Ngome ya CHADEMA yasambaratishwa: Yashindwa katika Kata 7 kati ya 20 jijini Arusha hata kabla ya Uchaguzi

Hicho ndicho kinachonishangaza sana. Watu mtasema kuwa CCM inawafanyia fitina, je hata la makatibu wenu kushindwa kujaza vyema fomu ni kosa la CCM? Ama mnataka kutuambia tena kuwa wamehongwa? Kwa hiyo nyie kumbe mnahongeka? Sasa kama mnahongeka, nini tofauti yenu na CCM?

Nimetoka muda mdupi kukuambia ww ni mpuuzi na ni mtu unayesubiri habari jf na kuanza kupiga propaganda za kizee.

Nikuambie kinachoendelea huku sehemu zenye chaguzi za marudio hakuna form inayokosewa kwani kila mtu anajua kusoma na kundika, na kama ni kukosea hata wagombea wa vyama vingine wanaweza kukosea. Wakurugenzi kwa nafasi zao wanakubali kwa shingo upande kushiriki uovu kwa shinikizo toka mamlaka za juu kusema fomu zimekosewa na hakuna mwandishi anayeruhusiwa kuripoti au kudhibitisha kosa hilo, na baada ya hapo polisi wanaanza kupiga wananchi wanaotaka kufahamu kulikoni na mgombea wa chama cha upinzani hasa cdm anapew kipigo cha mbwa mwizi ili kuhakikisha hapati haki yake.

Jambo hili la hujuma za wazi liko kimkakati nchi nzima na lengo ni kuhakikisha wagombea wa ccm wanapita bila kupingwa ili kuhadaa uma na kuepusha aibu nyingine ya kushindwa ccm, au kutumika nguvu kubwa kupindua matokea kwani hilo huchangia udhalimu huo kufahamika kuliko kumzuia mgombea wa upinzani kwa sababu za uongo na ccm kutangazwa kupita bila kupingwa.

Ni hivi ww mpiga propaganda mzee, uovu ni jambo lenye nguvu sana, lakini jambo la hatari kwani wanadamu kwa asili hawajawahi kukaa kwa amani muda mrefu kwa ushirikiano wa uovu. Kuna watu wengi bila kujali itikadi wanashuhudia uovu huu ukishika kasi na miongoni mwao ni viongozi wa dini, wasomi na raia wa kawaida, si muda mrefu umma utaondoa itikadi za kisiasa na kuchukua hatua dhidi ya uovu huu wa kutoheshimu box la kura kwani kufumbia macho uovu ni kifo chetu wote. Kumbuka hata wazungu wa Africa kusini walileta maendeleo ya kweli lakini umma wa walio wengi waligoma udhalimu ulio kuwepo.
 
Na hapo ndipo mbaodhani mnajitambua mnapokosea. Wakati Lowassa hajaenda Upinzani, CCM ilitawala maeneo yote ikiwemo ngome ya CHADEMA lakini baada ya kuingia mwaka 2015, CHADEMA iliongoza karibia Halmashauri zote za Arusha na zaidi ya nusu za Upinzani. Je, Lowassa angeteuliwa CCM, Je nyie mnaojitambua mngepata hizo kura za Kaskazini?
Kama mbajitambua, hauoni shida kuwa, mkiingia madarakani, mtaua nchi maana Upinzani (CCM) utabaki na wasiojitambua?
Hahaaaaa funny comment.
 
mwenye akili timamu ashangai kamwe. kwa sasa hakuna uchaguzi kamwe. polis,tume ya uchaguzi na vyombo vya dola wanatumia nguvu kuzuia wagombea wa upinzani wasishiriki uchaguzi. kwa tume hii ccm inaweza shinda kote nchini.
 
Uchaguzi ama varangati...awamu hii hatujawahi kufanya uchaguzi chief...aibu.
 
Tuombee iwe hivyo, otherwise itabakia doa kubwa sana kwa legitimacy ya CHADEMA huyo kunakodaiwa Ngome yao come 2020.
DED msimamzi wa uchaguzi wameisha ambiw ana Rais anaye wateua kuwa wakitangaza matokeo CCM KASHINDWA basi hawana kazi,TUME ya uchaguzi wa TANZANIA is stinking!Hamna tume Tanzania bali ni kigenge la wahalifu wanaofanya kazi kwa kufuata amri ya Rais anaye wateua na ambaye ana nguvu ya kuwafukuza kazi muda wowote akitaka!
CCM haiwezi shinda kiti chochote Arusha ktk uchaguzi huru na wa haki
 
Sasa Hivi, hatuongelei tena Kata 7 tena, jumla ya Kata 20 kati ya 77 zimeshachukuliwa na CCM.
IMG_5151.JPG
 
Back
Top Bottom