Makonda anafanya kazi ya wabunge na madiwani

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,266
Mfumo sahihi wa kusikiliza na kutatua kero za raia ni kupitia madiwani na wabunge, sio katibu mwenezi wa chama cha siasa.

Madiwani wanatakiwa wafanye mikutano ya kusikiliza kero za raia kisha waziwasilishe katika baraza la madiwani, Mkurugenzi au mkuu wa Wilaya.

Pia wabunge wanatakiwa kufanya mikutano na raia wa majimbo yao na kuzichukua kero zao, wao ndio wawasiliane na Mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, polisi, uhamiaji, wakuu wa mashirika kama TARURA, TANROAD, TANAPA, DAWASCO n.k. Tuzingatie utaasisi na mifumo ilu kujenga nchi bora.
 
Makonda hajateuliwa hao Wote ulowasema walikuepo kwenye Nafasi zao...!

Wamefanya nini hasa kutatua kero za Watanzania Masikini....!?

Mimi siiipendi CCM, Sikuwahi kukubaliana na Maghufuri kwa baadhi ya Misimamo yake!

Na hata sasa simkubari Makonda kwa Historia yake....!

Ila nakubaliana na kile anachokifanya, kuna changamoto nyingi sana huku chini hazitatuliki na Wabunge, Madiwani ama Wakuu wa Wilaya na Mikoa! Na nyingi ya chamgamoto hizo ni kwa sababu ya kutokujari tu Maisha
ya wengine!

Mimi naunga Mkono ufanyaji kazi wa Makonda....!

Mfano nilmebahatika kuona Mikutano miwili ya Makonda, mmoja alikua Mwanza, kuna Mtu akamuomba awasaidie waupate mwili wa ndugu yao marehemu, anayedaiwa 2 millions na wao hawana uwezo kulipa hiyo pesa!

Kwa hiyo kama hiyo Wafiwa wangeenda kwa Mkuu wa wilaya, mkuu wa wilaya angewaambia sijui wakamuone Mkurugenzi, Mkurugenzi angesema nendeni kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa angekua busy na Vikao week nzima...!

Lakini Makonda alichofanya ni kutoa Gari yake ikatoe mwili Hospital na kupeleka kuzika!

Hivyo ndo Wananchi tunataka, kuona shida zetu zinatatulika, na sio story za utawala Bora sijui Mihimili inaingiliana, haitusaidii....!

Kama kutuibia pesa za walipa kodi wanaiba kila siku na tumekosa namna ya kuwafanya!!! Basi raia wa kawaida wakipata chagamoto zinazohitaji utatuzi....! Natamani kuona zinatatuliwa kwa namna Makonda anafanya.

Alifanya Sokoine, alifanya Mrema, alifanya Lowassa, alifanya Maghufuri, sio kitu kipya akifanya Makonda mradi inawagusa wale Watanzania wa chini kabisa....!

Binafsi natamani hasa Waziri Mkuu ama Naibu wake wangekua kama Makonda...!
 
Unaijua kazi ya uenezi wa chama?

Unakumbuka Nape alikua akishiriki hadi ujenzi wa zahanati huko vijijini?
Nape kushiriki ujenzi wa zahanati vijijini ambazo tayari zimetengewa bajeti na serikali ni PR ya kisiasa inayowezwa kufanywa na mwanasiasa yoyote.
 
Ok vizuri unaonekana unaijua ccm...

Tutajie majukumu ya mwenezi wa ccm
 
Makonda hajateuliwa hao Wote ulowasema walikuepo kwenye Nafasi zao...!

Wamefanya nini hasa kutatua kero za Watanzania Masikini....!?

Mimi siiipendi CCM, Sikuwahi kukubaliana na Maghufuri kwa baadhi ya Misimamo yake!

Na hata sasa simkubari Makonda kwa Historia yake....!

Ila nakubaliana na kile anachokifanya, kuna changamoto nyingi sana huku chini hazitatuliki na Wabunge, Madiwani ama Wakuu wa Wilaya na Mikoa! Na nyingi ya chamgamoto hizo ni kwa sababu ya kutokujari tu Maisha
ya wengine!

Mimi naunga Mkono ufanyaji kazi wa Makonda....!

Mfano nilmebahatika kuona Mikutano miwili ya Makonda, mmoja alikua Mwanza, kuna Mtu akamuomba awasaidie waupate mwili wa ndugu yao marehemu, anayedaiwa 2 millions na wao hawana uwezo kulipa hiyo pesa!

Kwa hiyo kama hiyo Wafiwa wangeenda kwa Mkuu wa wilaya, mkuu wa wilaya angewaambia sijui wakamuone Mkurugenzi, Mkurugenzi angesema nendeni kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa angekua busy na Vikao week nzima...!

Lakini Makonda alichofanya ni kutoa Gari yake ikatoe mwili Hospital na kupeleka kuzika!

