NGOMA ZETU: Mchiriku jamani, balaa...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NGOMA ZETU: Mchiriku jamani, balaa......

Discussion in 'Entertainment' started by Sikonge, Feb 7, 2011.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pana wakati nikiwa nimekuja kutembelea jamaa zangu pale Dar, nilialikwa na binamu yetu ambaye amezaliwa na kukulia Dar uswahilini na kashakuwa kama Mzaramo.

  Siku hiyo alikuwa anatoa wajukuu zake wawili (kutoa mwali) wali.

  Wapiga Mchiriku walikuwa wamealikwa siku hiyo. Ila hawa jamaa ni wapuuzi sana maana kila mwaliko wanachukua na kasheshe ni kuwa watafika saa ngapi kwako.

  Kwa binamu yangu walikuwa wafike saa 15 mchana ila wazembe wale wakaenda sehemu nyingine kwanza na wakaja zaa 18 jioni. Binamu yangu alikuwa kachukia sana na kuweka mkwara mzito (ndivyo nilivyoona mie) kuwa wakija atawafukuza.

  Mie na kijana mmoja tulichaguliwa kutoa wali hao wawili. Baada ya kuwatoa, nilikaa na huyo kijana na akaanza kuniambia tabia ya wapiga Mchiriku. Jamaa ni wazembe sana, wachelewaji na milele usiwaazime vyombo vya mziki maana hawajali kabisa chombo cha mtu hata chombo chao.

  Jamaa walipofika, wakafungua vyombo vyao harakaharaka, wakavuta waya wa umeme hadi ndani na binamu yangu muda wote anawaambia waondoke kwani wamechelewa na hana hamu nao kabisa. Wale jamaa hawakujali sana maneno yake na wakaendelea na shughuli zao kama vile hayupo.

  Ilipopita dakika tano, MCHIRIKU huoo .... " ehhh, kwa baba na mama ......."

  Kuangalia pembeni, namuona binamu yangu anaHAHA. Mwenyewe kaacha mchiriku, yuko pembeni na kajifunga GUNIA lake safi kabisa. Anaondoka Mchiriku kwa zile step za kuchezesha mabega, kubaraza miguu na kurukaruka huku akiangalia kushoto na kulia (MSONDO walikuwa wakaiga hii staili).

  Siku hiyo ilikuwa kama vile nimeletwa dunia nyingine kabisa kwa kuangalia vituko hivyo kwa mara ya kwanza. Funga kazi ilikuwa kuona mtoto wa mwaka na miezi kadhaa anayejifunza kusimama dede, alisimama kwa shidashida na kunengua step kadhaa za Mchiriku na akaanguka (miguu ilikuwa haina nguvu bado) ila mchiriku aliurudi.

  Toka siku hiyo, huwa nikiuona au kuusikia tu Mchiriku, mie lazima nipite hapo nifurahi kidogo vituko vya Wazaramo.

  Kuna mtu anaweza kunipatia habari za ngoma hii? Vyombo wanavyotumia vinaitwaje na kwa nini wanapiga Ki-Stool na kutumia vingoma vidogovidogo? Ni umasikini au uvivu wa Wazaramo?

  Kwa wale wapenzi kama mie, Mchiriku kadhaa nawawekea:  Kuna comments nimesoma zinasema "Kulikuwa kuna kundi moja wahuni wanaitwa Hisani hao walikuwa wakipiga ngoma ikisha unakuwa ushaiibiwa."
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwaka jana naona WALIINGIA hadi kwenye PIPA na kutua zao Ulaya.....

  Jamaa wako juu sana sana hawa. Ila hii Video inanimaliza jinsi HALIMA alizima kweli kweli...

  Walioko Copenhagen naona waliburudishwa sana sana na Kiduku cha Halima.

  Mwingine ni Daliki Moko ambaye Kinanda alikiweka kichwani muda wote ila bado alijua kinachoendelea jukwaani....

  Hivi ukiishi karibu na wapiga mchiriku, USIKU si ni BALAA????  Yo Yo, ukikamatwa na Halima, utanena kwa KILUGHA........... hahahaaaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  hao jagwa kwa mchiriku wanatisha ila baba yao ni omary omary aliyeanzisha kundi la atomic akitokea topaz.....kuna dogo mmoja aliwika sana kwa uchezaji wa mchiriku miaka ya 90 kila wanapopiga aidha topaz au jagwa lazma awepo!alifahamika kwa jina la KIBAKA MDUDU huyo mtu alikuwa hatari kwa uchezaji mchiriku na polisi wengi walikuwa wakimtambua kwani alikuwa spidi ya umeme kuzama mifukoni kwa raia wema
   
 4. s

  shosti JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kimbia, kimbia mbio mbio kibaka mdudu anakuja kimbia.....,sauti ya Omar Omary du kweli tumetokea mbali:msela:
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa Mkuu.

  Kibaka Mdudu ni hatari tupu kwani hilo jina tu tayari nimeshaanza kumuona akizamia mifuko ya watu.

  Bahati nzuri huwa napenda kuwaangalia nikiwa nimesimama mbali kidogo kwani huwa siwaamini sana na chezaji yao sifahamu wanavyocheza ila vituko vyao, hata kama nina hasira siku hiyo, itakwisha.

  Kuna hawa wengine nasikia wanaitwa HISANI, jamaa kaandika maoni yake YOUTUBE anasema:
  "Kulikuwa kuna kundi moja wahuni wanaitwa Hisani hao walikuwa wakipiga ngoma ikisha unakuwa ushaiibiwa."
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sasa watu wanaambiwa" KIMBIA KIMBIA, Kibaka Mdudu anakuja kimbia...." na wao bado wapo tu?

  Huyo jamaa asijekuwa huyu hapa kwenye Video, angalia dakika ya 6:00 maana jamaa anakatika si kawaida.

  Ila Halima hapo juu kwa kweli na yeye si Mbovu sana kwa Kiduku.......  Mcheki Dogo aliyepo dakika ya 6:00
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. s

  shosti JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mhh ndugu yangu,ahsante kwa hii video sikuwahi kuiona,wamechakachua mpaka mnanda kweli kazi,mauno ya kufa mtu kaka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Shosti,

  Nimeshangazwa Comments za watu wengi YOUTUBE kuwa badala ya kujadili Mchiriku, wanajadili Mnanda.

  Kwani Mnanda ni ngoma ya wapi tena? Mie hata sifahamu kipi ni kipi......... Mtu wa bara.

  Ngoja nikuwekee Video yao ya mwisho ya Sauti ya Busara. Naona walikuwa wakicheza jinsi ya kutongoza......

  Nawasifu kuwa wameenda hatua kadhaa mbele kwa kutoa SHOW na si kupiga tu ngoma.

  Dunia hii inabidi uwe mbunifu na kuchanganya mambo ili kupamba bidhaa yako iuzike kirahisi.

  Inaweza kuwa moja ya ngoma tunayo -EXPORT nje ya nchi kila mwaka. Kila la kheri kwa hili group.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. s

  shosti JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nafikiri mnanda na mchiriku ni kitu kimoja kama sikosei,labda unaitwa mnanda kwa kuwa kinanda kinachukua nafasi kubwa sana kwenye hii ngoma,labda niko tofauti kidogo maana nimeshtuka mpaka na uchezaji wenyewe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Shosti,

  Asante kwa jibu. Unaweza kuwa sawa kwa sababu ya Kinanda wanaita Mnanda....... Ngoja nikawaulize WAHAPAHAPA. Wanaweza kuja na jibu la uhakika sana maana kama sikosei ni Wakongwe wa mambo ya Mziki na Video moja wapo hapo juu ni yao.

  Ntaweka jibu hapa baada ya kupata jibu.

  *** Nimewaandikia na kuwaomba wanijibu au waje JF waandike jibu wenyewe. Huko kuna Mkongwe anaitwa KITIME.
  Jagwa Music naona wanatesa tena sasa hivi huko Zenji kwenye Sauti za Busara. Hongera zao.
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nasubiri jibu kwa hamu
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13. Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na
  kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.
  "tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki."

  Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  wakuu simchezo mmetukumbusha mbali.kibaka mdudu.

  Komandoo yoso nao wale wauni waliishia wapi sijui.
   
 14. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Halima,Halima zimaa ahhh!! duh si mchezo
   
 15. shejele

  shejele Senior Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hahahahaha, nimecheka hadi basi eti "zile step za kuchezesha mabega, kubaraza miguu na kurukaruka huku akiangalia kushoto na kulia " Sikonge wewe mwisho.
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  JAGWA MUSIC aka DEGE LA JESHI Kupeleka Mchiriku Denmark leo Sep 08, 2010 02:24 EDT

  Wasanii 8 kutoka katika kundi linalopiga muziki wa Mchiriku (Mnanda) wanaondoka leo tarehe 8 Septemba kuelekea nchini Denmark. Wakiwa huko kundi hili linatarajiwa kufanya maonyesho mawili katika miji ya Copenhagen pamoja na Roskilde. Ziara hii ambayo itakuwa ni ya pili kwao barani ulaya imeratibiwa kwa pamoja na kampuni za Jahazi Media na Maisha Music Tanzania Ltd.kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea link zilizopo hapo chini ya huo wasifu wao kwa kimatumbi:From the poor suburbs of Dar es Salaam, Jagwa Music play a style of music with chakacha roots known as mchiriku. Jagwa Music guarantees to set any concert venue ablaze with explosive performances that always keep the crowds jumping and bouncing from start to finish. Their stage show is unique a non-stop gymnastic workout choreographed with skill and sensitivity, combining theatrics, acrobatic prowess, a big amount of humour and energy. The group featuresminimal instruments including a hand-held Casio keyboard, drums, whistles and a battered old stool beaten with sticks for extra percussive flavour."Suddenly, we are all swept up in something so frantic its difficult to know whether to run or get pummelled into the sand. Its like walking into a monsoon. This is possibly the most outrageously thrilling spectacle in Africa today.

  JAGWA MUSIC aka DEGE LA JESHI Kupeleka Mchiriku Denmark leo

  SHOSTI: Hapo tumepata jibu. Mchiriku ni Mnanda na ina asili kwenye Chakacha.
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Sikonge,

  Tuletee na Mganda kama unazo pamoja na gombe sugu.
   
 18. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  HISANI pia walikuwa wanatisha sana walijulikana pia kwa jina la GARI KUBWA...kati ya mwaka 1992 au 1993 yalifanyika mashindano ya mchiriku pale CCM TEMEKE KATA YA 14 ambapo wakali wengi wa wakati huo walishiriki kama BUTI KUBWA toka maeneo hayohayo ya temeke...mashindano hayakumalizika kutokana na mashabiki wasiyokuwa na viingilio kulazimisha kutaka kuingia bure huku wakirusha vyupa...kuonyesha mahaba ya mziki huu hata wale waliotiwa mikononi mwanzoni na polisi kabla tifu hilo waliserebuka wakiwa na pingu mikononi..hakika ilikuwa fujo yenye kufurahisha.....
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Wakuu mmenikumbusha mbali sana late 80 na 90'
  Kuna Askari alikuwa anaitwa mkapa sharp na alikuwa na kundi lake la Salama Stars, hapo unanikumbusha mambo ya Wamizoga, Muddy Guy, Sure, na sio Siri hivyo vikundi ndio ulkuwa mwanzo wa KIBOKO MSHERI, KOMANDOO YOSO, NK
  mwisho wa ilikuwa ni Topaz
  tulikuwa maskani
  maskani kwa makuka
  kukaa kidogo kaja mtu
  kaja anatuuliza
  eti kipaka kafa saa ngapi
  watu wote tukashangaa
  tulikuwa hatuna habari

  HIVI KWELI MINANDA KAMA HIYO BADO HIPO KWELI?, UKIMTOA DOGO MFAUME
   
 20. G

  Gari New Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mchiriku mnanda na mdundiko..ni mule mule?..
   
Loading...