Ng'ombe mmoja kuongezeka Kilo 2 na nusu kwa siku | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ng'ombe mmoja kuongezeka Kilo 2 na nusu kwa siku

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Apolinary, Apr 13, 2012.

 1. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,704
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Habari wana jf nakuombeni kujua zaidi ni wapi hizo lishe za ng,ombe mmoja kuongezeka kilo 2 na nusu kwa siku zinapatikana wapi katika mikoa ya Arusha na Moshi Natanguliza shukran
   
 2. Samcezar

  Samcezar JF-Expert Member

  #21
  Jul 12, 2018
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 2,144
  Likes Received: 1,589
  Trophy Points: 280
  Ng,ombe

  Ng'ombe

  Hivi walimu wa kusoma na kuandika huku shule za msingi hawapo siku hizi?!

  Maana kuna watu kanuni za uandishi ni sifuri kabisa....shuwain makatan kabisa
   
 3. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #22
  Jul 13, 2018
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,547
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Ningepata hiyo program inagenifaa sana ...embu MTU aiweke anitag
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #23
  Jul 14, 2018 at 10:45 AM
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,880
  Likes Received: 4,422
  Trophy Points: 280
  Hakuna program ya hivyo
   
 5. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #24
  Jul 15, 2018 at 10:10 PM
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,992
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya kuotesha mazao bora yenye tija kwa muda mfupi zaidi bila kutumia udongo kabisa, kwa kutumia maji na virutubisho (Hydroponic Nutrients).

  Hydroponic fodder Ni nzuri zaidi kwa sasa maana Ni nafuu kulinganisha na vyakula vingine vya mifugo.

  Hydroponic fodder Ni uoteshaji wa mbegu pasipo kutumia udongo kwa muda wa siku 5- 7 tu kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au shayiri au Mshindi zinaoteshwa na kumwagiliwa virutubisho maalum (HYDROPONIC NUTRIENTS) na kuongezeka kutoka kilo moja hadi kilo 10 za CHAKULA cha kuku.

  Kwakuwa kuku mmoja hula gram kati ya 100-120gm hivyo kilo moja ya mbegu ikitoa kilo kumi za fodder zinatosha kulisha kuku wakubwa 100 kwa siku Hydroponic fodder Ni CHAKULA cha Mifugo wa aina zote chenye faida nyingi sana.

  FAIDA ZA CHAKULA CHA HUDROPONIC FODDER KWA MIFUGO

  1. Ni nafuu sana kulinganisha na garama za CHAKULA cha madukani au viwandani
  2. kina virutubisho na vitamini mara 3 zaidi ya CHAKULA cha kawaida cha Mifugo
  3. Hupunguza magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile mafua kwa mfugaji na Mifugo kwani hakina vumbi kabisa.
  4. kina protein na Energy/nishati nyingi zaidi mara 3 ya inayopatikana kwenye vyakula vya kawaida vya Mifugo kama kuku.
  5. mifugo hukua haraka sana kutokana na wingi wa protein ambayo hufanya Kazi ya kujenga mwili na kukua
  6. CHAKULA hiki Ni laini sana na kitam kwa kuku na Mifugo yote (palatable)
  7. mmeng'enyo wa chakula hiki huongezeka kutoka 30% kwa CHAKULA cha kawaida hadi 95% kwa CHAKULA cha hydroponiki hivyo chakula kingi kutumiwa na mwili wa mifugo na kupunguza kinyesi na usumbufu wa usafisaji banda
  8. kinyesi hupungua na kuwa kati ya 5%-10% tu kwani CHAKULA kingi humeng'enywa na kutumiwa na mwili wa Mifugo
  9. mazao kama mayai au maziwa huongezeka kwa 40% kulinganisha na chakula cha kawaida.
  10. kiini cha yai la kuku anayelishwa hydroponic fodder huwa cha njano sana hata kama Ni kuku wa kisasa
  11. Hupunguza garama za ufugaji kwenye manunuzi ya chakula kwa 50-75% hivyo kuongeza faida.

  [​IMG]
  Banda la kuoteshea majani ya hydroponic fodder kwenye tray juu ya kichanja.

  [​IMG]

  Ng'ombe wakilishwa majani ya hydroponic fodder
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...