ngoja niwape kastori ka kulalia

ngoja niwape kastori ka kulalia

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
20,997
hapo zamani za kale palikuwa na mti mmoja mkubwa sana ili kuukumbatia unahitaji watu watano warefu! sasa mti huo ukatokeza matawi na tawi moja likawa kubwa sana ukubwa wake ukiwa nusu ya ya mti wenyewe. sasa tawi hilo likawa linatoa maua ambayo nayo yanatoa matunda, matunda hayo yakidondoka yanaanza kuchipusha miti mingine, pia tawi hilo lilikuwa limebeba matawi mengine mengi na makubwa. siku zilivyoenda tawi hilo likaanza kuwa na majivuno na kuanza kujifananisha na mti uliolibeba maana halikuona tofauti maana wote wana matawi, wote wantoa maua na wote wanatoa matunda. baada ya kibiri kuzidi mti ukaamua kulikatia maji na virutubisho toka udongoni! maskini tawi lenye kiburi likafa kwa majivuno yake.
meaning: binadamu tunapokuwa na hela, umaarufu na kufanikiwa sana maishani tunaanza kusahau mungu wetu kama tawi lililoanza kudharau mti
 
Duh bora ningelala zangu!kumbe kastori kenyewe ni hako?Anyway usiku mwema
 
huo mfano hadi kwa totos wanaopata kiburi kwa pesa za madume....mrija ukikata mambo yanakuwa .............
 
Kwel binadamu hatufanan,mim nafikiria hela sijala jamaa anafikiria kulala looh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom