Geita: Nguzo ya umeme imeua mtu mmoja pamoja na ng'ombe mmoja

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Mtu mmoja amefariki Dunia Kwa kupigwa shoti ya umeme Mkoani Geita katika Kijiji cha Nyamarimbe jirani kabisa na Kamena.

Tukio Hilo limetokea jana (Novemba 7, 2023) ambapo kijana huyo (marehemu) alikuwa anaswaga ng'ombe mara baada ya kuona mmoja yupo chini kwenye nguzo ya umeme iliyokuwa imeanguka bila kujua alienda moja kwa moja kwenda kumshika yule ng'ombe ambaye nae alikanyaga zile nyaya za umeme na kupigwa shoti papo hapo. Alipomshika yule ng'ombe ghafla nae alipigwa shoti na kupoteza maisha palepale!

Tunaomba sana hasa TANESCO toeni Elimu kwa wananchi pindi mnapoweka hizo nguzo kuhusu hatari za umeme hasa pale inapotokea nguzo imeanguka. Pia nguzo zenu zinachimbiwa kiboya sana unakuta nguzo imeinama na kila siku mnapita hata kuifanyia marekebisho hamfanyi.

Njia ya kutoka Kakola Mgodini kwenda Karumwa (Msalala) kuna nguzo muda wowote zinaanguka lakini hamna habari.

Vijana wenu wa kazi wako busy kuimba matusi kutwa nzima walakini hawachimbi mashimo ya kina vitendea kazi hamna yaani jembe na sururu ili hali ardhi zingine zinahitaji machine ya kuchimbia mashimo badilikeni.

Imeniuma sana.
 
Back
Top Bottom