Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Deal done..!
Mark my words!
Hizi za sasa ni purukushani za muda tu na kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji..!
Ngorongoro is no longer ours..and maybe be it will never be ours again ..! Nani anakumbuka ya Loliondo? Pamoja na kelele zote zile haikuwahi kurudi kwetu...!

Siku ile pm alipoenda Arusha na ile list ndefu ya Wamasai waliokubali kuhamia ugenini huko Handeni Tanga... Ndio ilikuwa hitimisho la kuiaga Ngorongoro..

Ule mkutano
Zile picha
Yale majina
Zile video
Vyote vimechukuliwa na kuhifadhiwa vizuri kwamba kila kitu kilifanyika kwa kuzingatia haki za binadamu, matakwa ya kisheria nknk..

Hawa waliopelekewa moto leo wanahesabika kama wavamizi na ndio maana jeshi la polisi lilienda kule.. Na trust me kile kilichifanyika asubuhi ya leo ni salam tuu.. Ile ni kifungua kinywa tuu.. Full menu ya bufee itawaendea usiku kukiwa kuna kiza kinene. Hapo ndio shetani atasimamia ukucha...

Kesho yaweza kuwa siku ya kuokota mizoga, majeruhi vituo vya afya, watuhumiwa kwenye selo za polisi, na matukio ya watu kupotea huko Ngorongoro national park.

Kwa wiki chache zijazo safisha safisha itaendelea kuondoa masalia yote ya kitu kinachoitwa Wamasai wa Ngorongoro wavamizi.. Tutawekwa busy na unit za umeme kupaa, kesi za sabaya na drama zingine zote..!

Itakapofika 30/6 ndio itakuwa mwisho wa kuiona Ngorongoro uliyozoea kuiona japo kwa picha tangu ukiwa mdogo.. Kama una picha zake ama ulibahatika kufika kule na kupata kumbukumbu kadhaa..ZIHIFADHI VEMA..Hiyo bahati haipo tena!

Hakuna picha zake zitapatikana tena huko kwa uhuru na kujiachia, hakuna selfies tena za mbuga yetu ile urithi wetu...picha zitapigwa na watu maalum..! Na kwa sababu maalum...!

Na wazawa watakaoruhusiwa kuingia kule ama ni mamluki ama ni wafanyakazi wasio huru,.. Itakuwa ni kama watumwa katika nchi yao wenyewe!

Tusitaharuki zaidi, tusilie, bali tuanue tanga.. Msiba ulishaisha kwasasa tusubiri kusomwa historia ya marehemu.. Tukipata wasaa tutawasimulia wana wetu picnic, na study tour za kishule wakati pale pakiwa kwetu..
 
IMG-20220610-WA0535.jpg
 
Inaumiza sana, nchi hii hakuna mzalendo na hamna mwenye hari ya kuipenda nchi yake ,kila mtu anavuta kwa urefu wa kamba ndomana jpm alisema historia ya tanzania lazima ifundishwe.ndomana kuna makundi ya waasi wanaibukaga. walaniwe wao na vizazi vyao washenzi waliofanya hili, na dhambi hii ya dhuruma isiache koo zao.
 
Kila kitu kitaenda mrama, kila jiwe litabinuliwa ili kuhakikisha wale waliojimilikisha hii nchi na familia zao na vizazi vyao vyote wanaishi kama wako peponi...enzi za utumwa bado zipo sema tu zinaendelea kwa akili na umakini mkubwa sana kiasi kwamba watumwa nao wanajiona ni sehemu ya watawala na kwamba wanaweza kuamua nani awe kiongozi wao lakini kumbe walaaa hawana Chao hata punje ila wameaminishwa hivyo ili watawaliwe kirahisi.
 
Back
Top Bottom