Ngoja niropoke

Ngoja niropoke

..
Screenshot_20220921-213834_Twitter.jpg


Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Takwimu zinaonesha Wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA), kwa mwaka unapokea maombi ya talaka yasiyopungua 500+ Tanzania nzima.

Kilichonishangaza ni kwamba asilimia 78% ya Ndoa zinazovunjika ni wanawake ndio wanaoomba talaka na kupeleka maombi hayo.

Kilichonishangaza na Kunimaliza zaidi ni kwamba asilimia 89% ya wanawake wanaoomba talaka ni WANAWAKE WASOMI (Intellectual Women)

Swali; Wanawake wasomi wana SHIDA GANI, kwanini kwao talaka ziwe nyingi, kwanini wengi wanasumbuka na mahusiano na kwanini wengi ni single mothers?

Honestly kuna kitu hakiko sawa kwa hawa Intellectual women, kwa takwimu hizi tunaweza kusema elimu zimewaharibu badala ya kuwatengeneza wawe wake bora.

Ndio, haiwezekani asilimia 89% ya maombi ya talaka yakaliwe na wao pekeao, ina maana elimu zao zinawaambia kwamba solution pekee ni talaka, nawaza sana yani

Ngoja niropoke; wanawake wengi wasomi wana kakiburi ka maarifa kanaitwa "INTELLECTUAL ARROGANCE"

Haka kakiburi kanawaambia hivi "wewe ni msomi, una akili, unajiweza na mwanaume hatakiwi kukusumbua kwa lolote lile"

Haka kakiburi kamewafanya wengi washindwe kuwa wanyenyekevu kwa sababu wanajiona ni classy and high, inafika hatua wanaanza kuvimba.

Wengi walifanikiwa sana kielimu kiasi cha kupata fedha, vyeo na status katika jamii vichwa vikaelemewa sifa na kujiona wanajua na kuweza kila kitu.

Pengine ofisini kwao yeye ndo Managing Director na ana watu wengi wakiume wako chini yake kikazi, anataka na mumewe awe chini yake pia.

Elimu yake, cheo na fedha vinamwambia "Unastahili kunyenyekewa na sio kunyenyekea na unaweza kila kitu" wengi hapa ndipo wanapofeli sasa na kuleta mabalaa.

Pengine walipokuwa wanasoma waliambiwa maneno kama "Soma sana, tafuta fedha zako ili mwanaume asikusumbue kwa lolote lile" (hii ndo shida kubwa)

Kwahiyo wengi kuanzia hapo wakawa wanatembea na competetive mentality (fikra za kishindani) na muda wote wapo kinyume na jinsia ya kiume.

Kinachotokea, wakiolewa wanafanya mambo kama washindani (competetors) kwa wanaume wao na sio wapambanaji wenza (teammates)

Kitu kingine kinachowaharibu ni hizi FEMINISTS MOVEMENTS (harakazi zinazodaiwa kumpa nguvu mwanamke na kumkomboa kifikra)

Ukizifuatilia vizuri hizi harakati zinawafanya wanawake wahisi kwamba hata wao wanaweza kuwa kama wanaume since they can pay bills na ada za watoto.

Sikatai, ni kweli kabisa kuna majukumu mwanamke anaweza kuyaperform kama mwanaume lakini haitatokea hata siku moja akawa kichwa cha familia.

Elimu walizopata wengi wao zimewasababishia kakitu kanaitwa "Control Freak Disorder" (unajua ni kanini haka, soma hapa chini)

Ni kale ka akili ka kumtaka mwanamke amcontrol mwanaume na kumfanya mwanaume aenende vile mwanamke anataka (amuweke chini)

Na hii inatokana na ukweli kwamba wengi wameweza kuongoza kakundi ka watu, wengi wameweza kufanya vitu vikubwa katika academic fields zao.

Kitendo cha kufanikiwa kuongoza kakundi ka watu kinawafanya hata kwenye ndoa nafasi ya kuongoza ambayo ni ya mwanaume aitake mwanamke, yaani yeye ndo awe kichwa.

Msuguano unaanzia hapo, mwanaume yeyote yule anataka yeye ndo awe top, ikitokea mwanamke akataka kumshusha mwanaume ili mwanamke awe top balaa linaanza.

