Nguo yake imeniponza

Nguo yake imeniponza

Jifanye unaumia zaidi yake kama yeye kalala ndani wewe kubali kung'atwa na mbu ukakae nje...halafu kama unaweza tuma message ya machungu kwa mama, dada au kaka ako kwamba unataka kufa kisa umemkosea mchumba wako halafu jifanye umekosea namba itume kwake. ila usisahau kuweka jina la huyo unayemtumia ili akisoma ajue kwamba si yake lakn kuna nduguyo anayestahili kutumiwa, atakuongelesha tu...I ONCE USED AND IT WORKED SO PERFECTLY...kama hujaelewa niambie nikupe mbinu zaidi!

duh..kweli we ni proffessional cheater#kudos to tht#....i can't buy tht lie though,ingekuwa ni mimi.
 
Nipe matokeo??
kajibu tu sms, kasema hii ni nakala baada ya kutuma kwa dada yako au unanijulisha unataka kutuma hiyo sms ya namna hiyo kwa wifi!
Kama ni nakala sitajibu chochote kama unahitaji ushauri kabla ya kutuma basi sikushauri utume na wanaojiua kwa taarifa yako huwa hawasemi unakuta tu mwili na maandishi!
 
Jifanye unaumia zaidi yake kama yeye kalala ndani wewe kubali kung'atwa na mbu ukakae nje...halafu kama unaweza tuma message ya machungu kwa mama, dada au kaka ako kwamba unataka kufa kisa umemkosea mchumba wako halafu jifanye umekosea namba itume kwake. ila usisahau kuweka jina la huyo unayemtumia ili akisoma ajue kwamba si yake lakn kuna nduguyo anayestahili kutumiwa, atakuongelesha tu...I ONCE USED AND IT WORKED SO PERFECTLY...kama hujaelewa niambie nikupe mbinu zaidi!

I love JF. period
 
kajibu tu sms, kasema hii ni nakala baada ya kutuma kwa dada yako au unanijulisha unataka kutuma hiyo sms ya namna hiyo kwa wifi!
Kama ni nakala sitajibu chochote kama unahitaji ushauri kabla ya kutuma basi sikushauri utume na wanaojiua kwa taarifa yako huwa hawasemi unakuta tu mwili na maandishi!

ushauri Wa kibavu umegonga mwamba? basi mchumba wako mbishi kiasili.
 
Last edited by a moderator:
Utakuwa mchafu sana wewe, ina maana usafi chini ya uvungu kwako ni mwiko.

Ungekuwa na kawaida ya usafi wa jumla wa chumba ungelikua ushaona hayo.

Otherwise the whole thing ni fiksi kuchangamsha kadamnasi.
Sina kawaida ya kufanya usafi either ni wa nguo au ndani, isipokuwa wa mwili na nguo zangu za ndani! yupo mtu kwa kazi hiyo hadi napokuwa na msichana chumbani huwa haingii mtu!
wezi wote hujihisi kuibiwa muda wote so siwezi kushangaa kwa nini unaamini nimetunga!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna binti niliwahi kuwa naye sasa kumbe aliacha kipichu chake chini ya godoro la kitanda changu, leo nilitoka nimerudi mchumba kanuna mpaka basi, nauliza tatizo nini? naonyeshwa pichu ya e-x, mchumba kalia mpaka basi haelewi hili wala lile mbaya zaidi sikuwahi mwambia nilikuwa na mtu kabla yake!
Mpaka naandika ujumbe huu kalala kwenye kochi chumbani jamani nifanyeje? na nyinyi bi-dada zetu unaachaje nguo tena ya ndani kwa mvulana wako bila taarifa? kichwa kinauma nahisi kupoteza mtu nilie msotea miaka mingi jamani duh!!!!!!!
ushauri wako jamani mtoto ana hasira hata sielewi nafanyaje ananiona si mwaminifu kabisa!

Utakuwa mchafu sana wewe, ina maana usafi chini ya uvungu kwako ni mwiko.

Ungekuwa na kawaida ya usafi wa jumla wa chumba ungelikua ushaona hayo.

Otherwise the whole thing ni fiksi kuchangamsha kadamnasi.

najaribu kuhusianisha nipate logic kwanza na hii thread
Sms iliyoniumiza kupita zote

Kupigwa kibuti nilisha wahi pigwa na ninayempenda zaidi kwa kunitumia sms fanya mambo yako, mimi na wewe basi! sikupata kuumia kama hii sms ya mpenzi wangu wa sasa ambayo si ya kunipiga kibuti!
sms yenyewe ni hii:
Sema July! pole kwa uchovu wa jana! mwaka unaisha sasa tunaanza mwaka mpya muda si mrefu kama tukibahatika, ila kuna mambo manne ulinifanyia mwaka huu yalinikera sana japo sikusema ningependa kuona hayajirudii mwakani kama tutabahatika kuuona!
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
Ndugu zangu wana jamvi sikupata kujua alikuwa anakereka moyoni hata kidogo kwa lolote maana alionekana mwenye furaha muda wote, na siku tunatembea kwa muguu nilijua namsaidia kufanya zoezi maana fedha sio siri ilikuwepo si tu kupanda dala dala bali hata kukodi tax! lakini hakupata kusema mpaka jana alipo nitumia hiyo sms niliumia sana kila muda nawaza juu ya sms hii na hakuna aliloongopa yote ni kweli! hata jibu hapa sina najibuje sasa?
hapo kwenye kijani UKIHUSIANISHA kuna walakini mkuu..
 
