Ngurumo: Mahakama na kikwete, nani mpuuzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngurumo: Mahakama na kikwete, nani mpuuzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, May 17, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  "....................Takrima iliasisiwa na serikali ya Mkapa. Baadhi ya wenzetu wakadhani JK aliye ‘chaguo la Mungu’ hataweza kuivumilia; ataifuta. Mahakama Kuu ilipoifuta, mashabiki wake wakaeneza propaganda kwamba, “imefutwa kwa amri na matakwa ya JK.” Miaka minne baadaye, sasa JK mwenyewe ametangaza urafiki na takrima.

  Pale pale, akavunja sheria yake mwenyewe; na akaenda mbali zaidi kupinga uamuzi wa mahakama kuu – akatetea takrima.
  Kitendawili ni hiki: mahakama imelaani takrima. Rais anasifia takrima. Ni nani mpuuzi kati ya hawa wawili?..............................."

  Ngurumo
  Tanzania Daima16/05/2010
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,602
  Likes Received: 4,715
  Trophy Points: 280
  Mtoto hata akiwa jeuri kiasi gani hawezi kumtukana baba yake. Kikwete ni zao la takrima hivyo hawezi kuilaani lazima ataipamba tu. Fedha ya epa iliyochotwa na kampuni zimwi ya kagoda ndiyo ilitumika kumuuza jk kwa wapiga kura mwaka 2005, hivyo jk akiwa na akili timamu ni lazima asifu takrima. Na ndiyo maana sasa wanatafuta bilioni 50 za kutoa takrma ndiyo maana ana andaa mazingira ya kutoa rushwa wakati wa uchaguzi baadae mwaka huu.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani muungwana wetu, pamoja na huo uungwana na rekodi yake ya miaka mi5 hawezi kurudi Ikulu hadi kwa njia ya hongo tena?
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tunayakuza tu haya kwa uandishi wetu hafifu na uwezo mdogo wa kufikiri na kuchambua mambo hasa hotuba za JK. Najiuliza mara nyingi kwa nini hotuba za Rais wetu zinapindishwa mara kwa mara. Hii ni kwa manufaa na madhumuni gani hasa?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Broda! gimme a break!!!!! Do you want to tell me tht JK do present such philosophical speeches ambazo zinahitaji uwezo mkubwa wa kuchambua ili kuzielewa? Yaani kama ile hotuba ya juzi ya TUCTA imekuzwa?
  Mapenzi gani haya????
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,654
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  Mkuu hotuba zake hazipindishwi, tatizo kubwa ni yeye mwenyewe. Huwa hajui wapi pa kuweka masihara na wapi pakuonyesha anayezungumza ni Rais. Kauli ni za hovyo hovyo tuu.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Imekuzwa mno. Imepata tafsiri nyingi kama mistari iliyomo kwenye Biblia au Quran. Kwa nini inakuwa hivi?
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Labda mnataka ahutubie kama Makamu wa Rais, Dr AM Shain? Mnamchukia mno Rais wetu sote.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hotuba za hovyohovyo zinajadiliwa hovyohovyo hakuna kosa. Mbona za kambarage hazijajadiliwa hovyohovyo hadi leo.abadilike la sivyo tunae.
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,654
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  Uko wrong mkuu,hakuna anayeweza kumchukia Rais wa nchi yake kama atakuwa anafanya yale aliyopaswa kufanya wakati anaomba hiyo kazi. Tunaipenda zaidi nchi yetu, na yeyote anayeitendea nchi hii mambo ya hovyo hovyo anaitafuta chuki ya wazalendo wa Tanzania.
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Nani anapindisha Hotuba?
  Muwasilishaji (Kikwete) ama wanaomnukuu neno kwa neno?
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Haswaaa!
  Hovyo kweli kweli!
  Wildcard, ungekuwa umesikiliza hotuba aliyoitoa Mei 3 akiwajibu wafanyakazi wa Tanzania, au mwaka juzi alipokuwa anaisagia filamu ya Sauper ya Darwin's Nightmare (mapanki) ndipo ungejua kwamba hatuna raisi makini.
  Hovyo kabisa!
   
Loading...