VERSE 1.
Alikuwa binti mzuri,
Enzi akiishi na babake,
Alipendwa sana,
Coz alimpata kwa shida,
Alipendeza kwa mavazi kila siku ukimuona,
Alivaa black shoes,
Iliyolandana na ngozi yake,
Sketi ya blue akimaanisha kuna bahari,
Blauzi ya kijani,
Kumaanisha hana jangwa,
Kitenge cha kujitanda, Kikawa rangi ya manjano,
Kwa makusudi akimaanisha,
Ana shehena za madini.
VERSE 2.
Binti kaanza kuchoka,
Dingike aliposepa,
Alipoenda kwa brother ruksa,
Akaachwa azurure,
Ndipo msala ulipoanza,
Historia ikaongezeka,
Alipoenda brother nche,
Utandawazi ukamtesa,
Na sera ya ubinafsishaji,
Kucha kapewa mchina,
Eti zing'are ka dhahabu,
Kumbe ranga alizopakwa,
Zilimuozesha kucha,
hayo ni baadhi,
Safari yake haikuishia hapo,
Utamuonea huruma,
Alipohamia kwa kaka smile,
Kageuzwa danguro,
Hata kwa jero tu unalamba,
Mvuto wa mavazi yake,
Na umaana wa rangi zake asili ukapotea,
Akapendwa na wa ng'mbo,
Wanamposa kwa bei che.
Alikuwa binti mzuri,
Enzi akiishi na babake,
Alipendwa sana,
Coz alimpata kwa shida,
Alipendeza kwa mavazi kila siku ukimuona,
Alivaa black shoes,
Iliyolandana na ngozi yake,
Sketi ya blue akimaanisha kuna bahari,
Blauzi ya kijani,
Kumaanisha hana jangwa,
Kitenge cha kujitanda, Kikawa rangi ya manjano,
Kwa makusudi akimaanisha,
Ana shehena za madini.
VERSE 2.
Binti kaanza kuchoka,
Dingike aliposepa,
Alipoenda kwa brother ruksa,
Akaachwa azurure,
Ndipo msala ulipoanza,
Historia ikaongezeka,
Alipoenda brother nche,
Utandawazi ukamtesa,
Na sera ya ubinafsishaji,
Kucha kapewa mchina,
Eti zing'are ka dhahabu,
Kumbe ranga alizopakwa,
Zilimuozesha kucha,
hayo ni baadhi,
Safari yake haikuishia hapo,
Utamuonea huruma,
Alipohamia kwa kaka smile,
Kageuzwa danguro,
Hata kwa jero tu unalamba,
Mvuto wa mavazi yake,
Na umaana wa rangi zake asili ukapotea,
Akapendwa na wa ng'mbo,
Wanamposa kwa bei che.