Hivyo ndo Wananchi tunataka, kuona shida zetu zinatatulika, na sio story za utawala Bora sijui Mihimili inaingiliana, haitusaidii....!

Kama kutuibia pesa za walipa kodi wanaiba kila siku na tumekosa namna ya kuwafanya!!! Basi raia wa kawaida wakipata chagamoto zinazohitaji utatuzi....! Natamani kuona zinatatuliwa kwa namna Makonda anafanya.

Alifanya Sokoine, alifanya Mrema, alifanya Lowassa, alifanya Maghufuri, sio kitu kipya akifanya Makonda mradi inawagusa wale Watanzania wa chini kabisa....!

Binafsi natamani hasa Waziri Mkuu ama Naibu wake wangekua kama Makonda...!
Kama huo ndio mtindo wa uongozi mnaoutaka na mnaoona una ufanisi sana basi hakuna haja ya kupoteza mabilioni ya pesa kufanya uchaguzi wa madiwani na wabunge ambao wanachaguliwa mahususi kutatua kero na kuleta maendeleo katika maeneo yao.
 
Nyie watu kuna kitu mnachanganya hapa bila kujua, haya majukumu ya Mwenezi na watendaji wengine serikalini yanaingiliana kwa kiasi kikubwa, ndio maana wengi mnapata tabu kumuona Makonda anakosea, kwangu hakosei yupo kazini.

Kazi ya Makonda ni kukitangaza chama chake, na anakitangaza kwa namna tofauti ikiwemo kufanya shughuli za kijamii, au kufuatilia utendaji kazi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na viongozi wa serikali ya chama chake.

Mpaka hapo, utaona Makonda anavyowaagiza mawaziri wafanye hili au lile, anafanya hivyo kwa manufaa ya chama chake, kwamba hao mawaziri wakizembea, lawama zitaangukia kwa chama chake, tena kwenye ofisi yake, yeye akiwa ndie mwenye jukumu la ufuatiliaji na utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyowaahidi wananchi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mfumo sahihi wa kusikiliza na kutatua kero za raia ni kupitia madiwani na wabunge, sio katibu mwenezi wa chama cha siasa.

Madiwani wanatakiwa wafanye mikutano ya kusikiliza kero za raia kisha waziwasilishe katika baraza la madiwani, Mkurugenzi au mkuu wa Wilaya.

Pia wabunge wanatakiwa kufanya mikutano na raia wa majimbo yao na kuzichukua kero zao, wao ndio wawasiliane na Mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, polisi, uhamiaji, wakuu wa mashirika kama TARURA, TANROAD, TANAPA, DAWASCO n.k. Tuzingatie utaasisi na mifumo ilu kujenga nchi bora.
Yes, madiwani wote wa sasa na Wabunge ni "zao la mwendazake", wapo wapo maana waliwekwa na Jiwe na hawana morali na mama.
 
Kama huo ndio mtindo wa uongozi mnaoutaka na mnaoona una ufanisi sana basi hakuna haja ya kupoteza mabilioni ya pesa kufanya uchaguzi wa madiwani na wabunge ambao wanachaguliwa mahususi kutatua kero na kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Mkuu mambo mengi wala sio Matakwa ya Wananchi Masikini, hayo yote yameletwa na Watu wachache!

Nikupe Mfano.

Kama mimi nimedhurumiwa Kiwanja changu na Mtu mwenye Pesa, na Documents zote ninazo, nimeenda Ardhi napigwa Danadana, nimeenda kwa Mkuu wa wilaya naambiwa njoo kesho njoo kesho, Diwani wangu kashindwa kunisaidia, nimeenda Mahakamani nikashindwa Kesi kisa tu Mtu aliyepora kiwanja changu ana pesa, na kahonga mpaka Mahakimu....!

Then naanza kupokea Vitisho kwamba ntapotezwa.... Kesho nasikia Makonda ana Mkutano mahari nilipo, najitokeza mbele yake kuwasirisha kero zangu nikiwa na Documents zangu....!

Wanaitwa Viongozi wa chama na serikali wanachosema tu Issue yangu wanaijua, wanaitwa Wanasheria na watu wa ardhi kukagua Documents zangu wanasema zipo sawa...!

Makonda anatoa Amri narejeshewa Kiwanja changu....!
Then ndo wewe uje uanze kusema taratibu hazikufuatwa, sijui Viongozi waliopo ngazi zote wana kazi gani kama Mtu mmoja tu atahodhi maamuzi yote...!

Mimi kama Mtanzania wa kawaida hilo halinihusu, ukiniambia kuhusu Mahakama ntakwambia haipo kwa ajiri ya Masikini, nnachoshukuru ni kwamba Nilinyang'anywa Kiwanja changu na mtu mwenye Pesa....! Na. Akaja mtu mwingine mwenye Madaraka karudisha Kiwanja changu!

