali ya kwamba huwezi pima kwa kuangalia wabunge wa CHADEMA wako wangapi, kwa sababu wabunge mliwatimua dakika ya mwisho. Ni sawa na leo Zitto atimuliwe harafu jamaa mwingine aje aseme CHADEMA haina wanachma kabisa kigoma kwa sababu hatuna mbunge hata mmoja. CHADEMA iliwatimua wabunge watarajiwa, hivyo kigezo hicho tunaki disqualify.

Kigezo halali cha kupima CHADEMA wana nguvu gani kigoma ni kipimo cha kupima kwenye Kura za urais, kwa sababu hiki ndicho kipimo std kwa sehemu yote ya nchi kwa sababu mgombea wa urais alikuwa yuleyule nchi nzima.
Kutumia kipimo cha wabunge hata kama wasingekuwa wametimuliwa akina Kafulila sio sahihi, kwa sababu watu hawawezi mpa tu mtu ubunge eti kwa sababu anatoka CHADEMA. Kura za urais ndio mwafaka maana ni yuleyule across the country.
 
Mkuu jmushi1 huyu sito sijui zito ana nguvu kubwa ya usaliti. Niliwahi kuanzisha thread inayozungumzia mpango wa zito kumsimika Kafulila, kwanini alimsponsor mwana nccr ma..., na siyo cdm? kwenye jimbo hilo angekuwepo mwana cdm zto angemsapoti yupi cdm au nccr madude? kama cdm hakuwepo mgombea kwanini hakumuweka /kumwandaa?
 
Last edited by a moderator:
Watanzania itakua ngumu sana kuendelea kwasababu katika siasa tunashabikia sana watu kuliko sela za vyama na kwahili itakuwa ngumu sana kupata mabadiliko kwani ushabiki huu ndo huwafanya wanasiasa wanao shabikiwa kujiona miungu watu na hivyo kufanya watakavyo eti wakiguswa chama kita kitasambalatika? ujinga hapa hakuna mjadala atimuliwe ili kuonyesh nidhamu kwenye katiba basi Zito sio CHADEMA,Hata yeye alikikuta.

Ni kweli kabisa unayosema lakini isiwe upande mmoja Mbowe naye afukuzwe kwa ufuska
 
Wewe umeshasema eti chadema hawakutaka wabunge wa kutosha Kigoma ili asipate uenyekiti.Hilo ni sawa na kutapa tapa tu.Hapa wala simlaumu Zitto,bali najiuliza hiyo nguvu ya chadema Kigoma,chama kinajengwa,na matokeo ya ujenzi huko Kigoma ndo yana utata.

post yangu ikijibiwa hapo juu tutapata majibu ya hili
 
Yeah, kwa sababu CHADEMA walipendelea NCCR iwe na nguvu. CHADEMA pamoja na Zitto wamewajenga hao vijana kwa kipindi cha karibu ya miaka 4 nusu, na kisha kuwatimua.
Anayetakiwa hapa kuhojiwa ni hiyo kamati kwanini ilitumia resources kwa kuwajenga hao vijana na kisha kuwatimu gafra dakika ya mwisho. Ni CHADEMA ndo imewajenga hao vijana kwa manufaa ya NCCR, kujaribu kumbebesha mzigo Zitto nafikiri si uungwana. Ni CHADEMA hao hao ndo walitaka Kigoma wasiwe na wabunge wa kutosha, kumuuliza leo Zitto na kuiacha kamati iliyowatimua si uungwana.

Ni sawa na kujenga watoto kisoka mpaka wakafikia kupiga soka vizuri kabisa, dakika chache kabla ya legi kuanza, mkawatimua wachazaji wenu hawa mliowajenga na wakahamia team pinzani. Mkikutana nao kwenye match wakawapiga mabao mtalaumu mshika kibendera? ama mtalaumu aliyewatimua wachezaji wenu dakika za majeruhi?
Hizi ndizo hoja ambazo baadhi ya wanaCHADEMA hawataki kuziangalia kwa undani hasa ikichukuliwa kuwa mazingira ya siasa za Tanzania ziko based on personality na siyo kitaasisi.

Jaribu kuangalia tu hata kwenye vyama vingine kama CCM utagundua vivyo hivyo.

Hata CCM wamepoteza majimbo na kata nyingi kwa sababu ya kuwaengua watu dakika za mwisho ambao wametumia miaka zaidi ya minne na nusu kujijenga ndani ya jamii. Matokeo yake, baada ya hao watu kuondoka na kujiunga na vyama vingine, walijikuta CCM wakikosa pia majimbo na kata.

NCCR-Mageuzi imepewa nguvu kisiasa Kigoma na maamuzi ya CHADEMA ya kuwafukuza waliokuwa wanaCHADEMA katika dakiki za mwisho. Baada ya hawa jamaa kufukuzwa, haikuwezekana Mh. Zitto kuanza kupambana nao tena katika majukwaa kutokana na urafiki wa karibu sana kisiasa na kijamii.

Katika mazingira hayo, huwezi kupima nguvu za mtu kisiasa na hasa katika siasa za Tanzania.
 
Binafsi naona chama chenye nguvu kigoma ni nccr, ikifuatia Chadema na kisha maccm! Maana Nccr wana wabunge wa nne wa kuchaguliwa, chadema mmoja, na ccm wabunge wa 3!

Sasa kwa hayo majimbo hapo utasemaje chadema ya pili au ndio Jf pro kuna wapiga kura na nyie wapiga domo voo
 
Mie nimekwambia toka awali ya kwamba huwezi pima kwa kuangalia wabunge wa CHADEMA wako wangapi, kwa sababu wabunge mliwatimua dakika ya mwisho. Ni sawa na leo Zitto atimuliwe harafu jamaa mwingine aje aseme CHADEMA haina wanachma kabisa kigoma kwa sababu hatuna mbunge hata mmoja. CHADEMA iliwatimua wabunge watarajiwa, hivyo kigezo hicho tunaki disqualify.

Kigezo halali cha kupima CHADEMA wana nguvu gani kigoma ni kipimo cha kupima kwenye Kura za urais, kwa sababu hiki ndicho kipimo std kwa sehemu yote ya nchi kwa sababu mgombea wa urais alikuwa yuleyule nchi nzima.
Kutumia kipimo cha wabunge hata kama wasingekuwa wametimuliwa akina Kafulila sio sahihi, kwa sababu watu hawawezi mpa tu mtu ubunge eti kwa sababu anatoka CHADEMA. Kura za urais ndio mwafaka maana ni yuleyule across the country.
Sasa unataka tujikite kwenye kujadili chama kutimuwa wasaliti na huku chadema ina diwani mmoja tu?halafu kuna memba anasema chadema itayumba kwasababu ya mapokezi aliyoyapata,ndo nikauliza kuhusu mafanikio ya chama Kigoma.
 
Kifupi zitto alikuwa ananadi majimbo 16 chakushangaza yeye pekeyake ndo alishinda tena kwaidadi ndogo yakura huku akipata madiwani wawili kwenye jimbo like Uyo ndio naibu katibu mkuu wachama.
 
Nafikiri ingekuwa vyema pia kubainisha kura za urais kila mkoa CHADEMA walizopata hiki nafikiri ndo kipimo sahihi. Maana madiwani na ubunge mara nyingi ni wangombea wa palepale na mara nyingi hawangalii chama zaidi, bali mshikaji wao. Kura za urais nafikiri ndo kipimo sahihi.

ni hizi hapa
1. Arusha (163560/357093 ) x 100 = 45.8 %

2. Kigoma (
148892/
349006 ) x 100 =42.7%

3. Kilimanjaro (
139392/
372229 ) x 100 =37.5%

4. Manyara ( 131951/
208458 ) x 100 =63.3%

chanzo ni https://www.jamiiforums.com/tanzani...oma-kilimanjaro-manyara-na-arusha-2010-a.html
au unaweza kuingia website ya nec
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom