mbasajohn
JF-Expert Member
- Mar 14, 2009
- 247
- 39
Nakumbuka waziri wa nishati na madin Mh. William Ngeleja siku alipokuwa akiwasilisha bajeti yake kwa mara ya pili alitamka kuwa "unafuu wa umeme unao onekana kwa sasa nchini unatokana na kuanza kwa kutekelezwa kwa mpango wa dharula hasa kuongezeka kwa uzalishaji wa Agreco kutoka MGw 20 mpaka 100".
Lakini cha kushangaza siku mbili tu baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo mgao umeongezeka kasi na kuwa maradufu sehemu nyingi hapa Tanzania, mfano Sikonge Wilaya mojawapo ya mkoa wa Tabora mgao kwa sasa ni usiku kwa usiku yaani wanakata saa moja asubuhi na kurudisha saa tano usiku kila siku toka bajeti hii ipitishwe, kabla ya hapo mgao ulikuwa kwa either kuanzia saa 3 asubuhi na kurudisha saa 10 jioni au wanakata saa 10 jioni na kurudisha saa 5 usiku.
Hali hii imejitokeza kwa jiji la Mwanza ambapo umeme umekatika kwa siku tatu mfululizo baada ya bajeti ya ngeleja kupata baraka za mjengoni. Sasa kwa hali hii Ngereja anaposema kuna unafuu anamaanisha unafuu upi ikiwa hali inazidi kuwa mbaya kama si kuwadanganya waheshimiwa ili wapitishe bajeti yake? au siku hizi mawaziri kusema uongo ndio sahihi badala ya kusema ukweli. Kama kuna sehemu unafuu umeanza kupatikana naomba tujuzane ili tuamini maneno ya Ngereja.
Naomba kuwasilisha.