Ngeleja Apita bila kupingwa kura za maoni Sengerema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja Apita bila kupingwa kura za maoni Sengerema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Malafyale, May 6, 2010.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimebadili utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge na udiwani kwa kuruhusu wanachama wao wote kupiga kura za maoni, uongozi wa chama hicho wilayani Sengerema, mkoani Mwanza umewapiga chenga wafuasi wao na kumpitisha mbunge wa Sengerema Mjini, Bw. William Ngeleja kuwa mgombea pekee katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  Uamuzi huo umetangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa wa CCM wilayani humo, Bw. Masumbuko Bihemo, alipozungumza na waandishi wa habari jana, akitanabaisha kuwa hatua hiyo ilifikiwa na Halmashauri kuu ya CCM wilaya kilichokutana Mei Mosi mwaka huu.


  Alisema kutokana na utaratibu uliowekwa na chama hicho, kikao Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ndicho kikao cha juu na chenye mamlaka katika kubaini viongozi wanaotekeleza shughuli za chama kama inavyotakiwa.

  Hata hivyo, uamuzi huo unapingana na maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iliyoketi Dar es Salaam Aprili 8, mwaka huu na kuamua yafuatayo kuwa: "(NEC) imesisitiza juu ya utaratibu mpya wa kura za maoni kwa wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani kwamba kura za maoni zitapigwa na wana CCM wote kwenye matawi yao kwa masharti matatu; "Kwanza mwanachama awe amejiandikisha katika daftari la wanachama tawini, pili awe na kadi ya CCM iliyo hai (iliyolipiwa ada) na tatu awe amejiandikisha katika daftari la wapiga kura na awe na shahada."


  Pia maamuzi ya viongozi hao yanakwenda tofauti na tarehe iliyopangwa ya kura za maoni ambayo ni Agosti 8, mwaka huu kwa matawi yote nchi nzima.


  Lakini katibu huyo alibainisha kuwa uamuzi wao wa kumpitisha Bw. Ngeleja umeanzia katika ngazi za matawi, kata na kuzishirikisha jumuiya za chama ikiwamo ya vijana (UVCCM) na wazee wa chama hicho na wote walitoa mapendekezo ya kutaka mbunge huyo asiwe na mpinzani.

  Alisema sababu pekee iliyowavuta na kufikia uamzi huo ni juhudi za mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini za utekelezaji ilani ya CCM na kuwatumikia wapiga kura wake ipasavyo.


  My take:

  Kamati kuu ya CCM ilitangaza kura za maoni ndani ya chama hicho ni mwezi August mwaka huu,iweje sasa Ngeleja awe kapita tayari tena bila kupingwa ili hali bado haujafika hata muda kisheria wa kila mwana CCM kuchukua fomu na kugombea kwenye jimbo hilo?
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mhhh kwa hiyo?
   
 3. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii itazua tafrani sana!!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tena hiyo ndiyo safi sana!!!

  cha maana ni wapinzani kuungana na kumtokomeza nduli huyu wa demokrasia kwa umoja wao!!!

  wekeni mgombea mmoja, na hao wa CCM waliokua wanatamani hicho kiti wakribisheni muunganishe nguvu

  Tanzania bila upuzi, inawezekana
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kama ni tafrani itakua ni ya kujitakia... wananchi wanajua wanachoiaka!!... hivi angekua magufuli tungelalamika?
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Malafyale kama wewe ni Deep Green inakuhusu ila majority ya JF member wanakerekwa na maduduz ya Deep Green, labda uiforward hii issue kwa Makamba na Tume yao ya Uchaguzi
   
 7. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Chanzo ni ni kipi isije kuwa magazeti ya RA bosi wake wa zamani Vodacom
   
 8. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45

  Source Tafadhari tuwekee isije kuwa imeandikwa na magazeti ya Bosi wake wa zamani Vodacom RA
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wameshaanza kampeni. Afu mwisho wa siku wanasema wameshinda kwa Kishindo!
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  These insanes are still existing? Mbona kijana huyu anajidhalilisha hivi,does it mean that he cannot stand competition? This is another Tyrannical move,it's disguisting...
   
 11. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tuwa source................
   
 12. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I don't think this is true!!
   
 13. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Chanzo cha habari hii ni;
  Gazeti la Majira;tarehe 5/5/2010
   
 14. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  kiwalani,
  Chanzo cha habari hii ni gazeti la Majira la tarehe 5/5/2010
   
 15. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ni upuuzi mkubwa, inaonekana hao viongozi wa ccm wa Sengerema uelewa wao ni mdogo. Hawana haki yeyote ya kikatiba kuzuia wanachama wengine kugombea nafasi za uongozi. Kwanza kumtangaza kuwa mgombea pekee kabla ya muda kufika ni batili na hiyo ni dalili kuwa Ngereja kawanunua ili waanze kuweka kauzibe kwa wana ccm wengine, inaonekana Ngereja hajiamini kama anaweza kushinda. Viongozi wa ccm Sengerema acheni huo ujinga na upuuzi wenu, kama mehongwa hiyo hongo itawatokea puani.
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huu ni utaratibu wa ajabu kidogo kwangu labda kama ndivyo taratibu za CCM zilivyo. Lakini utasemaje amepita bila kupingwa wakati hata mchakato wa uchaguzi haujaanza. Wanajuaje kama katika siku zijazo mpaka kufikia nomination hawatajitokeza watu wakachukua fomu na kugombea? Au tuseme watawazuia na kuwanyima fomu kwa vile tayari wameshautangazia umma juu ya yule wanayedhani anastahili kuendelea kukalia kiti? Nina hofu isije ikawa ni mbinu chafu inayotokana na desperation ya kutotekeleza ahadi alizoziweka maana kama mtu amefanya vema jimboni rekodi yake itamlinda hata wakijitokeza watu 100 kugombea. Ifike mahali watu waache siasa chafu. Naamini kama tangazo hili lingetotlewa 2005 yeye alipoamua kugombea basi leo asingekuwa hapo alipo!
   
 17. M

  Mchili JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Rushwa hizo. wanataka kukatisha tamaa wengine na huo ni mtandao wa RA
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Iko kazi
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hii ndio sisi m.
  Tukisema huwa viongozi wao wengi hamnazo wanasema twatukana.
  Lakini ndivyo walivyo. Alafu utegemee lolote humo? Haya ndio matunda yao wenyewe wanaita ndio wenye chama.
   
 20. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mongoigwe,

  Mbona unakuwa kama mtu ambaye hajaenda shule..

  achana na mambo ya speculation..
   
Loading...