Fuatilia, wanawake ninaowazungumzia hapa wengi wana kakiburi, wanajiona, na wanaamini kwamba hakuna kitu wanahitaji kutoka kwa wanaume na wanaweza kila kitu pekeao.

Wanaume wengi wanatafuta fedha ili wahudumie familia zao na kuwatimizia mahitaji, ila kwa wanawake mambo yako kinyume kabisa!

Wengi wanasoma na wanatafuta fedha ili waweze kuthibitisha kwamba wanaweza kufanya kama wanaume, wanaweza kuishi bila wanaume na hawawezi kusumbuliwa kwa lolote.

Ndio maana, kukiibuka kaugomvi kadogo wengi solution inakuwa ni kuachana ili kuthibitisha kwamba "NINAWEZA KUISHI MWENYEWE NA KAMA NI MTOTO/WATOTO NITALEA COZ NINA FEDHA"

Dear ladies, black brother wenu nawakubali kinoma na nafurahi kuwaona vile mnastrugle kupambania ndoto zenu (hongereni kwa hilo)

Lakini, jitahidi kadri uwezavyo fedha zako, elimu yako na cheo ulichonacho/utakachopata visikutie Kiburi mbele ya mumeo uliyenae/utakaekuwa nae.

Ni kweli umefanikiwa kielimu, pengine una mshahara mkubwa, au biashara zako zinaenda safi, una cheo/position fulani somewhere lakini WEWE BADO NI MWANAMKE.

Wakati wowote uwapo mke, mpe nafasi mwanaume awe mume, awe baba, awe kuongozi, awe dereva wa familia huku wewe ukiwa kwake msaidizi.

Hata kama ofisini kwenu una wanaume wengi unaowaongoza na wananyenyekea mbele yako usitake na mumeo akunyenyekee..

Mpe yeye nafasi ya kuwa king, mtii, msikilize na panapohitajika ushauri mpe ushauri kwa upole huku ukionesha kwamba unamuheshimu na kuamini..

Kwanini wanawake wa sahivi wamesoma lakini hawadumu kwenye ndoa kama mama na bibi zetu walioishia darasa la nne/la saba.

Kadri mwanamke anavyoanda juu kielimu, kuna namna anapoteza WIFE TRAITS umakini unahitajika sana ndo mana wengi wanabaki single/single mothers.

Fuatilia wanawake woote unaowajua Tanzania ambao wana vyeo vikubwa, wamefanikiwa kibiashara au wapo top kwenye eneo lolote lile.

Wengi utagundua kwamba hawajawahi kuolewa, waliolewa wakaachika, walizalishwa na wakabaki hapo.

Elimu sio mbaya, fedha sio mbaya..lakini inakuwa mbaya pale inapoanza kumfanya Quuen atake kuwa king, haiwezekani!

[Nimemaliza kuropoka

Credit: WhatsApp forwarded msg
Author: Unknown
Kaka mkubwa mliambiwa ishini nao kwa akili, tatizo wenye elimu ya kawaida wanaume huwa wanawadharau wanataka wale wanao ongea nao kidhungu sasa pambaneni na hali zenu
 
Dear ladies, black brother wenu nawakubali kinoma na nafurahi kuwaona vile mnastrugle kupambania ndoto zenu (hongereni kwa hilo)

Lakini, jitahidi kadri uwezavyo fedha zako, elimu yako na cheo ulichonacho/utakachopata visikutie Kiburi mbele ya mumeo uliyenae/utakaekuwa nae.

Tutaruka nao hivyohivyo watakavyo wewe waache.

Kwanza hiyo inatupunguzia Msalaba na inafurahisishia kuwatumia Kwa wengi Kwa wakati mmoja.

Kwa sasa mambo yamerahisishwa Sana.
 
Tatizo lenyewe kabisa

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app

Na wenyewe watalipuuza kuendekeza ubabe wao. Na wamesahau kwamba huyu mke anayelalamikiwa leo ndio huyu anayewalea watoto wao wa kike.

Imagine huyu mtoto wa kike mwenye miaka 6 sasa hivi abahatike kusoma kufikia degree ya pili miaka 20 ijayo.
Aje kuolewa na mwanaume mwenye mentality ya kiafrika asiyetaka kubadilika kama ndugu yangu Mshana Jr .
Balaa lake si la kitoto.
 
Share ili tujifunze.
Watu tunakosea sana kuchagua wenza, tukitegemea tutawabadilisha lakini kuna tabia hazibadiliki kamwe.

Kuna mtu kaoa binti matawi ya juu, kasoma...kwao wafanyakazi kibao, hajui kunyenyekea kamleta mgombani huku...
Akitegemea mke awe mke kweli na hata asiajiriwe.
Why kupotezeana muda...ipo wazi kabisa hawaemdani halafu anataka abehave kama mke wa kijijini asiyesoma. Hili litawezekana vipi?
Mume mwenyewe wa kizamani mwenye mfumo dume hasa. Nani anataka?
Inawezekana sana tu, nina Rafiki zangu zaidi ya 6 waliwaachisha Ke zao kazi wanaishi vizuri tu na hadi sasa wameshawini sana kiuchumi wakiwa na Watoto wao.

NB:

MAISHA HAYANA KANUNI ILA YANAHITAJI NIDHAMU SANA.
 
Duh! Me nataka wao ndo walalamike ndo nitaamini inawa-affect nje na hapo ni kiherehere chetu kuoa.
 
kwenye hili bandiko...kila mtu abebe mzigo wake tu...hakuna cha msomi wala asiye soma...tena bora mwanamke aliyepiga kitabu...yaani kwanza hamna hata aliye bora....kila mtu afe na mzoga wake...nimemaliza.
 
Mshana Jr naomba uanze kuukubali ukweli hata siku moja kichwa hakipaswi kuhama sehemu yake ya kuwa juu na kishuke chini kiwe sehemu ya shingo au hata kuwa miguu, Sasa basi ukizaliwa mwanaume tayari wewe ni mtawala upo juu na uwe kwa vitendo juu na usitengeneze mazingira ya kuwa miguu yaani ubebwe na ni mpango wa Mungu uwe kichwa, sasa jamii imebadilisha kichwa kimechoka kuu juu kinataka msaada angalau kiwe sawa sawa na kiwiliwili au miguuni kabisa Sasa basi kwa vile umegeuka kiwiliwili basi inabidi kuwa mpole Ili gurudumu liende, hata zamani ilipotokea hivyo kichwa kilikuwa kipole maisha yakaendelea mfano yule kijana aliyekuwa na uchumi mbaya na mke anahitaji na muda umefika wa kuoa alikubali kutumika kwa baba mkwe bila hiyana maisha yakaenda.

Viumbe wa kike wao wamepewa jukumu lao la kuleta viumbe huku wakihudumiwa na baba watoto na ikitokea wameweza na majukumu mengine ya kichwa basi hiyo ni hatari maana walionekana wao siyo kuoa na kutunza na mume Bali watataka watoto tu na ubini wa baba kwa watoto wao na kulea watalea wao, hivyo kwa vile mataifa mengine yashajifunza kwenye hili na kujiandaa haya Mambo hayawapi shida tena ni mwendo wa kubadilika tu, swala la mapenzi au ndoa liwe la kuelewana tu ikitokea hamuelewani Kila mtu achukue njia yake ila swala la malezi liwekewe Sheria ya malezi, kingine wake kwa waume wajulishwe mapenzi au ndoa siyo sehemu ya kujipatia uchumi kama uchumi Kila mtu atengeneze wake na aonyeshe jinsi anajithaminisha, kingine mtu asiingie kwenye mapenzi au ndoa kama kilema au mgonjwa hayo yafanyike wakati kama love moment na siyo kama Sheria yaani mazingira yajengwe ya watu kujihudumia kwenye mambo ya maisha kama kupika, kufua, kuosha vyombo yawe mambo ambayo mtu anayejiita mtu mzima ajue kujifanyia na mapenzi yawe mapenzi tu huku mambo ya maisha kwa Kila mmoja yakiendelea, Sasa hao wasomi watatunza ndoa maana hazitawachosha.
 
Back
Top Bottom