Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imetangaza kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Wananchi (CUF) wa Desemba 2024 ni batili na kuelekeza chama hicho kurudia uchaguzi wa nafasi za juu za uongozi mara moja.
Hoja ya awali hii hapa ~ Msajili amtaka Profesa Lipumba na wenzake warudie uchaguzi CUF
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Uhusiano wa CUF, Mohamed Ngulangwa amekiri chama hicho kupata barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
"Ni kweli Baraza Kuu lilibadilisha kanuni zinazotaka viongozi wa juu wapatikane kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura.
"Hiyo ni kwa sababu kulikuwa na wagombea wengi na uchaguzi ulikuwa na ushindani mkali. Kwa mfano nafasi ya uenyekiti ilikuwa na wagombea tisa, sasa ukiwachuja wabaki watatu, ingezua malalamiko.
"Hivyo tukawaacha waingie wote kwa kubadili kanuni. Sasa ukishaondoa hilo sharti maana yake hakuna atakayepata asilimia 50 ya kura, itakuwa simple majority," amesema.
Amesema licha ya wagombea kukubali mabadiliko hayo, lakini baadaye walienda kulalamika kwa msajili.
"Utaratibu wa kubadilisha kanuni kwenye chama chetu ni wa kawaida na umekuwa ukituvusha. Hata CCM umeona kwenye chaguzi zao, walibadilisha kanuni za uchaguzi wa ndani wakaruhusu wagombea wote wapigiwe kura," amesema.
Ngulangwa amehusisha agizo la Msajili na kauli za mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye hivi karibuni amekuwa akiikosoa serikali majukwaani.
"Kwa sababu uchaguzi wetu ulifanyika Desemba 2024, Msajili alikuwa na nafasi ya kutosha kusikiliza malalamiko na kutoa uamuzi, lakini leo ndio anakuja na maamuzi yake.
"Inawezekana kauli za mwenyekiti (Profesa Lipumba) zinahusika, kwa sababu sisi tulikiwa wa kwanza kutoa tamko kwamba hatuutambui uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025.
Huo ni msimamo wa vyama mbalimbali na hata jumuiya ya kimataifa imesema hakukuwa na uchaguzi.
"Hata Januari 27 tumefanya kumbukumbu ya mauaji ya 2001, mwenyekiti akakosoa uchaguzi ule na alisema tunataka Serikali ya mpito kabla ya maridhiano.
"Kwa hiyo inawezekana kauli hizo zimesababisha," amesema Ngulangwa.