Hivyo tu ndo sisi Masikini tunataka...!!
 
Makonda yeye atathibitishaje wewe umedhulimiwa kiwanja na sio kwamba wewe ndiye unayetaka kudhulumu au kung'ang'ania kiwanja kisicho chako?

Lazima nchi iongozwe kwa utawala wa sheria tena za haki na "due process".
 
Nyie watu kuna kitu mnachanganya hapa bila kujua, haya majukumu ya Mwenezi na watendaji wengine serikalini yanaingiliana kwa kiasi kikubwa, ndio maana wengi mnapata tabu kumuona Makonda anakosea, kwangu hakosei yupo kazini.

Kazi ya Makonda ni kukitangaza chama chake, na anakitangaza kwa namna tofauti ikiwemo kufanya shughuli za kijamii, au kufuatilia utendaji kazi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na viongozi wa serikali ya chama chake.

Mpaka hapo, utaona Makonda anavyowaagiza mawaziri wafanye hili au lile, anafanya hivyo kwa manufaa ya chama chake, kwamba hao mawaziri wakizembea, lawama zitaangukia kwa chama chake, tena kwenye ofisi yake, yeye akiwa ndie mwenye jukumu la ufuatiliaji na utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyowaahidi wananchi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kama anafanya kazi za madiwani na wabunge huoni kwamba anamaanisha wamepwaya na hawatimizi majukumu yao hivyo wanapaswa kuondolewa ?
 
Mkuu mambo mengi wala sio Matakwa ya Wananchi Masikini, hayo yote yameletwa na Watu wachache!

Nikupe Mfano.

Kama mimi nimedhurumiwa Kiwanja changu na Mtu mwenye Pesa, na Documents zote ninazo, nimeenda Ardhi napigwa Danadana, nimeenda kwa Mkuu wa wilaya naambiwa njoo kesho njoo kesho, Diwani wangu kashindwa kunisaidia, nimeenda Mahakamani nikashindwa Kesi kisa tu Mtu aliyepora kiwanja changu ana pesa, na kahonga mpaka Mahakimu....!

Then naanza kupokea Vitisho kwamba ntapotezwa.... Kesho nasikia Makonda ana Mkutano mahari nilipo, najitokeza mbele yake kuwasirisha kero zangu nikiwa na Documents zangu....!

Wanaitwa Viongozi wa chama na serikali wanachosema tu Issue yangu wanaijua, wanaitwa Wanasheria na watu wa ardhi kukagua Documents zangu wanasema zipo sawa...!

Makonda anatoa Amri narejeshewa Kiwanja changu....!
Then ndo wewe uje uanze kusema taratibu hazikufuatwa, sijui Viongozi waliopo ngazi zote wana kazi gani kama Mtu mmoja tu atahodhi maamuzi yote...!

Mimi kama Mtanzania wa kawaida hilo halinihusu, ukiniambia kuhusu Mahakama ntakwambia haipo kwa ajiri ya Masikini, nnachoshukuru ni kwamba Nilinyang'anywa Kiwanja changu na mtu mwenye Pesa....! Na. Akaja mtu mwingine mwenye Madaraka karudisha Kiwanja changu!

Hivyo tu ndo sisi Masikini tunataka...!!
Upo sahihi
 
Kama huo ndio mtindo wa uongozi mnaoutaka na mnaoona una ufanisi sana basi hakuna haja ya kupoteza mabilioni ya pesa kufanya uchaguzi wa madiwani na wabunge ambao wanachaguliwa mahususi kutatua kero na kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Hao Madiwani wako wamewafanyia nini wananchi zaidi ya kuwafanyia majungu wafanyakazi wa Halmashauri zao, je huoni kwenye TV wakitetea matumbo yao kimtindo? Kama na wewe ni diwani jifunze kupitia kwa Makondo sio kutetea
 
Kama mwenezi wa chama anafanya kazi za madiwani na wabunge huoni kwamba anamaanisha wamepwaya na hawatimizi majukumu yao hivyo wanapaswa kuondolewa?
 
Kama anafanya kazi za madiwani na wabunge huoni kwamba anamaanisha wamepwaya na hawatimizi majukumu yao hivyo wanapaswa kuondolewa ?
Huyu anawasukuma madiwani, wabunge na mawaziri wa chama chake kutekeleza yale yanayowahusu wananchi, waliyowaahidi wananchi ili kukiondolea lawama chama chake.

Suala la kupwaya ili kuondolewa ni issue nyingine separate, na ndio maana Makonda anajaribu ku avoid hiyo kwa kuwakumbusha hao watendaji majukumu yao, kumbuka kwa upinzani kushinda popote, maana yake Makonda na chama chake wamefeli.

Back
Top Bottom