Jaribu kumuhakikishia kuwa hiyo ilikuwa ni ya ex kwa kushika bible na kusema ukweli na kwamba kama una danganya basi baya likufike.

Ila inaonyesha kama huwa unaishi nao ingali hujaoa bado!!!!
Nilichofanya mimi tumelala sote kwenye kochi, mwanzo alinihama nikamfuata akahama tena nami nikamfuta mwisho wa siku nikawa naongea ananiangalia nilimweleza ukweli akanitaka nimupigie e-x nikawa namba sina ila nikampigia rafiki yangu anayo akanipa tukaweka loud akapigiwa naye inaonesha alikuwa na mchizi usiku akarusha hanifahamu labda nimekosea namba! nikatuma sms akajibu usitume sms niko na mme wangu tulisha achana kwa nini kuharibiana july? basi nitafute kesho nakuomba jul usipige simu wala kutuma sms! japo mimi najua hajaolewa ila angalau majibu yake yalimufanya mrembo wangu kunisikiliza ila kasema nisiende job wala yeye haendi job leo anataka baadae apigiwe e-x athibitishe kama kweli chupi ni yake akisema ni yake ajue kwa nini aliiacha akishajua hayo basi ndio atachukua maamzi anayoona yanafaa ila sote tumelala kwenye kochi! no game wa kuvua nguo duh! japo usiku sana mpaka asubuhi nilikumbatiwa! na kanisalimia ila sasa kalala kitandani sihitaji kumsumbua ili ahsubuhi tumpigie e-x!
 
Utakuwa mchafu sana wewe, ina maana usafi chini ya uvungu kwako ni mwiko.

Ungekuwa na kawaida ya usafi wa jumla wa chumba ungelikua ushaona hayo.

Otherwise the whole thing ni fiksi kuchangamsha kadamnasi.

Umeniwahi mkuu nilikuwa nawaza mtu kama huyu atakuwa mchafu kupindukia. Hiyo pichu na mauchafu yake imeachwa katikati ya godoro kwa siku zote hizo hadi mdada akaja kuikuta; huyu jamaa hata kuswaki atakuwa anasahau.
 
Kwani ile dawa yako imemsaidia yule aliyekua anaharisha baada ya kutumia asali?
 
Jaribu kumuhakikishia kuwa hiyo ilikuwa ni ya ex kwa kushika bible na kusema ukweli na kwamba kama una danganya basi baya likufike.

Ila inaonyesha kama huwa unaishi nao ingali hujaoa bado!!!!

Mkuu bible haisaidii... Kuna watu wana ujasiri wa kifisadi, unamshikisha bible na bado anaapa uongo!!!
 
najaribu kuhusianisha nipate logic kwanza na hii thread
Sms iliyoniumiza kupita zote


hapo kwenye kijani UKIHUSIANISHA kuna walakini mkuu..
unajitahidi lakini mwisho wasiku utagundua hakuna sehemu niliwahi kumwambia nilikuwa na mtu kabla yake nje na hapo utaishia kusikia yeye anasema alipata taarifa je unajua nilikanusha au nilikubali? pia unajuaje kama ndio huyu namuita e-x? any way sitaki kubishana sana ila ukichulia event ni ya kweli toa mchango wako ukiona ni fix basi soma then piga chini kwani kuna ulazima wa kujibu ukisha soma!
 
unajitahidi lakini mwisho wasiku utagundua hakuna sehemu niliwahi kumwambia nilikuwa na mtu kabla yake nje na hapo utaishia kusikia yeye anasema alipata taarifa je unajua nilikanusha au nilikubali? Pia unajuaje kama ndio huyu namuita e-x? Any way sitaki kubishana sana ila ukichulia event ni ya kweli toa mchango wako ukiona ni fix basi soma then piga chini kwani kuna ulazima wa kujibu ukisha soma!

nikueleweshana tu mkuu..usiwe na hasira..nachotaka kuelewa ni huyo uliyemsotea miaka mingi na huyu ambayr hadi mwaka huulikuwa nae..refer tene kwenye bold ya kijani post yangu ya kwanza..
Lengo si kutokukuamini..bali kujiridhisha kwanza
 
wezi wote hujihisi kuibiwa muda wote so siwezi kushangaa kwa nini unaamini nimetunga!!!!!!!!!!!!!!

Visa vyako na sredi zako za nyuma zinanipa kila sababu ya kutokuiamini hii habari mkuu...

Wakati mwingine tunashindwa kutoa msaada wa mawazo kwa kuwa hatujui nani mkweli na nani mchangamsha kijiwe...
 
Kwani ile dawa yako imemsaidia yule aliyekua anaharisha baada ya kutumia asali?
kapona na alileta mrejesho hapa MMU! na si huyo tu watu wa PM ni zaidi ya uwezo wangu kuwapa majibu na maanisha ni wengi mno hata yule alianzia kule PM baada ya kuharisha ndio akaja huku! sasa hilo swali na hii topic kaka vinahusianaje?
 
nikueleweshana tu mkuu..usiwe na hasira..nachotaka kuelewa ni huyo uliyemsotea miaka mingi na huyu ambayr hadi mwaka huulikuwa nae..refer tene kwenye bold ya kijani post yangu ya kwanza..
Lengo si kutokukuamini..bali kujiridhisha kwanza
Rejea thread ilikuwa ya lini? alafu utagundua maneno mwaka unaisha sasa july yalimanisha mwaka wa mahusiano au mwaka 2013? soma kwa umakini bila papara utaprove failure mwisho wa siku kwani mimi najua uongo huwa unajitenga na ukweli! narudia sina hasira ila hii ni true story upo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom