Ngeleja kupokelewa Kifalme!!

Ngeleja kupokelewa Kifalme!!

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.
 
Bado ni mbunge wa sengerema, wao wana sengerema kama wanaendelea kumuona anawafaa wasije kulalamika kuwa hawapati maendeleo, hapo kila mtu na jimboni kwake aamue nani awe kiongozi wao. Na hiyo ndiyo democracy, ila kitaifa hakutufaa sasa kazi kwenu wanasengerema damu yake ipo mikononi mwenu, mkitaka fanyeni alichofanya Pontio Pilato alipotoa hukumu kwa Yesu.
 
kutakuwa kuna mpunga tu!! acha na mm nikafinye kisha niondoke!!!
 
Ameandaa pilau nini? Maana wanachama wa ccm kwa pilau huwawezi wapo radhi wasafiri toka dsm mpaka segerema
Haukosekani, c unajua hicho ndcho kshawishi pekee kilichobakia cha kuwavuta WanaCCM kuhudhuria mikutano.
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Wana haki ya kumpokea kishujaa. Kuna hotuba moja Mama Kilango aliitoa Bungeni akisema hataki kununuliwa chai na Ngeleja akasema Waziri anapeleka umeme kwenye vijiji 6 kwenye jimbo lake wakati wananchi wa Same hawana umeme. Hivyo si ajabu huenda Sengerema imejaa umeme.
 
Acha majungu mkuu!
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Kumwandalia mapokezi mtu anayetuhumia kwa ubadhilifu wa raslimali za nchi ni ushabiki usio na maana.Wananchi tunapaswa kushikamana na kuwakemea wale wote wanaofanya vitendo vya kuihujumu nchi yetu hata kama ni 'wenzetu'.
 
Inatakiwa M4C nao wawemo kenye mkutano ili wampe ujumbe laivu kwamba ni gamba
 
kule sengerema ngereja hapendwi kabisa narudia hapendwi kabisa..na mwaka 2015 wala asijaribu kugombea hata yeye analijua hilo tena vizuri kabisa..

siku ile wakati Lema na Slaa wako hapo sengerema huyuhuyu ngereja alimwambia mkurugenzi wa wilaya aitishe kikao na madiwani wote lengo lilikuwa ni kwamba wale madiwani wa ccm wasiende kwenye mkutano na chadema....hata walipofika kule kwenye kikao walikoitwa hakukuwa na kikao wala nin badala yake walifungiwa ndani ya ofisi hadi mda wa mkutano wa chadema ulipoisha..

hayo mapokezi atakayofanyiwa hiyo kesho ni njama za magamba ili aoniekane bado anaweza na anapendwa...hapendwi kabisa kuanzia kijijini kwako bitoto, kalangalala, igulumuki,buyagu, nyancheche,nyanzeda,busulwangiri,busisi,nyampande kote huko watu wamevaa magwanda na wanaifagilia chadema sana....
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Asubiri PINGU tu huyo ...
 
huu ndiyo mwisho wa safari ya kisiasa kwa William Ngeleja ... asitegemee kurudi tena kwenye baraza la mawaziri katika maisha yake ..pia come 2015 hata ubunge ni patapotea kwake ...hili ndilo kosa linalofanywa na watu wengi wanaodandia uongozi pasipo kuwa na utashi nauwezo .... uongozi ni "Charisma"
 
Kweli nchi inaenda kombo. Wana-Sengrema kumkaribisha Ngeleja aliyeshindwa kuongoza wizara kama shujaa inashangaza!. Hivi Wasukuma wameanza lini kuwapatia taji la ushindi na kuwafanya mashujaa watu waliowasaliti vitani?

Huyu Ngeleja anatuzuga tu. Yeye mwenyewe kaandaa sherehe hizi, watu aina ya Ngeleja ni jadi yao kuhonga. Atashindwaje kutumia sehemu ya fedha alizoiba kufanya sherehe ili aonekene msafi. Huyu anaogelea ndani ya bwawa la maji taka. Anazidi kuuthibishia umma kwamba kaiba za kutosha.
HONGERA Ngeleja. Bhebhe wabhubhi gete gete.
 
Wajameni huyo mtu hataa huo ubunge si alipewa na R ili amtumie kwenye ishu zake sasa kazi hana tena nani atampakata 2015, kwishnei.
 
Nina uhakika hayo mapokezi atakuwa amejiandalia mwenyewe na ghalama zote zitakuwa ni za kwake, ni kama alivyo fanya Mzee wa Vijisent kujiandalia mapokezi, Hata mzee wa Monduli nae alijiandaliaga mapokezi baada ya kujiuzulu UWAZIRI MKUU
 
Ila akumbuke kumuomba radhi yule askari mlinzi aliyemfukuzisha kazi pale Harbour View!

Nadhani yule mtanzania mwenzetu atakuwa amepata amani ya moyo baada ya huyu fisaditembo kurambishwa mchanga!!!!!!muosha huoshwa!

Ndugu zangu wa sengerema kumpokea kifalme ngereja ni yale yale ya fisadi vijisenti ambaye aliangusha ng,ombe kila alipokatiza wakati anapokelewa kwao mkoa mpya.
 
Back
Top Bottom