Ngeleja kupokelewa Kifalme!!

Ngeleja kupokelewa Kifalme!!

Nafananisha hili na Mtu kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe!Cost za show born from Ngeleja himself!

Hapo alitemwa wanajianda kumpokea hivyo kama angejiuzu ndo wangempokea kama mfalme! Akili ya mbongo bana inamtosha mwenyewee!
 
Ile laana ya yule mlizi itamtafuna hadi mwisho,sidhani kama anaweza fikiria adha ya familia ya mlizi yule baada ya kufukuzwa kazi,sitashangaa akiishia gerezani,mbya sana kuwaonea wanyonge kwa kuwa tu wewe una nafasi fulani

Mkuu hii ya mlizi imekaaje maana sikuipata embu fanya kufunguka zaida
 
kwa ufupi wamemshushua jk kwamba amekosea kumfukuza uwaziri. mi nadhani hawa majambazi walitakiwa hata ubunge wafutiwe. sasa huko bungeni anaenda kuongea a nini? hii nchi inachosha 2015 ifike tuseme nao kwenye masanduku ya kura.
 
Vipi, jimbo la sengerema limeendelea kiwango gani. Kwa vile kazi ya uwaziri imemshinda, ninadhani kuwa huenda kazi ya ubunge aliifanya vizuri. Niliwahi kusikia jamaa huyu akizuia ndege isiondoke Airport Mwanza kumsubiri hadi atoke Sengerema. Mheshimiwa Ngeleja alikuwa na matatizo fulani ya kutaka kuabudiwa kwani kila mara alikuwa anataka watu wamtambue yeye ni nani halafu wafanye anavyotaka yeye; alimfukizisha kazi mlizni wa benki kwa jambo dogo sana, na aliwahi kutishia mapailoti wa ndege za kibongo wasifanye kosa la kumwacha Mwanza awapo safarini hata akichelewaje.

bwana utanisababishia ban buree napatwa hasira na hy fisadi
 
Ndio tatizo letu watanzania,vibaka tunawachoma mto,lakini mtu akiiba mali ya umma amnaonekana shujaa,sasa wanampokea hivyo kwa kizuri kipi alichowafanyia watanzania.Tatizo ili naona liko kwa wasukuma nadhani ni kwa ajili ya elimu duni,nakumbuka hata mzee wa vijisenti walimpokea hivyo,mbona mawaziri wa mikoa mingine wailong'olewa hatujasikia mbwembwe kama izo?
 
watu wa ukanda huo sijui wana tatizo gani maana hata chenge alipopigwa chini alipokelewa kishujaa! mnapokea wezi kishujaa?? fungukeni nendeni na kasi ya m4c!!
 
Hapo ndipo napodhani CCM ingekuwa inaingilia kati na kuzima mienendo hii. Bila shaka hao wanaoenda kumpokea ni mkusanyiko wa wanachama na washabiki wa chama. Haipendezi! Rais na mwenyekiti wa Chama keshamuengua mtu kwa utendaji mbovu, halafu yeye anaaenda kupokelewa kishujaa jimboni? (Lowasa, vijisenti na sasa huyu). Ni kauli ya dharau (snub) kwa mwenyekiti na hata wabunge waliochachamalia uozo serikalini. Inazidi kushusha hadhi ya uongozi ndani ya chama.
 
Vipi, jimbo la sengerema limeendelea kiwango gani. Kwa vile kazi ya uwaziri imemshinda, ninadhani kuwa huenda kazi ya ubunge aliifanya vizuri. Niliwahi kusikia jamaa huyu akizuia ndege isiondoke Airport Mwanza kumsubiri hadi atoke Sengerema. Mheshimiwa Ngeleja alikuwa na matatizo fulani ya kutaka kuabudiwa kwani kila mara alikuwa anataka watu wamtambue yeye ni nani halafu wafanye anavyotaka yeye; alimfukizisha kazi mlizni wa benki kwa jambo dogo sana, na aliwahi kutishia mapailoti wa ndege za kibongo wasifanye kosa la kumwacha Mwanza awapo safarini hata akichelewaje.

acha uzushi na usengeusenge,hilo ulilipata wapi? Mijitu mingine bana,jf unaiharibu kwa udaku.
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Kama kawaida mtaji wa wajinga
 
Back
Top Bottom