Nguvu Iliyopo ndani ya mtu

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,381
1,414
Kila mwanadamu ana nguvu ndani yake na anaweza kuitumia akafanya mambo makubwa na ya ajabu na ya kushangaza na ya kustaajabisha. Nguvu tulizopewa ni kubwa mno, kuna mambo unaweza dhani hayawezekani lakini ukweli ni kwamba ukiamua, wewe mwenyewe utaweza kuyafanya bila ya hata kusaidiwa na mtu.

Basi Leo nakuletea mambo kama matano tu hivi yanatosha japo yapo mengi, mambo ambayo unahisi kwamba huna nguvu ya kuyatenda na kila jambo nitakalolitaja nitakupa na mifano ya watu waliofanya hivyo na wakaweza. Vilevile kwa ushahidi zaidi, hapo chini nimeweka video ya watu hao waliofanya mambo haya matano live tena hadharani ili iwe ushahidi msiseme nadanganya.

1. KUKATA KICHWA NA KUTEMBEA NACHO UKIWA UMEKISHIKA MKONONI.

Hii imekaaje? Inawezekana, hata wewe unaweza ukakata kichwa na kutembea nacho njiani. Angalizo lazima uwe umekwisha kutambua nguvu uliyonayo inakuwezesha kufanya hivyo au utumie magic vinginevyo utakufa. Nadhani wengi tunafahamu magic imenzia wapi, hilo silizungumzii leo. Hili limefanywa na jamaa mmoja anaitwa Julien na ameweza yupo anaishi duniani mpaka sasa.

2. KUTEMBEA KWA MIGUU MITATU.

Hata wewe na mimi pamoja na kuwa na miguu miwili unaweza ukaamua uwe na miguu mitatu na utembee nayo. Julien pia aliweza hili. Ukitaka kuamini, wakati anatembea huku ameshika kichwa chake mkononi alikuwa na miguu miwili. Lakini cha ajabu anajitokeza tena hadharani akitembea na miguu mitatu.

3. KUBEND KWA NYUMA KAMA UMELALA.

Hapa sijui nielezeeje vizuri ieleweke yaani ufanye kama unalala flat kwa nyuma, sio chini, ila mguu mmoja tu ndo utakanyaga chini. Hii ilifanywa na jamaa mmoja anaitwa Dynamo.

4. KUTEMBEA JUU YA MAJI.

Hii tulishaona mtu wa kwanza Yesu akitembea juu ya maji. Pia Dynamo alifanya hii pia akashangaza umati wa watu, alikuja kutolewa na ma askari kwa sababu alisababisha watu wasiendelee na shughuli zao za kiuchumi wakabaki wakimshangaa yeye. Je unaamini na wewe unaweza hilo?

5. KUPAA HEWANI.

Pamoja na hayo tuliyoaona, pia unapaswa utambue pia unauwezo wa kupaa ila lazima utumie magic. Dynamo pia alifanya hili na akaweza, hata wewe unaweza.

Wanasema ni asilimia chache sana ya nguvu zetu ndizo tunazozitumia. Zaidi ya asilimia tisini hatuzitumii. Ikiwa tutatumia asilimia 100 ya nguvu tutafanya mambo makubwa na ya kustaajabisha sana. Baadhi ya scientist ambao tunawaterm kama magenius, utofauti ni kwamba wametumia asilimia nyingi kiasi ya nguvu zao na uwezo wao wa kufikiri.

Binafsi mimi nimepractice naweza kumwita mtu aliye mbali pasipo kutoa sauti kubwa au pasipo kutoa sauti kabisa na mtu yule akanifuata kuniuliza kama nimemwita au kama yupo mbali zaidi akanipigia simu na nikamweleza nililotaka kumwambia.

View attachment:


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mental hospital gani iyo ime wai ivi kutoa graduates ..

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
Dah! Ngoja niendelee kutafuta hela ili nami nitengeneze kirusi kingine mwaka 2022
Nalog off
 
...Umejaribu kutumia neno LA kiingereza ili kujaribu kutia Uzito Mada yako LA Magic...ambalo linamaanisha Uchawi tu!
Na kwa bahati mbaya umeeleza tu matukio unayodao kutokea na Reference yako no YouTube tu!!...bahati mbaya hakuna popote ulipotoa maelezo ya jinsi ya kuyatenda yote hayo!...na bado Mkuu unaona umetoa Boonge LA Uzi. !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom