Tuyasikie ya miss Tanzania

Tuyasikie ya miss Tanzania

MC Chere

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
586
Reaction score
400
Alikuwa binti mzuri,enzi akiishi na babake,alipendwa sana coz alimpata kwa shida,gauni la bluu mwilini mwake lilifana,kiatu cheusi kikapamba urembo wake,na kilemba cha njano kichwani kikawekwa,akajisitiri na baridi kwa koti la kijani,wageni wengi walimpenda ikawa vipi wamfaidi.

Babake kafariki,akahamia kwa kakake RUKSA,Na RUKSA alipozeeka akahamia kwa brothe NCHE,hapa aliishi kwa shida kwa sera za ubinafsishaji,mchina alipata tenda ya kumpaka kucha rangi,kumbe rangi alizopakwa,zilimuozesha kucha,Akaona akimbie akaenda kwa kaka SMILE,hapa akageuzwa danguro hata kwa jero tu unapiga,imani ikampotea haoni wa kumsaidia,Aliporudi kaka POGBA akajawa na matumaini,misimamo ya kaka POGBA,akaiamini kuwa ni bora,sasa mwaka umekatika uso wake umepauka,imani aliyoiweka imegeuka kuwa shubiri,kadri siku zinavyoenda ndiyo anahisi kifo kikaribu,kwa ahadi tamu anazopewa,ni za fisi kusubiri mkono uanguke,tayari ameshaanza kumkumbuka kaka SMILE,maana pamoja na alichofanywa bado aliishi kwa raha.SASA ANASOMA HERUFI.

Pole MISS
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom