Tafsiri sahihi ya nguvu ni kumpandisha MTU na sio kumshusha MTU

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,058
45,660
Lengo la sisi kuwa na nguvu za kimamlaka sio ili tuwashushe watu bali tuwapandishe watu.

Kama walivyo ndege Angani wanavyoweza kupaa bila kugongana , Hivyo hivyo ndivyo zilivyo hatua za Maisha unaweza fanikiwa pasipo kumuumiza MTU yoyote.

Ikiwa umeridhika na MAISHA yako basi unaweza endelea kudharau sauti zinazokulalamikia na kuumia juu yako .

Binadamu huwa anahitaji watu wengi ili kufanikiwa zaidi na kupanda Juu ila pia Binadamu huwa anashushwa na Mtu mmoja na kubaki pale pale.

Isikilize sana sauti yako ya ndani uone inakuambia nini ikiwa haipo na wewe basi jitafakari maana sio ulinzi utakaokufanya kubaki salama tena wala nyumba ilyofungwa na mageti makali.

Tafuta sana Mafunuo

Nakutakia Mema sana ndo maana nimekupa UKUMBUSHO katika hii safari yako ya MAISHA sipendi kukuona unarudi nyuma
 
Back
Top Bottom